Hatua za kufuata ili kujenga uaminifu katika jamii

Jamii Africa

Ukikosa uaminifu huwezi kuwa na mahusiano mazuri na watu

Je watu wanaokuzunguka wanakuchukuliwa wewe kama mwaminifu na mkweli? Mtazamo wako kwa watu wengine ukoje? Uaminifu ni tabia inayojenga heshima, upendo na mafanikio katika jamii.

Wakati mwingine unajiuliza kwa nini mimi siheshimiki lakini fulani anathaminiwa na kupewa heshima. Sababu ni moja tu wewe sio mwaminifu katika yale unayokubaliana kufanya na wenzako iwe ni kazini au katika biashara.

Fuata hatua zifuatazo kujenga uaminifu kwa jamii:

 1.Uwe mkweli

Hatua ya kwanza kujenga uaminifu ni kuwa mkweli

  • Sema kweli daima. Epuka kudanganya hata katika mambo madogo.
  • Washirikishe wenzako taarifa za ukweli hata kama zinaweza kusababisha hasara kwako. Usisambaze taarifa ambazo hazijathibitishwa.
  • Usiibe wala kuchukua kitu kisicho chako bila ruhusa ya mwenye nacho.

2. Fanya Maamuzi Sahihi

Hatua ya pili ni kufahamu wakati upi uwashirikishe wengine taarifa na wakati upi ukae kimya.

  • Linda faragha ya rafiki yako. Usitoe taarifa za mtu binafsi kwa wengine ili kumuharibia heshima yake katika jamii.
  • Fikiria mara mbili kabla ya kutoa hukumu/maamuzi juu ya mtu fulani ili kuepusha kumdhuru mtu asiye na hatia.
  • Usitarajie kuomba msamaha kutafuta mabaya yako. Utasamehewa lakini kila utakapoonekana mbele ya macho ya watu watakumbuka mabaya uliyotenda.
  • Upuka mazungumzo ya siri ukiwa katika kundi la watu. Zungumza kwa uwazi ili wengine wasikie kuepusha hisia hasi.

 

3. Uwe na Msimamo

Hatua ya tatu ni kuwa na msimamo katika maneno, tabia na matendo. Haitoshi kuwa mwaminifu kwa kipindi au mazingira fulani lakini uaminifu ni muda wote na mahali popote.

  • Simamia kile unachokiamini
  • Fanya kazi; timiza malengo, masharti vigezo vilivyowekwa katika kazi uliyopewa.
  • Tenda unachosema. Timiza ahadi kwa wakati, epuka kuwa na ndimi mbili.

4.Kuwa mkweli kwa mawasiliano ya vitendo

Viungo vya mwili vinaongea zaidi kuliko maneno. Maneno unayongea yashabiane na muitikio wa viungo vya mwili kama mikono, uso n.k. Kuongeza uaminifu kwa kutumia viungo vya mwili fanya yafuatayo wakati unaongea na mtu:

  • Waangalie watu machoni wakati unaongea. Usipepese macho huku na kule. Macho yana siri kubwa kutambua anachosema mtu kama kina ukweli au la!
  • Wakati unaongea na mtu: fungua mikono yako usiikunje kwenye kifua au kuweka mikono mfukoni. Vingo vya mwili visaidie matamshi yako kufikisha ujumbe uliokusudiwa.

5. Uwe na mtazamo chanya

Upuka kujiona wewe ni bora kuliko wengine na kuwaona wengine hawafai. Kila mtu ni bora na anajivunia kuwa alivyo lakini majivuno yasivuke mipaka na kuwaathiri wengine wakajiona duni. Kuongeza uaminifu:

  • Upuka umimi ‘mimi’. Kwa ustaraabu wathamini wengine na wakati wote sisitiza ‘sisi’ kuonyesha wote mko pamoja na mnastahili hadhi sawa.
  • Kubali taarifa ya kweli na kukosolewa.
  • Tengeneza mahusiano mazuri na watu kwa mawasiliano ya wazi. Epuka mawasiliano ya siri.

 

6. Kwa Viongozi

Viongozi waaminifu wanahitajika sana katika jamii. Viongozi lazima wawe na uwezo:

  • Kusikiliza na kuziingatia mawazo ya wengine
  • Kujikita kwenye masuala muhimu na kutafuta majibu ya changamoto kuliko mambo binafsi ya watu
  • Kuuliza maswali ili kuongeza uelewa
  • Kutoa mifano iliyo hai inayoendana na mazingira husika
  • Kuwajibika kwa watu wako
  • Kuwa muwazi kwa mambo yanayohusu maendeleo.

 

 

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *