Kijana amchinja baba yake na kumzika

Jamii Africa

BukobaWATU wawili wanasakwa na jeshi la polisi mkoani Kagera kwa tuhuma za kumkata vipande  viwili Richard Raphael (55) na kumzika, mmoja wa watuhumiwa akiwa ni mtoto wa marehemu.

Kamanda wa polisi mkoani hapa Henry Salewi  ameiambia Fikrapevu kuwa tukio hilo lilitoke May 23  asubuhi katika kata ya Kanyangereko Bukoba vijijini ambapo Kaiza Richard (22) alimuua baba yake akishirikiana na rafiki  yake ambaye hajatambuliwa jina.

Alisema siku ya tukio muda wa asubuhi Raphael alimwamsha binti yake (mtoto wa dada yake)aliyekuwa akiishi naye aitwaye Alinda Joachimu (10) kwenda shule na hivyo kumuacha mjomba wake akiwa na kijana wake huyo Kaiza.

Salewi alisema kuwa hata hivyo, baada ya binti huyo Joakim kufika shule alirejea nyumbani baada ya kufukuziwa mchango wa uji na hivyo kumkuta Kaiza na mtu mwingine wakiwa wanachimba shimo.

Baada ya mtoto huyo kuwauliza  sababu za kuchimba shimo walimjibu kuwa ni kwa ajili ya choo,huku wakimzuia binti  asiingie ndani ya nyumba lakini alifanikiwa kuingia na kumkuta mjomba wake  amekatwa vipande viwili na kulazwa kitandani.

Salewi ameieleza Fikrapevu kuwa mtoto  baada ya kuona hari hiyo alikimbia na kwenda kutoa taarifa kwa ndugu na majirani ambao walifika nyumbani kwa marehemu walimkuta Kaiza anafunga mlango akiwa amebeba begi mgongoni huku ameshikilia baiskeli ya baba yake.

Alisema baada ya kuona kundi la watu alifanikiwa kutoroka ambapo wananchi walingia ndani  na kukuta mwili wa marehemu haupo bali nyumba ikiwa imetapakaa damu na mtoto aliwapeleka sehemu alipomkuta binamu yake akichimba shimo na kukuta  tayari limefukiwa.

Alisema kuwa wananchi waliamua kufukua shimo hilo na kuukuta mwili wa marehemu ukiwa umekatwa  vipande na kufungwa kwenye mashuka na blanketi ndipo walitoa taarifa polisi watuhumiwa bado wanasakwa.

Habari hii ni kwa mujibu wa mwandishi wetu Phineas Bashaya aliyeko mkoani Kagera

2 Comments
  • bado kuna umuhimu wa kunyonga majangili wasiokuwa na utu kama hao na wengine wote ikibidi sheria ya mkononi ni njema kwa makatili kama hao inatisha,imenichukiza na kuniogopesha nachukizwa na vtendo vyote vya knyama!

    • fikiri kuwa mungu anakujaalia mtoto ambaye unaona ni zawadi kubwa kutoka kwa mola wako ,then anakuwa ni njia yako ya kuondokea duniani tena kinyama! real scary!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *