Kesi namba 456 inayowakabili Wakurugenzi wa JamiiForums kuendelea kuunguruma Kisutu leo

Jamii Africa
KISUTU: Jamhuri imeanza kutoa ushahidi dhidi ya Wakurugenzi wa Jamii Media kulikwamisha Jeshi la Polisi kumkamata aliyetoa taarifa za "Michezo michafu ya Oilcom". Kesi hiyo itaendelea tena kesho. Fuatilia mtiririko mzima wa kesi hii ktk mtandao wa JamiiForums.com

KESI namba 456 inayowakabili wakurugenzi wa kampuni ya Jamii Media inayomilikia gazeti tando la FikraPevu na mtandao maarufu wa JamiiForums, Maxence Melo na Mike Mushi, inatarajiwa kuendelea tena leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kuanza kusikilizwa jana Mei 2, 2017.

Jana, shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka, SSP Ramadhan, kutoka Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam alipanda kizimbani kutoka ushahidi.

Fuatilia mtiririko mzima wa kesi hii ktk mtandao wa JamiiForums.com

Shahidi huyo na yuko kwenye ofisi hiyo kwa mwaka mmoja na nusu, ambapo kabla alikuwa Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke.

Shahidi huyo alieleza: "Mwaka jana mwishoni nilitoa amri lifunguliwe jalada dhidi yao, msingi wa amri hiyo ni kwa sababu washtakiwa walishindwa kutoa taarifa sahihi kwa maafisa wa upelelezi kuhusu shauri lililoripotiwa polisi."

“Tarehe 19/02/2016 alifika mwananchi aitwae Usama Mohammed katika ofisi yetu, huyu ni ofisa msimamizi wa mauzo ya rejereja katika kampuni ya Oilcom. Alifika na malalamiko kuwa tarehe 13/02/2016 alisoma habari moja JamiiForums kwamba kampuni yake ya Oilcom imetuhumiwa kukwepa kodi Bandarini na kuiibia Serikali na akasema taarifa hizo hazina ukweli wowote.

“Baada ya kumsikiliza kwa kina yaliandikwa maelezo na kufunguwa jalada DSMZ/CID/PE/64/2016. Jalada hilo lilikuwa la uchunguzi wa ukweli wa taarifa hiyo iliyoletwa na mteja wetu. ASP Fatuma Kigondo alielekezwa kuandika barua JamiiForums.

“Ili kupata taarifa za mtu aliyejiita "fuhra JF" au Expert Member, Mkurugenzi aliandikiwa barua ili kutoa taarifa za mtu huyo, barua iliandikwa tarehe 23/2/2016.

“Tulipokea barua kutoka JamiiForums, ilitoa maelezo marefu lakini haikuwa na majibu chanya tuliyoyaomba.

“Walihoji mamlaka ya polisi kutaka taarifa hizo na kusema wana haki ya usiri wa taarifa za wateja wao.”

 (Hakimu akaoneshwa barua ambayo inarejea: REJEA YA MADA TAJWA: USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar.

Shahidi alisema anaikumbuka barua ile aliiona kwa macho yake na akaiomba aitoe mahakamani kama kielelezo. Shahidi akaambiwa aisome barua.

Wakili akamuuliza shahidi ana maoni gani kuhusu barua kutoka JamiiForums, lakini shahidi akasema yeye hakuona taarifa yoyote ya faragha katika zile walizoomba.

Akaendelea kueleza kuwa tarehe 01/04/2016 waliandika barua nyingine kukumbushia taarifa hizo na walinukuu kifungu cha 10 vifungu vidogo vya 2-8 vya Sheria ya Makosa ya Mtandao (Crime Procedure Act).

“Kifungu hicho kinawapa mamlaka polisi kupata taarifa kutoka ofisi yoyote kama taarifa inahusiana na suala linalofanyiwa upelelezi. Baada ya barua hiyo JamiiForums hawakujibu tena, hivyo tukaona kuwa wanadhoofisha upelelezi wetu tukaamua tuwakamate wakurugenzi,” akaeleza shahidi huyo.

Alipoulizwa walichukua hatua gani, akasema wamefungua shauri ambalo liko mbele ya mahakama.
Baada ya hapo, aliingia wakili Tundu Lissu ambaye alisema ana maswali mengi sana.

Tundu Lissu: Anasema aeleze kisomo chake mpaka amekuwa SSP wa Polisi.

Shaidi anasema: Mei 2001 nilihitimu Chuo cha Polisi Moshi (CCP) kama Konstable wa Polisi, kati ya Februari 2002 na Julai 2003 nilipanda cheo na kuwa Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (Assistant inspector). Mnamo Desemba 2006, alipanda na kuwa Mkaguzi wa Polisi. Kati ya Februari – Julai 2009 nilipata mafunzo ya uofisa na kuwa Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP). Mwaka 2014 nikiwa katika ulinzi wa amani Sudan nilipanda kutoka ASP hadi kuwa SP. Mwaka 2016 ndiyo akawa SSP.

Tundu Lissu:Kkwa maelezo yako ni sawa nikisema wewe ni afisa wa polisi mwenye uzoefu wa upelezi wa makosa ya jinai? 

Jibu: Ndio.

Tundu Lissu: Ni sahihi kuwa una uzoefu wa upelelezi ndani na nje ya nchi? 

Jibu: Ndio.

Tundu Lissu: Kwa mujibu wa maelezo yako taarifa ya Usama Mohammed ndio ilipelekea mfungue jalada?

Jibu: Ndio 

Tundu Lissu: Na ndio zilipelekea muandike barua kwa JF 23 Februari 2016? 

Jibu: Kweli.

Tundu Lissu: Naomba umueleze hakimu kama hiyo barua iko mahakamani.

Jibu: Haipo.

Tundu Lissu: Sasa shahidi mimi ninayo hiyo barua(Anampa shahidi na kumwambia aiangalie).

Tundu Lissu: "Angalia hiyo barua SSP Kingai".

Tundu Lissu Anamwambia amwambie mheshimiwa hakimu kama ile barua imeandikwa kwa Maxence Melo.

Jibu: Haijataja jina la mtu.

Tundu Lissu: Kwahiyo jina la Max Melo Mubyazi halipo? 

Jibu: Halipo.

Tundu Lissu: Je! Imeelekezwa kwa Mike William?

Jibu: Haijataja jina.

Tundu Lissu: Sasa naomba useme kama kwenye hiyo barua mmesema kuwa mmepata taarifa toka kwa Usama Mohammed?

Jibu: hatujaandika na hatukuwa na sababu ya kufanya hivyo.

Tundu Lissu: Jamiiforums ni kampuni?

Jibu: Ni kampuni.

Tundu Lissu: Kama ni kampuni inatakiwa aiandikishwe brela, hati ya kuandikishwa Brela iko wapi? 

Jibu: Mheshimiwa mimi natoa ushahidi kama mtoa maelekezo, walioandika hizo barua watakuja na kueleza.

Tundu Lissu: Nauliza iko wapi? Yaani iko mahakamani sasa?

Jibu: Ndio.

Tundu Lissu: Kama kampuni inatakiwa iwe na Memorandum of Association, iko wapi?

Jibu: Sifahamu.

Tundu Lissu: Inatakiwa iwe na Bodi ya Wakurugenzi…ipo?

Jibu: Sifahamu.

Tundu Lissu: Nilikusikia ukisema mliwaandikia wakurugenzi ili wawape taarifa, ulimaanisha nini kama sasa unasema haujui kama ina bodi ya wakurugenzi?

Jibu: Mimi najua Wakurugenzi, bodi sijui.

Tundu Lissu: Una ushahidi wa aina yoyote kutoka brela kuhusu JF kama kampuni na washtakiwa kama wakurugenzi.

Jibu: kwa sasa sina ushahidi.

Tundu Lissu Kampa ile hati ya mashtaka, anasema aeleze kama kuna sehemu wanasema kama walipata taarifa kutoka kwa Usama Mohammed.

Jibu: Hakuna.

Tundu Lissu: Naomba useme kama kuna sehemu mmesema kuwa mlikuwa mnachunguza taarifa zinazohusu ukwepaji kodi au kuiibia serikali. 

Jibu: Hapana.

Tundu Lissu: Taarifa za ukwepaji kodi za Fahrer mliziprint??

Jibu: Sijui kama ziliprintiwa.

Tundu Lissu: Kwa hiyo ziko wapi?? Wewe si ndio kiongozi wa upelelezi.

Jibu: Hazipo mahakamani kwa sasa.

Tundu Lissu: Unataka hakimu azifate shimoni?

Jibu: Mimi ni shahidi mmoja kati ya wengi wengine watakuja nazo.

Shahidi amesoma barua toka kwa wanasheria wa JF. Kipande kimoja kinasema "mteja wetu yuko tayari kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa mujibu wa sheria".

Tundu Lissu anamuuliza sasa " ulisema kuwa katika barua hiyo JF ilijibu kuwa ina wajibu wa kulinda faragha za wateja wao. Kwa ufahamu wako kuna haki ya kila mtu kulindiwa faragha ya mawasiliano yake au hakuna?"

Jibu: Inategemea.

Tundu Lissu: Haki ipo au haipo?

Jibu: Kwa private person sifahamu…

Tundu Lissu: Kwa ufahamu wako kuna haki ya kulindiwa faragha ya mawasiliano kwa kila mtu including private persons? 

Jibu: Sifahamu.

Tundu Lissu: Barua ile ya kutoka kwa wanasheria wa JF inasema " mteja wetu anaomba ufafanuzi wa sheria itumikayo kuomba taarifa za mteja" kwa uelewa wako mtu anayeomba ufafanuzi amekataa kutoa taarifa au hajakataa?

Jibu: Kwa maelezo hayo amekataa.

Tundu Lissu: Mtu anayeandika kuwa " mteja wetu angependa kujua kipi cha sheria kinatumika kuomba taarifa za mteja ukiacha kifungu namba 32 cha Cyber Crime Act" Mtu aliyeuliza ni kifungu kipi cha sheria kinatumika amekataa kutoa taarifa au hajakataa?

Jibu: Kwa maelezo hayo ya sasa hajakataa.

Tundu Lissu: Umesema baada ya kupokea barua ya kutoka kwa wanasheria wa JF mliandika nyingine 1/4/2016…je iko mahakamani?

Jibu: Sina uhakika nadhani ipo mahakamani.

Hakimu: Mimi sina.

Tundu Lissu: Mimi ninayo.

Hakimu: Haiwezi kutumika wakati mimi sina haijafika mahakamani.

Tundu Lissu: Inaweza tumika Sababu ameitaja.

Tundu Lissu: Mweleze hakimu kama barua imewataja watuhumiwa.

Jibu: Haijawataja.

Tundu Lissu: Kwenye ushahidi wako wa msingi umesema kuwa barua hii haikujibiwa si ndio?

Jibu: Sijui kama haikujibiwa.

Tundu Lissu: Wewe ni msimamizi gani wa upelelezi usiyejua taarifa muhimu.

Jibu: Sikupata taarifa kama imejibiwa.

Tundu Lissu: Katoa barua toka kwa Victory attorneys iliyojibu barua ile ya 01/04/2016.

Tundu Lissu: Shahidi tafadhali ieleze mahakama kama barua hiyo haina mhuri wa kupokelewa na ofisi ya mkuu wa upelelezi kanda maalum ya Dar.

Jibu: Sina uhakika na Mhuri huu na wala Mhuri sina uhakika nao.

Tundu Lissu: Naomba uulinganishe mhuri huo na ule wa kwenye exhibit PI (barua ya majibu ya mwanzo) .

Jibu: Mimi sio expert wa hayo mambo siwezi kulinganisha.

Tundu Lissu: Tusomee hiyo document imeandikwa kupokewa lini

Jibu: Kwa mujibu wa document hiyo inaonesha ilipokewa 06/05/2016.

Wakili wa serikali alipinga suala hilo na kusema shahidi hawezi kuendelea kuhojiwa kwa document asiyokuwa na uhakika nayo.

Tundu Lissu: Naomba barua hii iwe admitted in evidence for purposes of impeaching….(itumike kama kielelezo).

Upande wa serikali: Shahidi aliyesimama mahakamani ameletwa na jamhuri, kumuimpeach shahidi ni kwa yule aliyemwita mahakamani….Lissu hawezi kumuimpeach shahidi aliyeletwa na jamhuri. Purpose of cross examination ni kucheck credibility ya shahidi…hawatakiwi kumuimpeach…wasubiri muda wa defence kutumia hizo documents…shahidi hawajamleta wao. Au wanipe kifungu wanachotumia kutaka kumuimpeach shahidi.

Tundu Lissu anatoa kifungu…Hakimu anapelekewa akisome 164 (1).

Baada ya kusoma hicho kifungu, Hakimu akaahirisha kesi hiyo hadi leo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *