CHADEMA yatoa tamko kuhusu vijana wanaopewa mafunzo ya ‘Janjaweed’ Mbeya

Thompson Mpanji

CHAMA cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimetoa tamko kuhusu mikakati ya Chama cha mapinduzi (CCM) kutoa mafunzo ya kijeshi ya 'Janjaweed' kwa vijana zaidi ya 200 katika makambi ya Shule ya Sekondari ya jumuiya ya wazazi ya Ivumwe, Igawilo na Itende kwa lengo la kuanzisha vurugu itakayoondoa amani na utulivu kwa wananchi wa Kata ya Iyela.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, katika Ofisi ya CHADEMA Kata ya Iyela, Mkuu wa operesheni ya M4C kanda ya Nyanda za juu Kusini, John Mwambigija maarufu Mzee wa Upako, amesema Chadema wamebaini njama za CCM kutoa mafunzo kwa vijana na wanao ushahidi wa kutosha na tayari wameshawasiliana na vyombo vya ulinzi na usalama vya Mkoa kwa hatua zaidi. 

Msikilize sehemu ya kwanza: Tamko la CHADEMA juu ya Mafunzo ya Janjaweed mkoani Mbeya (Part 1 – Audio)

Mwambigija ambaye pia ni Mwenyekiti wa hamasa kanda ya Nyanda za juu Kusini na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbeya mjini amesema, Chadema wangependa kuona amani inatawala na kuepusha yale yaliyotokea katika kampeni zinazoendelea jijini Arusha.
 
Msikilize sehemu ya pili: Tamko la CHADEMA juu ya Mafunzo ya Janjaweed mkoani Mbeya (Part 2 – Audio)
 
Mwambigija ameendelea kufafafanua kuhusu rafu zinazoendelea kuchezwa na Chama Cha mapinduzi katika kata ya Iyela.
 
Msikilize sehemu ya tatu: Tamko la CHADEMA juu ya Mafunzo ya Janjaweed mkoani Mbeya (Part 3 – Audio)

Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Mhe. Mwigulu Nchemba, amekanusha vikali taarifa hizi za CHADEMA na kuziita kuwa ni Siasa za majitaka za CHADEMA Mbeya na hofu ya kushindwa uchaguzi!

Akitoa ufafanuzi kupitia JamiiForums, Mwigulu amedai kuwa hajawahi toa maelekezo yoyote yanayohusu mafunzo ya kijeshi au kigaidi au ya aina yeyote kwa vijana wa CCM Mbeya au Tanzania kwa ujumla.

"Mafunzo yanayoendeshwa ndani ya CCM kwa vijana ni mafunzo ya tangu kuanzishwa kwa chama chetu, ambayo ni mafunzo yanayohusu siasa, itikadi, afya, elimu ya kujitegemea na mapokezi ya viongozi. Kabla ya mafunzo hayo vijana hufanya gwaride na mchakamchaka. Huu ni utaratibu unaofanyika miaka yote na sehemu zote za Tanzania bara na visiwani" alisisitiza Mwigulu.

2 Comments
  • CCM HUENNDESHA MAFUNZO KUWAANDAA VIJANA WAKE KUWA VIONGOZI WA KUKITUMIKIA CHAMA,HIO NI MIPANGO ENDELEVU YA CCM TOKA ENZI YA TANU NA AFRO SHIRAZ PARTY.NADHANI KILA MMOJA ANAELEWA TARATIBU ZA CHUO.CHADEMA NAO WAANZISHE MAFUNZO SIO KULALAMIKA

  • HABARI ZA SAA HIZI, CHDEMA NI CHAMA KINACHO ONYESHA MATUMAINI  JAPO KIDOGO, KWA SABABU HEBU HAO VIONGOZI WA JUU WACHAMA WAKUBALIANE KUACHIANA UONGOZI NDIO TUTA AMINI HATA WAKI WA WATAWALA WATAENDESHA VIZURI.

    LA PILI TUJARIBU KUWAAAMBIA WANA NCHI UKWELI SIO SIASA WA ANZE WAO KWA VITENDO NDIPO WANA NCHI WAJE NYUMA MFANO MANDELA ALIFUNGWA NA BADO ALIPO TOKA HARAKATI HAZIKUISHA TUKIFANYA HAYO TUPIGE MBIU YA MNYONGE UONE KAMA WANA NCHI WATAKAA KIMYA WA TAJIOTOKEZA NA WATAPINGA, TATU NI SIKU CHACHE SANA NDANI YA MWAKA HUU VIONGOZI WA KUBWA KIDUNIA KUJA KWETU 

    LAZIMA KWA MTU MWENYE AKILI UJIULIZE
    WANAFATA NN, SS NI WATU GANI, TUNA UKUBWA GANI, NATUNA NN, NA TUNA HITAJI NN, JE WANANCHI WANA FAIDIKA NN KISHA JIBU, ALIANZA RAIS WA CHINA SAWA NIRAFIKI ENZI YA MWALIMU, LAKINI ENZI YA MWALIMU TUNA ONA URAFIKI WAO NI WA MANUFAA KWA TAIFA WALI JENGA VIWANDA MFN. URAFIKI MPAKA LEO KIPO, RELI YA TAZARA MPAKA LEO IPO, KARATASI, KATANI LEO TUNA VITU VINGI NA TUNA MIKATABA MINGI NAO KIKWAPI KAMA VYA MWALIMU, SASA RAISI OBAMA ANAKUJA KUFANYA NN, KWA MANUFAA YA NANI, JIBU NI KWA MANUFAA YA KWAO LEO MAREKANI KUNA KUNDI LA VIJANA HAWANA AJIRA  JE WW WAPO KUNA MTU ANAEWEZA KUMTATULIA MWENZIE KABLA YA KWAKE ?

    BUSHI NAE ANA KUJA KUFANYA NN? HALAFU WAKE WA MARAISI NAO WANA KUJA KUFANYA NN? SASA JIULIZE NI MUDA MFUPI TANGIA MGOGORO WA GESI YA MTWARA UWEPO NA UGENI UNA KUJA? SASA ONA MFN. NCHI YA KATARY NITAJIRI KWA SABABU YA GESI LEO HII TANZANIA TUNA GESI TU NAWEZA KUWA KAMA KATARY NITAIFA AMBALO NI JANGWA LAKINI WANA MAFANIKIO MAKUBWA KULIKO SS TWENYE MALIASILI YA KILA AINA,JE NI VIONGOZI WETU WA MEKOSA UTASHI KUANZIA JUU MPAKA CHINI KWANI ENZI YA MWALIMU HA VIKUWEPO KWU NN HAKUFANYA HIVYO NI SWALI DOGO LA KUJI ULIZA, JE NI UROHO WA MADARAKA NA MAFANIKIO EBU TUWE WAZALENDO TUBADILIKE NA VIONGOZI KUWA NA HURUMA HUTA ISHI MILELE UNA ANGAMIZA KIZAZI KIKUBWA HII SIO AMANI YA MWALIMU NIUJINGA

    "WASWAHILI WANASEMA MRITHI ANA UCHUNGU " NDIO VIONGOZI WETU WALEO WOTE HAKUNA HATA MWENYE UNAFUU, SWALI KUNA MTU ANYE WAJUA WA TOTO WA BABA WA TAIFA WOTE JIBU HAPANA, LEO HII MWINY YUPO HAI MWANAE WAZIRI WA MWALIMU HA WAPO AMA KUNA KITU NDANIYAKE CHUNGUZA, LEO RIDHIWANI ANA JULIKANA KULIKO WAZIRI JE KIPINDI BABA YAKE WAZIRI ALIJULIKANA HIVYO JIBU? KWA SABABU GANU? ANGALIA UONGOZI NI HAYO TU KWA LEO NINA MENGI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *