CCM YAIBUKA KIDEDEA IGUNGA

Jamii Africa

(Updated 6:29PM)

Chama cha Mapinduzi kimetangazwa kuwa ni mshindi wa kiti cha Ubunge cha Igunga baada ya kukibwaga Chama cha Demokrasia na Maendeleo ambacho kilileta upinzani mkubwa. kimeibuka mshindi wa kinyang’anyiro cha Ubunge jimbo la Igunga baada ya kupata kura zaidi ya 26,000 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambacho kimepata kura zinazokaribia 23,000. Ukijumlisha na kura zote ambazo zimepigwa CCM imeshinda kwa karibu asilimia 49 huku CDM kikiwa na asilimia 45. Hata jumla ya matokeo mengine yote yangeenda kwa CDM bado CDM isingeweza kushinda.

 

Ushindi huo wa CCM umehitimisha mojawapo ya michuano mikali ya kisiasa nchini ambapo vyama vya CDM, CUF na CCM vilionekana kufukuzana vikali. Mshindi wa kiti hicho cha Ubunge ni Dr. Peter Dalaly Kafumu ambaye kabla ya nafasi yake hiyo alikuwa ni Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini. Mshindani wake mkuu huko Igunga alikuwa ni Mwalimu Kashindye wa CDM.

 

Licha ya matatizo ya hapa na pale upigaji kura ulifanyika katika hali ya amani na utulivu mkubwa. Kiasi cha wapiga kura hata hivyo kilienda sambamba na kile cha waliopiga kura katika uchaguzi uliopita na hivyo kuonesha kuwa pamoja na kampeni motomoto za huko Igunga bado haikupatikana njia ya kuwashawishi watu wengi zaidi kujitokeza kupiga kura.

 

Ushindi wa CCM umekuja na kuwa pigo kubwa kwa CDM na hivyo kukifanya chama hicho kushindwa kushinda uchaguzi mdogo hata katika mazingira ambayo kilitarajiwa au kuonekana kukubalika zaidi. Chaguzi nyingine ambazo CDM ilidhaniwa kushinda ni ile ya Babati, Busanda na Biharamulo ambako kote CCM iliweza vyema kuvitetea viti vyake.

 

Uchaguzi huu umefanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa Igunga Bw. Rostam Aziz kujiuzulu nafasi zake ndani ya chama – ikiwemo Ubunge – na hivyo kusababisha kuitishwa uchaguzi mdogo miezi michache baada ya kushinda.

 

Hata hivyo kitakwimu, CDM imetoa ushindani mkali dhidi ya CCM kama ilivyotarajiwa. Katika uchaguzi uliopita CCM ilishindwa kwa zaidi ya asilimia 70 huku ikipata kura zaidi ya 35,674 huku CUF ikipata kura 11,321. CDM haikuwa na mgombea. Ni wazi kuwa kitakwimu tu CCM imepunguza kura zake lakini ni punguzo ambalo limetosha bado kukipatia ushindi na kazi kubwa ilikuwa kwa CDM kuweza kukabili idadi hiyo kubwa.

 

Matokeo hayo yamepokewa kwa mshangao mkubwa na baadhi ya viongozi wa CDM ambao wameonekana kushangazwa na mwelekeo huo hasa baada ya matokeo ya Igunga Mjini kuonekana kuwa hayakuw akama yalivyotarajiwa mahali ambapo ilionekana ni ngao yao. “Kwa kweli hatujui nini kimetokea, lakini kuna mengi ya kujifunza” amesema mmoja wa viongozi hao wa kitaifa aliyezungumza nasi bila kutajwa jina lake kwani matokeo yalikuwa hayajatolewa rasmi.

Jedwali la matokeo ya awali kwa kadiri tulivyoweza kuyapata yanaonesha matokeo kuwa hivi.*

KATA CCM CDM
Ntobo 730 302
Nguvumoja 694 284
Nkinga 1484 1079
Itumbo 1079 590
Nango 897 645
Igurubi 1064 801
Mwisi 926 992
Mbutu 1335 1427
Kinungu 855 756
Bukoko 1136 931
Nyandekwa 691 613
Ndembezi 866 806
Chabutwa 545 581
Ziba 1053 860
Igoweko 1051 808
Mwamashija 806 590
Sungwizi 1225 718
Isakamaliwa 525 593
Ngulu 622 412
Choma 1227 918
Kininginila 700 451
Mwashiku 798 484
Simbo 738 1016
Itunduru 738 784
Mwamashinda 1224 1421
 Igunga  3181  3358
JUMLA 26190 22220

Naye  Katibu Mwenezi wa Itikadi wa NEC ya CCM Bw. Nape Nnauye ametangaza kupitia mtandao wa JamiiForums.com kuwa chama chake kimeibuka mshindi. Akitupa vijembe vya kisiasa Bw. Nape amesema kuwa “MAGWANDWA NOMAAAAA kelele zote hizo aibu hii sasa inakuaje? kati ya kata 22 mmeambulia 3 CCM ikiibuka na 18 cuf moja tu, masikini”

* Matokeo hayo si rasmi bali kwa kadiri ya vyanzo vyetu mbalimbali yanawakilisha kwa kiasi kikubwa idadi kamili na hayatotofautiana sana na matokeo yatakayotangazwa rasmi. Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa wakati wowote na Msimamizi wa Uchaguzi huo Mdogo jimbo la Igunga.

 

Na. M. M. Mwanakijij

15 Comments
  • Dah! Ndugu Julius Mtatiro naomba arudie kauli yake kua CUF inamtaji wa kura zaidi 11,000. Hongereni CDM mmeonesha njia ya 2015!

  • Pongezi sana kwa CCM kwa ushindi. Pia angalizo kwa chama cha wajuaji CHADEMA, vitendo vyenu vya ujeuri na kuzarau dini ya wapiga kura wenu vinawagharim na bado Mungu atawapiga bakora zaidi mimi siipendi CCM, lakina kwa vitendo vya CHADEMA nitawachukia mpaka kufa

    • kaka ile sio dini ni ukweli wa kawaida. msiingize dini kwenye siasa. ina maana ukimkuta mwizi ana hijabu utamwacha???

    • kuna wkt tutaonekana wazembe sbb ya kushindwa kuelewa siasa Dini zikitumika vibaya kama ambavyo imethibitika hatutapata maendeleo tuyayotegemea ni kazi yetu kupima maneno ya wanasiasa ili tusipoteshwe katika imani zetu, pole Abdallah!

  • CCM watu bado wanaiamini,kama imejivua kamba na ingeweza kuitapika sumu waliyokunywa viongozi wake ya KUPENDA mali bado wangekuwa na nafsi kubwa ya kuliongoza Taifa la Tanzania.
    LAKINI wanapaswa kusoma maandiko UKUTANI. “MENE MENE,TEKELI TEKELI,NA PERESI”

    Wanayo nafasi,maana wanao wakati.

  • Ah!Hongeren sana CDM japokuwa hamkufanikiwa kuwa washindi.Joto mlilowapa CCM limewapa funzo! Msikate tamaa bado mna nafasi 2015 ila jitahidi kuondoa kasoro za vurugu zitawagharimu kwa maana Watz wanawaunga mkono!

  • Bw.NAPE acha kujidanganya ushindi huo usikupe asilimia CCM ilizopata na CDM mmeachana kidogo sana kwa hiyo hata usemeje CDM bado inaungwa mkono tofauti na mawazo yako.Subirin 2015 kama mtaendelea kuwa na hiyo jeuri yenu! Hujajifunza ya Zambia eh???

    • Ushindi ni ushindi hata wa tofauti wa kura moja!, CDM endeleeni kuishi kwa matumaini. Kujifanya mnajua sana huku mnataka kutugawa watanzania kidini!. Hongera Dr. P.D. Kafumu. KIDUMU CHAMA TAWALA!

      • hakuna anaeshabikia dini. chama sio dini. nategemea mtu anaeweza hata kufungua browser uwe umeelimika uwasaidie walio kijijin wasiojua hata maana ya V8(luxury car), walokaa giza since january, wanaoibiwa pesa yao ya kodi na watu wazwaz. lakini wewe una log in humu kuleta hoja za dini zisizokupeleka kokote.

  • Katika uchaguzi huu mshindi ni Chadema, kwa sababu miezi 11 iliyopita hawakupata hata kura 10,000 sasa wameongeza mara dufu kura zao na kwa mtindo huu 2014 (Serikali za mitaa) na 2015 (Uchaguzi Mkuu) ni miaka muhimu katika historia ya nchi hii kwani yatatokea yasiyotarajiwa!
    Nawashauri Chadema wajipange kuchukua serikali za mitaa na uchaguzi mkuu

  • Hongera sana CCM. tatizo la CDM ni kudharau na kubeza viongozi wa kitaifa. Hii inaondoa imani kwa wananchi kwani wanaeneza sera za chuki.
    Waache nguvu za hoja zishinde na sio hoja za nguvu.
    Waige mfano wa CUF sasa hasa Zanzibar walivyoweza kupata serikali ya mseto.

    By Joseph Massawe

    • Hongera CHADEMA.

      Ilikua vita nzito, sio dhidi ccm bali serikali but hawatuwezi tulichofanya ingunga ni kuuonyesha CCM, tofauti ya nguvu ya umma na nguvu ya rushwa,ghiriba na vitisho 2015. kura zita tosha. Polen mnaojiita CCM_”B”(cuf). Mmepoteza mvuto kwa wanwnchi. na MUSTAPHA ABBDALAH CCM ndio wanagawa watanzania kwa udini kwani umesahau juzi tu walikuahidi mahakama ya kadhi baada ya kuwapa kura wamekurusha.leo wamekudanganya mkristo ni muislam umewapa kura duuuuu!

      Peoples power

  • Rostam ndiye ana siasa uchwara wa kushinikizwa kujiuzulu, kisha kapandishwa jukwaani kwa lazima amnadi kafumu. Mkapa anasiri ya passport ya kipakistan ya rostam. Unisamehe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *