Abiria watano wafa kwa ajali ya magari Magu mkoani Mwanza

Jamii Africa

ABIRIA 5 wamefariki dunia  ambapo   wengine 11 kujeruhiwa baadhi yao vibaya  baada ya magari  waliyokuwa wakisafiria  kugongana katika wilaya ya Magu Mkoani hapa.

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Liberatus Barlow

Habari zilizolifikia FikiraPevu  na kuthibitishwa na  Kamanda wa apaolisi mkoani hapa zinadai kwamba  ajali hiyo ilitokea jana  ( Februali 29) katika  eneo la barabara kuu  la lami, Mwanza-Musoma.

Inadaiwa kwamba  ajali hiyo ambayo ilihusisha basi na gari dogo la abiria ilitokea jana majira ya saa 2:45 katika kijiji cha Bulula Kata ya Nyanguge, Tarafa ya Kahangara.

” Mimi  alikuwemo  ndugu yangu  katika moja ya magari yaliyogongana” kilidai chanzo cha  habari  kwa sharti la kutotajwa jina.

” Ni kweli kuna  ajali imeuwa; chanzo cha ajali hiyo  ni dereva wa gari dogo aina ya Noah kugeuka ghafla akiwa katika mwendo kasi na kugongana na basi hilo” alithibitisha Kamanda  wa  Polisi mkoani hapa, Liberatus Barlow .

Alisema gari hilo lenye namba za usajili T 716 BMV aina ya Noah Toyota,mali ya Mzamilu lilikuwa likitokea Magu mjini kuelekea jijini Mwanza ,ambapo  liligeuka ghafla kuelekea Magu.

Alifafanua kuwa  hali iliyosababisha  gari hilo kugongana  na basi hilo lenye namba za usajili T655 BDP mali ya kampuni ya Zakaria Wambura lililokuwa likiendeshwa na Bw. Aziz Hassan (4).

Alisema ajali hiyo ilisababisha vifo vya watu watano papo hapo waliokuwa wakisafiri na gari aina ya Noah akiwemo dereva wake.

Alisema  abiria 11 waliokuwa katika basi la Zakaria waliijeruhiwa katika ajali hiyo , 10 kati yao  walikimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Magu kwa matibabu.

Alieleza kuwa majeruhi mmoja kati ya hao 11 aliyetambuliwa kwa jina la Mbarouk Taka (52) mkazi wa Vingunguti Dar es salaam amevunjika  mkono wake wa kulia .

Kamanda Barlow  alisema majeruhi huyo alikimbiza  katika hospitali ya Rufaa Bugando (BMC)Jijini Mwanza kwa ajili ya kupatiwa matibabu na kwamba ali yake ilikuwa mbaya.

“Leo majira ya asubuhi imetokea ajali mbaya ambayo imesababisha vifo vya watu watano, baada ya gari aina Noah kugongana uso kwa uso na basi la abiria mali ya kampuni ya Zakaria ambalo lilikuwa likielekea Sirari wilayani Tarime likitokea Jijini Mwanza,” alisema na kuongeza kuwa,

“Baada ya kufika katika kijiji cha  Bulula, kulikuwa na gari dogo la abiria likitokea Magu, ambalo ghafla liligeuka kulekea  Magu na kusababisha yagongane na hiyo ni baada ya dereva  wa basi la Zakaria kujitahidi kulikwepa bila mafanikio”

Alisema marehemu wanne wametambuliwa ambao ni pamoja na dereva wa Noah,Deus John Kengele (42) mkazi wa Kiloleli Wilaya ya Ilelema jijini,mfanyabiashara,Peter Lubisha (45) .

Wengine  aliwataja kuwz ni  fundi umeme,Emmanule Kapesa (30) na mwinegine aliyetambuliwa kwa jina moja la Mwinyi mkazi wa Igoma wilaya ya Nyamagana jijini hapa.Marehemu mmoja bado hajatambuliwa.
Imeandaliwana na  Juma Ng’oko, Mwanza

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *