Chuo Kikuu cha SAUT chamuasa Kikwete kuhusu “Misaada na ushoga”

Jamii Africa
Rais Kikwete

MAKAMU Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Augustino (SAUT), cha jijini Mwanza, Dk. Charles Kitima, ameionya Serikali ya Tanzania chini ya Rais Jakaya Kikwete, kutoridhia vitendo vya ushoga kufanyika hapa nchini, na kama itakubali mambo ya ushoga, Watanzania wataiondoa Serikali yao
madarakani.

Amesema, Tanzania haipo chini ya utawala wa kikoloni, na kwamba ni lazima Rais Kikwete ahakikishe ushoha hapa nchini unapigwa marufuku na
haupewi nafasi kama inavyotaka nchi ya Uingereza, na kwamba ni vema Watanzania wafe na umasikini wao kuliko kusujudia maovu kama hayo.
Dk. Kitima alitoa kauli hiyo jana, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa hafla ya kupokea msaada wa vitu mbali mbali kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya mafuta ya MOIL, Altaf Hiran Mansoor, maarufu kwa jina la ‘Dogo’, kwa watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Kiislamu tawi la SAUT.

Makamu Mkuu wa Chuo cha SAUT jijini Mwanza, Dk. Charles Kitima (kulia), akiteta jambo na mkurugenzi wa kampuni ya mafuta ya MOIL ya jijini Mwanza, Altaf Hiran Mansoor, wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa chakula uliotolewa na Mansoor kwa watoto yatima wanaolelewa na kituo cha Kiislamu kilichopo tawi la SAUT, ikiwa ni kusherehekea sikukuu ya IDD El-Hajj, jana. (Picha na Habari na Sitta Tumma).

Kauli hiyo ya Makamu Mkuu huyo wa Chuo cha SAUT, imekuja siku chache baada ya Waziri wa Uingereza, David Cameron kuzitaka nchi zinazopokea misaada mbali mbali kutoka nchini humo, kuridhia ushoga, vinginevyo vitanyimwa misaada hiyo. “Tanzania hatutaki mambo ya ushoga, tupo tayari kupigania hilo, tutapigana. Na kama Serikali itaridhia ushoga tutaiondoa madarakani, maana itakuwa haifai tena.”

“Watanzania tupo huru, hatupo chini ya utawala wa kikoloni. Kama Uingereza na Cameron wake wanapenda ushoga, wao huko huko!.
Wasituletee sisi huku. Ni bora tufe na umasikini wetu kuliko kukubali maudhi kama haya ya ushoga. Serikali ikikubali ushoga tutaiondoa
madarakani, ee ni bora iondoke kabisa”, alisema kwa jazba Makamu Mkuu huyo wa Chuo cha SAUT, Dk. Kitima.

Kwa mujibu wa Dk. Kitima, ushoga ni vitendo vya uovu na ukinuiwa na Serikali ni kuwaudhi wananchi wake, na kwamba kauli ya Waziri Cameron
wa Uingereza ni sawa na kauli ya kutaka kuua utu wa watu, hivyo ni bora Watanzania wafe kwa msimamo huo wa kupinga maagizo ya nchi za
agharibi juu ya ushoga.  Hata hivyo, Dk. Kitima alisema madhehebu yote ya dini hapa nchini hayakubaliani na vitendo hivyo vya ushoga, na kwamba hawakubaliani kueneza ugonjwa, badala yake waliowagonjwa wa ugonjwa huo wanatakiwa kutibiwa na si kueneza ugonjwa wa ushoga.

Kwa mujibu wa Makamu Mkuu huyo wa Chuo cha SAUT, Tanzania haipaswi kubabaishwa na Mataifa ya Magharibi na washirika wake, bali iwe na
msimamo wa kupingana na maovu yanayotaka kufanywa na mataifa hayo kwa kigezo cha umasikini wa Watanzania na nchi nyingine za Kiafrika.

“Wakristu na Waislamu hapa Tanzania hatukubali ushoga. Hatukubali kueneza ugonjwa, tunataka tutibu ugonjwa kwa mwenye ugonjwa!. Hivyo
Uingereza isilete chokochoko, na tunasema tutapigana katika hili kupinga ushoga”, alisisitiza Dk. Tizeba na kuongeza.  “Ushoga unaharibu utu wa mtu. Kukubali ushoga ni sawa na kuua vizazi vijavyo…maana Mungu aliumba mume na mke kwa mapenzi yake ikiwa ni pamoja na kuzaa watoto kwa njia aliyopendezwa nayo Mungu mwenyewe!”.

2 Comments
  • Co lazima uambiwe u ndo mwisho wa dunia, ukckia utakufa kwa upanga ndoiv, na colazma huone Upanga, bali wale watakao kubali ushoga ndio watakao pona na Upanga na wale watakao kataa watakufa kwa dhik

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *