CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) kimeibuka kidedea katika uchaguzi mdogo wa Mbunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki ambapo mgombea wake Bw. Joshua Nassari amembwaga vibaya mgombea wa chama tawala Bw. Siyoi Sumari. FikraPevu inaweza kutangaza kwa uhakika baada ya kufuatilia kura zote za vituo kuwa CDM imeshinda kinyang’anyiro hicho kwa ushindi usio na utata.
Matokeo ya awali yasiyo rasmi yanaonesha kuwa mgombea wa CDM ameshinda kwa zaidi ya kura 6000.
Ushindi wa Bw. Nassari umekuja baada ya kinyang’anyiro kikali cha ushindani uliojaa kila aina ya vituko, vijembe, kejeli, na propaganda za kila aina kati ya vyama vikuu viwili vya kisiasa nchini yaani CCM na CHADEMA. Uchaguzi huu mdogo umefanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa Arumeru Mashariki Bw. Jeremiah Sumari aliyefariki takribani miezi mitatu iliyopita.
Kampeni ya uchaguzi mdogo huo huko Arusha ulihusisha vigogo mbalimbali wa vyama hivi vikubwa. Wakati CDM iliwapeleka viongozi wake wa juu CCM nayo ilipeleka viongozi wote wa juu isipokuwa Mwenyekiti wake ambaye ni Rais Bw. Kikwete pamoja na kumtumia Rais Mstaafu Bw. Benjamin Mkapa ambaye alifungua na kufunga kampeni yake.
Kwenye matokeo ya Udiwani kwenye kata zilizopiga kura hadi hivi sasa taarifa zinaonesha kuwa
Kirumba, Mwanza imeenda CDM
Lizaboni, Songea imeenda CDM
Msambweni, Tanga imeenda CUF
Bariadi, Shinyanga, imeenda CCM
Tutaendelea kuwaletea taarifa zaidi.
hata kiwira mbeya cdm tumeshinda
Ongera sana Chadema. Chadema is power! chama pekee kitakacholeta mabadiliko ya kimaendeleo .
sasa wameru wameamka. je kama baba alishindwa mtoto angeweza nini?
Ongera Chadema. wameru sasa wameamka.
Kweli mmeshinda sasa kilicho mbele yenu ni kufanya kazi nasio kubweteka na ushindi mlio upata.
MKAPA, LOWASA, WASIRA, ( VUVUZELA) LUSINDE, MWIGURU POROJO ZENU, UNAFIKI WENU umeshitukiwa na wanaarumeru, wamewachambua kuaanzia kwako Mkapa na wamegundua kichwani mmejaza funza na mataputapu, mmeisoma namba, Mkapa licha ya kuendelea kula pesa ya wavuja jasho wa tanzania bado unatafuta perdm ya kwenda kutoa matusi arumeru? imekura kwako, lowasa licha ya kuendelelea kuwaibia watanzania kwa kujiita mstaafu wakati huna ustaafu wowote umeisoma namba? hapo vipi! Mwiguru umehonga bei gani arumeru? watu wmekula ccm kura Chadema, na wewe vuvuzela vipi umetunga yapi? wasira aka king usingizi umeamka? au bado unaota?
chadema wakafanye kile wamekihaidi ili kujenga imani zaidi kwa wananchi ili kupata ushindi mkubwa 2015 mungu akipenda
hongera chadema wao wanapesa sisi tunamungu daima ila la msingi ni kutekeleza ahadi zote mlio wapa wanannchi ili kuongeza imani kwao ili 2015 tufanye ukweli zaidi..
ushindi mmepata tekelezeni ahadi co kwenda dodoma na waliopiga kura mmechaguliwa kutuwakilisha co kuongozana kwenda dom au kuna biashara za hoteli zenu huko chimba visima rudisha mashamba kama maji wamepeleka monduli yaelekezwe yanakostahili hayo na mengine ndio tunataka
hongera chadema, kueni kielelezo kwa wana arumeru mashariki,