Lowassa aliteka Bunge; kusafisha njia ya Urais 2015?

Islam Mbaraka
Edward Lowassa

edward lowassaKUCHAGULIWA kwa Edward Lowassa, Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond/Dowans, kuwa Mwenyekiti wa Kamati nzito ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kumethibitisha nguvu kubwa aliyonayo mwanasiasa huyo kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Wachammbuzi mbalimbali katika mtandao maarufu wa JamiiForums na mitandao mingine ya kijamii kama FaceBook na Twitter, wameelezea uamuzi huo wa wabunge wa kumpa madaraka Lowassa na wabunge wengine ambao ni maswahiba zake, ni hatua muhimu kuelekea 2015.

Mmoja wa wachambuzi hao, ‘Fareed’ yeye ameanika wazi kwamba uamuzi huo wa wabunge umetoa nafasi kubwa kwa mafisadi ambao sasa watafanya watakavyo ndani ya Bunge.

Fareed yeye anatoa sababu zifuatazo;

1. Anajitengenezea CV ya kuwa mgombea Urais wa CCM 2015. Moja ya vigezo vikubwa vya CCM ni mgombea wa Urais kuwa na uzoefu wa mambo ya nje. Hapa Lowassa anajipatia CV hiyo kupitia kamati hii ya Bunge.

2. Akiwa mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje, ulinzi na usalama, atakuwa anapata security briefings (taarifa za usalama) na issue zote nyeti, kama Meremeta, rada, Kagoda, usalama wa taifa, Takukuru, polisi, jeshi, nk, vinapitia kwake. Anakuwa na powers ku-summon wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama hapa nchini.

3. Anapata meno ya kumshuhulikia adui wake mkuu kwenye mbio za urais, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, kwani kamati ya mambo ya nje ndiyo inayosimamia wizara ya Membe. Pia Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, naye anakuwa anasimamiwa na kamati hiyo ya Lowassa.

4. Mpambe wa Lowassa, Peter Serukamba, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu ili awashuhulikie kina John Magufuli na Dk. Harisson Mwakyembe wa wizara ya ujenzi.

5. Mpambe mwingine wa Lowassa na Rostam Aziz, January Makamba, amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya nishati na madini ili amfukuze kazi Ngeleja na kumuweka waziri wao mwingine na azime issue za Dowans/Richmond.

6. Zitto Kabwe, ambaye ni mtu wa kina Rostam kabaki kamati ya mashirika ya umma kama kanyaboya. Kamati za PAC na local government wamepewa TLP na UDP ambao ni vibaraka wa CCM kama CUF.

Lowassa, January na Serukamba na wapambe wao wa kamati za upinzani (Zitto, Augustino Mrema, John Cheyo) wanaingia kwenye kamati ya uongozi wa Bunge wakiwa wenyeviti wa kamati za Bunge. Watakuwa na majority vote kwenye kamati ya uongozi wa Bunge. Hii ina maana kuwa watakuwa wana uwezo wa kuamua moja kwa moja shuhuli za Bunge, kanuni, miswada, mwenendo na hoja mbali mbali za Bunge.

Spika Anne Makinda aliyehakikisha kina Lowassa, January, Serukamba na wengine wanapita kuwa kwenye kamati hizi anatajwa kuwa anapokea maelekezo ya Rostam Aziz anayetajwa kuwa ndiye aliyemuweka kuwa Spika. Amewateuwa wajumbe wachovu kwenye kwenye kamati hizi ili watu hawa wakamate uongozi wake.

Mchambuzi mwingine anayejiita ‘Kagemro’ alikua na haya ya kusema:

Kutokana na mambo ambayo leo yametokea mjini Dododma ni dhahiri kuwa kumekuwa na mapinduzi ya wazi ya kuliteka Bunge letu na kuanzia sasa litakuwa halina nguvu tena za kuwawajibisha mafisadi wala hakutakuwa na mtu wa kuzungumza lolote juu ya Mafisadi na ufisadi.

Nayasema haya kutokana na mambo yafuatayo;

1.       Uchaguzi wa wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge ni kama ifuatavyo;

(i)      Mwenyekiti wa kamati ya fedha na uchumi ni Abdallah Kigoda

(ii)    Mwenyekiti wa kamati ya katiba ,sheria na utawala ni Pindi Chana

(iii)   Mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje, ulinzi na usalama ni Edward Nyoyai Lowassa

(iv)  Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii ni Magreth Sitta

(v)    Mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya jamii ni Jenista Mhagama

(vi)  Mwenyekiti wa kamati ya ardhi, maliasili na mazingira ni ………….

(vii) Mwenyekiti wa kamati ya kilimo,mifugo na maji ni Prof.David Mwakyusa

(viii) Mwenyekiti wa kamati ya Miundombinu ni Peter Serukamba.

(ix)  Mwenyekiti kamati ya hesabu za za serikali za mitaa ni Augustino Mrema.

(x)  Mwenyekiti wa kamati ya hesabu za mashirika ya umma ni Zitto Kabwe

(xi) Mwenyekiti wa kamati ya heswabu za serikali ni John Momose Cheyo.

(xii) Mwenyekiti wa kamati ya viwanda na Biashara ni Mahamoud

(xiii)  Mwenyekiti wa kamati ya nishati na madini ni January Makamba.

Baada ya kuwaangalia wenyeviti hao ni kuwa kamati ya uongozi ya Bunge huwa ina wajumbe ambao ni wenyeviti wote kamati za kudumu pamoja na wafuatao;

(i)   Spika –Anne Makinda

(ii)  Naibu Spika- Job Ndugai

(iii)  Kiongozi waUpinzani- Freeman Mbowe.

(iv)  Mwanasheria Mkuu wa Serikali- Fredrick Werema

(v)  Waziri wa Nchi Bunge na uratibu- Willium Lukuvi.

Hivyo basi utaona kuwa kamati ya uongozi ya Bunge ambayo ina wajumbe 18 .

Kazi za kamati ya uongozi ya Bunge ni;

(i)  Kuendesha bunge siku hadi siku

(ii) Kuamua ni hoja gani zipelekwe Bungeni kujadiliwa

(iii) Kuamua nini kifanywe na Bunge na nini kisifanywe na Spika huwa ni msemaji wake wakishaamua.

Hivyo basi kati ya wajumbe 18 wa kamati ya uongozi ambayo kimsingi ndio Bunge lenyewe utaona kuwa Edward Lowassa amejigeuza na kuwa yeye ndiiye atakuwa anafanya maamuzi yote ndani ya Bunge na kuamua lipi lifanyike na lipi lisifanyike kwani wajumbe 13 wanamuunga mkono yeye ama ni watu wake. hao ni pamoja na ;

(i)      Lowassa

(ii)    Cheyo

(iii)   Serukamba

(iv)  January

(v)    Pindi Chana

(vi)  Jenister

(vii) Mrema

(viii) Zitto

(ix)  Makinda

(x)    Ndugai

(xi)  Lukuvi

(xii) Werema

(xiii)  Mahamoud (mbunge wa Kilwa Kasikazini)

Hivyo utaona jinsi Bunge lilivyotekwa.

Lowassa sasa ataweza kufanya yafuatayo;

(i)      Kumuita Membe na kumpa maelekezo ya kibunge

(ii)    Kumuita Sitta na kumpa maelekezo

(iii)   Kuita upya hoja ya Richmond kupitia January

(iv)  Kumuita Magufuli na Mwakyembe kupitia Serukamba

(v)    Kumuita IGP, DG-TIS kumpa briefing kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama.

Hivyo hii inaonyesha kuwa tutakuwa na Bunge la kumi la aina gani.

Yafaa kila mmoja akatafakari na kuchukua hatua nini kifuate baada ya hapo!

20 Comments
  • Sisi wananchi ambao tunapenda kuangalia sinema kama hizi bila kuzingatia madhara yake ndio wa kulaumiwa.
    Hatuwezi kuwa reasonable thinkers endapo Taifa linachezewa na kuvuliwa nguo mbele yetu bila kuchukua hatua.
    Sisi ndio tuliowachagua wabunge, sisi ndio tuliochagua rais na kadhalika. Ni sisi tunaoweza kuwawajibisha endapo vyombo tulivyoviunda kwa mujibu wa katiba vitasita kufanya hivyo.
    Tuendelee kuangalia senema na mwisho wa siku sterling atatoka kwenye screen na kutufanyia actions za kweli tukabaki tunashangaa.

  • Ombi langu kwa wabunge waachane na mambo ya kuendeleza kambi zao, huu sio wakati wake,waangalie taifa lilipofikia wajenge upya taifa bila kujali itikadi zao za vyama. Kwa sasa kuna shida nyingi zinazomgusa karibu kila mtanzania wa kawaida. umeme wa mgao, njaa hasa vijijini, nchi kudaiwa mabilioni na wtu binafsi ambao inasemekana ni watanzania wasio na uzalendo nk. hivyo kuondoa haya WABUNGE WASHIKAMANE.

  • hii inaonesha wazi kuwa ukombozi wa nchi hii sasa upo mikononi mwa waTanzania wenyewe si katika chama tawala.. naona hawa jamaa wanatuchezea mchezo wa madange.. kwa nini Watanzani atunaendelea kuwa hivi jamani?? hivi inawezekanaje kuwa mtu aliyejiuzulu nafasi ya uwaziri mkuu leo awe kiongozi tena jamani tuwe wawazi:: inawezekanaje hii lakini watanzania kwanini tunawaacha hawa wezi waendelee kutuibia nasi tupo macho… tunataka malaika wa Mungu ndo ashuke ashike hatamu?? no way ni lazima sisi watanzania tafadhali tuamue kama walivyofanya wa Misri kwa kweli lazima kikwete atoke madarakani!!! anajua sisi hatukukmchagua na hivyo yote anayofanya anafanya kwa ajili ya mafisadi wachache!! tumtoe Mshezi huyu jamani kabla nchi yetu haijageuka mahame!! hawezi kuongoza huyu hana sifa hana uwezo mwoga na mjinga hawezi kupambanua mambo hana sauti anaburuzwa tu NI KIBARAKA!!!!!

  • Yetu macho,tuone basi hiyo 2015,uwepo wa katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi itawezekana?.ladba kwa sabuni ya chuma itawezekana kujisafisha

    • TANZANIA KUSHNEI, SERIKALI INAONJESHWA CHATNEY NA KULISHWA PUTNEYH.

      MWAJAMENI TUGAWANE VYAKWETU KILA MTU AFE NA CHAKE..MAANA TUNAVISHWA MIWANI ZA CHUMA SASA.

  • JAMANI WADAU CHA MSINGI NI KUJIEPUSHA NA HII CCM KWANI HAITUFAIDISHI CHOCHOTE ZAIDI YA KUTUNYONYA LASILIMALI ZETU JAMANI HEBU FIKILIENI NI MIAKA MINGAPI CCM IMEONGOZA NCHI HII LAKN CHA AJABU NA CHA KUSHANGAZA CHADEMA IMECHUKUA JIJI LA MWANZA JUZI TU MACHINGA TUMERUHUSIWA KUFANYA BIASHARA BILA YA BUGDHA JE TUKIIPA NCHI NZIMA SI MABOMBA YATATOA MAZIWA JAMANI TUSIFANYE KOSA TENA WAPEDWA……CHECK OUT +255766201280

  • Fundisho tunalo tumeona yaliyotokea Algeria,Misri ,Libya Gagaffi kajificha hajulikani halipo,Sudan Omari Bashir kaanza kujisalimisha kwa umma.Tumeona sera mbovu za CCM shule za kata zimefelisha kwa 51%,WAMESHNDWA KUTENGENEZA AJIRA KWA WAHITIMU WA VYUO VIKUU NCHINI,Vyombo vya usalama vinafanya siasa badala ya kazi,Mafisadi wanakula bata wakitumia utajiri wetu.Nin kifanyike kuondoa hii kero ya udalali na utapeli kama Dowans,Deep Green Finance,KAGODA na Meremeta moja ni kuishinikiza serikali ijiuzulu nyingine ni kuwafungashia virago kwa kutowapa kura uchaguzi ujao 2015 pamoja na vyama vya upinzani ambao ni vibaraka waoHila za kuwazuia tena wanavyuo kutopiga kura haitowezekana

  • Akigombea Lowassa urais wajue ccm imekufa kifo cha mende na ci cha membe fisadi aliyejiuzuru kwa ufisadi aje kuongoza nchi? Tanzania kweli imekuwa nchi ya maigizo kwa viongozi wetu 2015 hatutachagua chama bali ni mtu mwenye mapenzi ya kweli kwa nchi yake si CCM wala CHADEMA bali ni yeyote mwenye mapenzi ya kweli kwa watanzania. lakni watanzania ni muda mwafaka kutambua kuwa tulie mchagua awmu zote hizi mbili ndie aliyechafua nchi yetu LOWASSA kaa chini tulikuonaa bado hatujasahau mambo uliyotufanyia watanzania wenzako mwisho (JK NCHI HII SI YA KULITHISHANA MAFISADI KWA MAFISADI,UFISADI WAKO UISHIE AWMU YAKO TUACHE WATANZANIA TUANZE KULIKAVA)

  • Watanzania tumekuwa tunafata mkumbo wa kifikara, wengi tumekuwa tukimuhukumu Lowasa bila kujua kuwa nini kafanya, Tumebakia na neno FISADI tu. Lowasa katumiwa na wana mtandao kama mbuzi wa kafara, Hivi hakuna hata jambo moja JEMA ambalo huyu Lowasa kafanya? hebu tuwe waungwana kidogo. Mimi siyo CCM wala sijawahi kuwa, ila sipendi kufata mtazamo kwa mkumbo.

  • Jojo naungana na wewe kabisa, tumekuwa tukimlaumu Lowasa kwa kiwango kikubwa wakati wahusika wakubwa wameachwa pembeni. Lowasa ameendelea kunyanyaswa, sasa kama hizo tuhuma zipo wabunge si waliongelee bungeni na apelekwe mahakamani kwa nini wanapiga tu kelele kuwa ni fisadi au kisa anaonekana akigombea atawasumbua wapinzani kwenye kinyang’anyiro?

  • Nashindwa kuelewa kwanini ufisadi wa lowasa umekuwa ni wa vyombo vya habari na hata cku moja sheria haichukui mkondo wake, Au no kusema yeye ni juu ya sheria? Lazima tuliangalie na pia tuwe tunaongea tukiwa na takwim la sivyo tutakuwa tunapotosha jamii. Binafsi namkubali lowasa kama mtendaji na naamini tungekuwa na mawaziri kama yeye tungekuwa mbali.
    NI MTAZAMO TU WANA JAMII

  • Tujiulize kwanini mwalim nyerere alimkataa huyu bwana .kushika nyadhifa nzito serikalini .sababu hizo zinatia mashaka miongoni mwa watanzania na zitatumika 2015 kupunguza kura zake pamoja na network nzuri kazi ya ziada inahitjika .Hakuna mtu mwingine ambaye hagharimu chama kumsafisha hadi akubalike? ATAFUTWE mtu hata kama yupo nje ya chama maadam anakubalika na watu wote sawa.apitishwe

    • Kazi kubwa tunayo kama watanzania, tuamke tufikiri nini la kufanya huko mbele ya safari yaani kabla ya hiyo 2015 vinginevyo tutakuwa hatuna pa kukimbilia!!

  • Huo ni mtazamo wa mwandishi kuwa Lowassa ameliteka bunge.Lakini ninamtazamo toafauti na siasa za nchi yetu na tukubaliane kuwa Tanzania si kiwanja kizuri cha kuchezea mchezo wa siasa.Leo hii CCM wanataka kutuaminisha kuwa Lowassa amekichafua chama mbele ya wapiga kura na ndio maana wana hasira mpaka kura za mh. JK zilipungua ukilinganisha na mwaka 2005.Nasema hivi si kweli ufisadi wa kimfumo ueitafuna serikali ya CCM hata kabla ya JK kutinga ikulu so tatizo si Lowassa.Na nafikiri huyu jamaa kwa uchapakazi wake anastahili tumpe nchi 2005 tusubiri tuone naamini atavuka vikwazo vyote

  • Ki2 ki1 nafahamu, kwamba; whether they like or not, they have already planted the seed of their own destruction. they made a great mistake to their survival. we, patriots, lets never give up fighting for our future excellency. hey guys, I need every tanzanian to understand this thing, that, changes are not necessary as fast as you may thought. Let us be patient to work on things which the fruit are anticipated with our grandchildren. it is bare truth that hawajui kwamba iko cku nchi hii itakuwa chini ya utawala wa wengine nje ya sisiem. The development of any nation in the world depends upon the exisxtence of creative leaders and uncorruptible one. under the ground of corruption the contry will remain poor. I’ve a single suggestion to Tanzanians that, Let us make trials and errors, I mean let us try to give chance to the oppositional party and I’m sure the devevlopment of our country won’t remin slagish as it is now. I hate the fraud ad corruptible leaders.

  • Salaam wanajamii,
    Yote nilyosoma hapo juu nilichogundua mambo mawili labda watu hawaijui siasa ya nchi yetu au kuna ushabiki wa kimaslahi,kwa kuweka sawa watanzania hatuna uzalendo iwapo uzalenndo utakuwepo hapa kwetu Tanzania kuanzia watu wa chini mpaka wa juu nawaakikishieni nchi hii itakuwa kijani kitupu nikiwa namaana itastawi,maneno haya nitafakari tosha,kwa kumalizia wasiomjua lowasa nawaambieni mtu huyu ni nguzo na akishika nchi hii pale bungeni na mitaani WAPINZANI watakosa la kusema maana kila idara itasafishika.AMINI nichosema

    • well said maliwe!!

      Lowassa ataigeuza hii nchi na kuwa ya kisomi na maendeleo

      mark my words!!

  • watz sisi wavivu,kutenda na kila kitu,naona sasa hata kufikiri tu wavivu.kila mtu anahaki ya kutoa mawazo na kusikilizwa, ila baadhi ya mawazo ukiyasoma unashangaa.unashindwa kujua kwamba jamaa ni mjinga au mpumbavu,cheo kinakuwa kigumu kumpa labda ukiwaunamsikiliza anawezajua ndicho kitokacho ubongoni au amepindisha tu maneno na yameanzia tu mdomoni ili apate ulaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *