Dereva wa Usalama afa kumuokoa Salma Kikwete

Jamii Africa

MSAFARA wa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete umepata ajali na kusababisha kifo cha dereva wa Idara ya Usalama wa Taifa, Ramadhani Mkoma, Fikra Pevu, limethibitishiwa.

Habari zilizoifikia Fikra Pevu na ambazo zilianza kumiminika katika mtandao wa Jamiiorums.com zimeeleza kwamba ajali hiyo imetokea eneo la Ruvu saa 6.30 Jumapili (Februari 13,210), wakati Mama Salma akielekea katika nyumba yao mpya kijijini Msoga.

Imeelezwa kwamba marehemu Mkoma aliyekua akiendesha gari la ulinzi alitoka pembeni kuhakikisha basi la Moro Best lililoonekana kutaka kuelekea upande wa gari la Mama Salma na kuligonga uso kwa uso.

Basi hilo T237 BHC likitokea Mpwawa, lilipoteza mwelekeo baada ya kuigonga basi dogo aina ya Toyota Hice lililokua limepaki pembeni kupisha msafara huo na kuanza kuserereaka kuingia barabarani.

“Dereva alijitoa mhanga kuhakikisha Mama Salma hapati ajali na ndio maana alitoka nyuma na kutangulia mbele ya gari lililombebe mama na kuligonga basi hilo,” anaeleza mtoa habari wetu.

Shuhuda mwingine aliyetoa taarifa yake katika mtandao wa Jamiiforums.com alisema:

“Nimepita hapo Ruvu, kweli gari ya Usalama wa Taifa aina ya Land Cruiser imeharibika vibaya sana upande wa dereva, inaonyesha dereva ameumia vibaya sana, basi la Moro Best pia limehusika katik ajali.”

Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, Absalom Mwakyoma, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Watu kadhaa wamejeruhiwa.

Picha: Michuzi

6 Comments
  • mikosi ya JK na familia yake! marehemu alitaka kujifanya shujaa, kiko wapi sasa, mama kikwete amepeta

  • Dereva kaonesha ushujaa kulinda viongozi wetu,angekuwepo kama huyu katika msafara wa Edward Moringe Sokoine asinekufa.May God rest him in peace,AMEN

  • Serikali Ifikirie jinsi ya kuwatunza familia ya shujaa aliyeokoa maisha ya mama salma Kikwete

  • kwa kweli ukizingatia watoto wanasoma na mke alikuwa mama wa nyumbani, tena afauatiliwe kwa ukaribu sana bila kupoteza mda wa kuzungushana.amejitoa kwa ajili ya mke wa rais hakuna anayeweza kujitoa mhanga ila yesu peke yake alijitoa lakini huyu hana tofauti na yesu.

  • Mimi naona Mke wa Mkwere angekufa tu, huenda Mkwere angeshtuka. Sio kwamba namchukia sana Mkwere au mkewe, ila tu ukweli ni kwamba tabia zake zimeshakera kupita kiasi. Nimesikia leo (11.05.2011) asubuhi kwene redio kwamba IMF imeishauri Serikali kuangalia upya misamaha ya kodi, VAT na tozo la madini ili kuiongezea serikali mapato kutokana na ukweli kwamba mapato yameshuka sana na inaonekana serikali imezidiwa sana. Tukishafikia kukopa kwa ajili ya kuendesha operation za kawaida kama mishahara tumeshaisha…!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *