Igunga: Mgombea wa CUF arejesha fomu

Jamii Africa

Mgombea Ubunge katika Jimbo la Igunga kwa tiketi ya Chama cha CUF Leopold Mahona amerejesha fomu ya kugombea nafasi hiyo katika ofisi za Mkurugenzi wa wilaya ya Igunga ambaye ndiye Msimamizi wa Uchaguzi mdogo Magayane Protus.

Mgombea Ubunge Jimbo la Igunga CUF Leopold Mahona akionyesha Bango atakalotumia wakati wa kampeni zake.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Kitaifa ya Zanziba na Katibu Mkuu wa CUF Seif Sharifu Hammad akiwasili ofisi za Mkuu wa wilaya ya Igunga jana kwa ajili ya kupokea taarifa za wilaya, kiongozi huyo yupo wilayani hapo kwa ziara fui ya kikazi

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Igunga Leopold Mahona arudisha fomu za kugombea ubunge kwa Mkurugenzi wa wilaya ya Igunga ambaye ndiye Msimamizi wa Uchaguzi mdogo Magayane Protus jana

Mkurugenzi na Msimamizi wa Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga Magayane Protus akimuelekeza namna ya kujaza baadhi ya nyaraka mgombea Ubunge Jimbo la Igunga kwa tiketi ya CUF Leopold Mahona wakati aliporejesha fomu zake jana. (Picha zote na Eliya Mbonea)

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *