IRAN: Watu 44 wafariki dunia, 82 wajeruhiwa baada ya treni mbili kugongana

Jamii Africa
Takribani watu 44 wamepoteza maisha na wengine 82 wamejeruhiwa baada ya treni mbili za abiria kugongana huko katika jiji la Shahroud lililopo kilometa 400 Mashariki mwa mji mkuu wa Tehran. Runinga ya Taifa imesema kuwa huenda idadi ya vifo ikaongezeka.
 
Picha zinaonyesha mabehewa manne yakiwa yameacha njia huku yamepinduka na mawili kati ya hayo manne yakiwaka moto.
 
iran_train_crash_25_11_2016
 
Gavana wa eneo lilitokea ajali, Mohammad Reza Khabbaz amesema kuwa bado haijujalikana idadi kamili ya abiria waliokuwa kwenye treni hizo lakini hadi jioni ya leo (Ijumaa, Novemba 25, 2016); kati ya abiria 82 waliojeruhiwa, ni 17 pekee waliobaki hospitali wakipatiwa matibabu.
 
Runinga moja imeripoti kuwa mpaka sasa ni helikopta moja imeshafika eneo la tukio kusaidia juhudi za uokoaji kwa sababu ya ugumu wa kufikika kwa eneo hilo sababu ya miundombinu mibovu.
Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *