Mabadiliko makubwa yaja CCM, January kupata mrithi

Jamii Africa

Chama cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kufanya mabadiliko makubwa katika uongozi wake wa juu, ikiwa ni pamoja na kubadilisha baadhi ya viongozi wake wa juu ikiwamo wajumbe wa Kamati Kuu (CC) yake, Fikra Pevu imejulishwa.

Taarifa za ndani ya CCM zinaeleza kwamba, Mwenyekiti wa CCM, Taifa Rais Jakaya Kikwete, anatarajiwa kuwasilisha mapendekezo yake katika kikao cha Kamati Kuu ambacho kimeanza mchana huu mjini Dodoma.

“Mwenyekiti atatoa taarifa kwa wajumbe wa CC mchana huu, kabla ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kitakachoanza Jumatatu. Tutarajie mabadiliko makubwa ndani ya CCM maana ameona akichelewa madhara yatakuwa makubwa zaidi,” anasema kiongozi wa CCM aliyeko Dodoma.

kikwete mwenyekiti ccm

Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya M. Kikwete

Miongoni mwa nafasi ambazo zinatarajiwa kufanyiwa mabadiliko ni nafasi ya January Makamba, ambaye ni Katibu wa NEC Siasa na Mambo ya Nje, ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

Katika mabadiliko ya hivi karibuni, viongozi wa serikali hawapaswi kuwa viongozi wa Kamati Kuu, jambo ambalo liliwagharimu aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, George Mkuchika na aliyekuwa Katibu wa NEC Siasa na Mambo ya Nje, Bernard Membe.

Nafasi nyingine inayotarajiwa kubadilishwa ni ile ya Itikadi na Uenezi inayoongozwa na Nape Nnauye, ambaye anatajwa kukabidhiwa madaraka makubwa zaidi na anatajwa mmoja wa viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kuchukua nafasi yake.

Katika mabadiliko hayo, inaelezwa kwamba kuna maandalizi ya kumrudisha katika siasa aliyekua Katibu Mkuu wa CCM, Philip Mangula, ambaye anatarajiwa kurudi katika nafasi nyingine badala ya ile ya Katibu Mkuu.

Imeelezwa kwamba, Kikwete anatarajiwa kuweka msimamo kuhusiana na hali ya kisiasa inayoendelea sasa ambako tayari Erward Lowassa, mtu aliyejigamba kuwa swahiba wake ambaye “hawakukutana barabarani” amejitokeza hadharani kukishambulia chama chake, huku akitajwa kuwa nyuma ya hujuma kubwa dhidi ya CCM.

Lowassa ambaye alitajwa kuwa mmoja wa watu wanaotakiwa kujivua gamba, amekua akipambana kujinasua na hivi karibuni watu kadhaa walio karibu naye, wamejiondoa CCM na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Pamoja na mabadiliko na mambo kadhaa kutajwa kujadiliwa Dodoma, Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Nape Nnauye, alisema kupitia blogu ya CCM kwamba chama hicho kinatarajia kujadili matatizo yanayowagusa wananchi na kuyatolea misimamo na ushauri wa hatua za kuchukua kuyatatua na kuyakabili.

Katika taarifa hiyo Nape amesema  CCM itajadili mambo mbalimbali ikiwemo ughali wa bei za vyakula na kero mbalimbali zinazogusa wananchi.

“Kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakilalamika hali ngumu ya maisha na kupanda kwa bei ya vyakula, hivyo NEC itapata taarifa ya serikali kuona hali ikoje na kuangalia nini kifanyike kupunguza au kuondokana kabisa na hali hiyo”, alisema Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi.

Nape alisema ajenda nyingine katika kikao cha NEC ni mchakato wa katiba mpya akisema ni lazima chama nacho kijadili ili kuona mapendekezo na mawazo ya Chama kuhusu mchakato huo.

Alisema pia CCM inatarajia kujaza nafasi zilizo wazi za makatibu wa mikoa na wilaya kwa kuwa kuna maeneo yamebaki wazi kutokana na watendaji wake kuteuliwa kuwa wakuu wa wilaya katika uteuzi uliofanywa hivi majuzi na Rais Kikwete.

30 Comments
  • CCM; huu sio wakati wakutolea misimamo wa matatizo ya wananchii. NI KUYATATUA. MTATOA MISIMAMO ILI NANI AJE ATATUE?? WEKENI BAYANA MIKAKATI INAYOTEKELEZEKA YA KUTATUA MATATIZO YA WANANCHI NA HAPO NDIPO WATU WANATAKA!!

  • HAWA CCM WAMEONA CHADEMA WANAKUJA JUU NA WAO MEKOSA MVUTO NDIO WANAANZA KUPARANGANA KUANZA KUTAFUTA KUJIPANGA. NAWAPA POLE SANA!

  • Wananchi wamekuwa wakilalamika kuhusu ukali wa maisha!! What a striking statement is this? Does it enter in your mind? It seems you are so ignorant of Tanzanian poor citzen and very unfortunately wewe ni kiongozi wetu. In short hujui unafanya nini. Statement yako ni kavu sana. Hujali!!!

    • Umesaau kuwa Mwenye shibe huwa hamkumbuki mwenye njaa? Hiyo ndo CCM na maela ya kifisadi, watawakumbuka watanzania mwaka 2015 baada ya hapo wanaendelea na utaratibu wao wa kugawana mkate wa Taifa

  • Ama kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa. Hadi leo CCM walikuwa hawaijui hali ngumu inayotukabili kutokana na ubadhirifu wao! Wanatarajia kukutana hivi karibuni eti wajadili namna ya kutuhurumia ili waipunguze!

    Inashangaza lakini hatupaswi kushangazwa sana, kwani wao wanaishi maisha tofauti kabisa na yetu; wanajilipa vizurh kabisa, watoto wao wanasoma kwenye ma-academy, wanazurura na dola baada ya kuihujumu shilingi yetu, na wanatumia mabenki ya nje kutunza ngawira walinazotuibia.

    Wametukabidhi kwa matambazi wenzao wa kimataifa ili watusulubu hadi tukome. Wameuza viwanda vilivyojengwa kwa jasho la mababu na mababa zetu kwa bei za kutupa kuhakikisha wanatuondolea ajira na kuwakabidhi wahuni waliovigeuza magodown au shule za kusomeshea watoto wao huku taifa likitoboka kuagiza bidhaa zilezile yilizokuwa zikitengenezwa na viwanda walivyogawana na kuwagawia maswahiba wao waliowaacha maelfu ya waliokuwa wafanyakazi ombaomba!

    Naam hii ndiyo CCM yenye kansa, iliyopoteza mwonekano wake na kupauka mithili ya mtu aliyekuwa akigaragara kwenye majivu. Kuna dawa moja tu ya watanzania kuondokana na balaa hili, nayo ni kuwafuta kwenye orodha ya uongozi wa nchi CCM na wote wanaojitanabaisha nao katika chaguzi zote zijazo.

    Mwaka 2015 ugeuke laana kwao wahaini wa utu na ustawi wa mtanzania. Mungu tubariki ili hili litokee.

    Mungu ibariki Tanzania.

  • ”Changes are inevitable in any soceity,those who resist it have to thrown away” Mabadiriko ndani ya CCM ni muhimu sana kwani ndio waliobeba ilani ya serikali iliyopo madarakani, ili kutimiza ilani yake. kuhusu matatizo ya wananchi chama kitoe msimamo wake pamoja na njia mbadala za kuondoa au kupunguza matatizo ya Watanzania!

    • Tunakubali kuwa mabadiliko ni muhimu; lakini siyo kwa CCM ya leo, kwani matatizo ndio leo wanayaona. Siku zote wamefumba macho leo wanafanya mabadiliko ya nini??

      Waendelee kufumba macho lakini wakijua kuwa SIKU YAO YA KIAMA IMEKARIBIA WAJIANDAE TU.

      UVUMILIVU HUWA UNA MWISHO, WANANCHI TUMECHOKA KUSHUHUDIA WENZETU WACHACHE WAKIJINUFAIFA KWA KISINGIZIO ETI NI VIONGOZI.

      MIZAMBWA
      INANIUMA SANA!!!

  • Haya ni maneno tu hata kwenye magazeti, vitabuni na sehemu zingine mbalimbali. Mfa maji haachi kutapatapa. CCM inajaribu kujirejesha lakini ni jambo gumu sana kufikia hilo kwani siyo rahisi imezungukwa na watu wabaya sana kuliko wakati mwingine wowote na hata maneno ya lowasa ni ngumu sana kujiamoni kurudia kuyasema na hasa kwa watu waliokuwa na akili timamu.

    Waovu ni wengi sana na kama misingi ni mizuri basi ililkuwa na si sasa. Kwa sasa misingi ni mibovu sana kwani wamebadili juu chini na wanatenda kinyume chake.

    NITOE POLE KWA KIKWETE MWENYEWE NW WENGINE WOTE MAANA HILO BOMU LA KUJITOA MHANGA LITAKAPOLIPUKA WATASAMBARATIKA WOTE. LKN HAPANA BUDI AWEPO MTU ATAKAYESAIDIA KUFA KWA CCM KAMA CYO KIKWETE NI NANI?

    NASEMA LAZIMA KIFEEEEEE….!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    • Hakuna mwingine atakayeshuhudia CCM ikifa zaidi ya Raisi Kikwete. Hili bomu litapasuka kichwani mwake. Na hii yote ni kutokana na kukumbatia marafiki na ufisadi wao.

      WANANCHI TUMECHOKA, TUNATAKA UHURU; YU WAPI MTU KAMA NYERERE AU INABIDI NYERERE AFUFUKE ILI ATUSAIDIE KAMA MWAKA 1961.

      MIZAMBWA
      INANIUMA SANA!!!

  • Hawajachelewa saaaaaaaaaana, lakini kuchelewa ni kuchelewa tu. Wana mda wa kutosha kujipanga zaidi pindi wakiwekwa pembeni ili wajichunguze vizuri!!!!!!!!!!!!!!!.

  • CCM kinaelekea kufa sasa wanatafuta mti wa kujishikilia. Muda mrefu wananchi tunalalamika kuhusu hali mbaya ya maisha, mfumuko wa bei; lakini viongozi wetu waliweka pamba masikioni kama wimbo tunaoimba wao hauwahusu kabisa.

    Sasa baada ya kuona moto unamaliza msitu ndio wanashituka na kutafuta mbinu za kuzima.

    CCM IMESHINDWA KUONGOZA NCHI HII, HIVYO NI WAKATI SASA KUTORUDI NYUMA TUIONDOE MADARAKANI WAENDE WAKAJIFUNZE KUONGOZA WANANCHI.

    MIZAMBWA
    INANIUMA SANA!!!

  • Mi nafikiri CCM sasa wapo ukingoni na wanajaribu kusema kila kinachowezekana kusemwa! Sasa chama tawala kinataka kutoa msimamo wake juu ya hali ngumu ya maisha? Haiingii akili kabisaa! sasa kinatoa msimamo wake kumwambia nani? wakati wao ndo watekelezaji wa sera zao ambazo ni pamoja na maisha bora kwa kila mtanzania! Kweli wamechanganyikiwa, na huu ni mwanzo tu! nataka watangaze uchaguzi kwenye majimbo yaliyo wazi ili wachanganyikiwe zaidi yanapochukuliwa na wapinzani

  • hv kupanda kwa gharama za maisha ni lazima kamati ikae kujadili! serikali haina wataalamu wa kutoa maamuzi ya kitaaalam kuhusu mfumo wa bei?hii nchi itaacha lini kufuata ushauri wa kiasili na kuanza kufanya kitaalam zaidi. CCM mmetufikisha hapa sababu ya kufanya kazi za taaluma kuwa ni za kisiasa.

  • ccm ni chama kikubwa kama vilivyokuwa vyama vingi vya siasa barani Afrika na duniani kote, ambavyo kwa kutojitambua wao walipoteza dola,kwa kutokusoma alama za nyakati..zipo nchi nyingi kama u.s.a..kenya nyingine nyingi nyingi haziko tena madarakani..Tatatizo hapa magamba wanalindana na wanafanya kazi za ufisad kama timu.hivyo kupelekea kwamba hata leo ukamweka malaika atachafuku tu.kwa kuwa mfumo ni mcafu..hakuna yeyote anaeweza kutoa maamuzi magumu.wote wanaangalia yao tu

  • ee mungu wote waliohusika katika ufisadi si wa madini,,mikataba mibovu,wizi wa kodi za wananchi,pembejeo kule sengerema bila kusahau dowa-asi ,Rich-munduli..I-patel (IPTL) ..UWALIPI KWA KADRI YA STAHILI ZAO,…Kilio chetu kikufikie ……..

    WAO WANA PESA!!!SISI TUNA MUNGU ASIE SHINDWA,people—poweeeeeeeeeeeeeeer!!!!P>>>Poweeeeeeeeeeeeeer

  • Hawana cha maana cha kuwaambia watanzania wanaotaabika na hali ngumu za maisha zaidi ya kuwaongezea ulaji wale wanaowaona ni wenzao, hili ni kosa la mwaka wanasahau wenzao wa dhati, ni yule mwananchi hoehae ambae anasubiri khanga,tisheti na kofia na kuwapigia kura wakitarajia maisha bora.

    Ni jukumu la mpiga kura kuwasaidia CCM kujua kwamba vipaumbele vyake ni uchwara kama havizingatii kumuondolea umaskini badala yake kujikita katika uswahiba.

  • Ni jukumu letu kuibadilisha jamii hii tuliyonayo, Hakika tumeumia, tumeumizwa na waliotuumiza hawana sababu za kuendelea kutudanganya. Tuamuke sasa tuachane na ujinga wa kurithishwa kifikra kuwa mtawala lazima atoke CCM, tujipange kuunda serikali bora na si bora serikali kwa wachache wanaoneemesha matumbo yao na familia zao mf (BMW)

    • Naungana na wewe lLINA kwa hayo uyasemayo!! Mwananchi kama mlengwa mkubwa haswaa mpiga kura ndiye mwenye kuleta mabadiliko akianzia kwa kumkataa kiongozi asiyewajibika kama impasavyo……na si kuchagua watu kwa kukariri!!

      Pia mwananchi anatakiwa aelewe fika kuwa, anapomchagua kiongozi basi kuondoka kwake madarakani ni mpaka amalize muda wake..HAPANA!!! Mwananchi anao uwezo wa kumwajibisha na kumuondoa madarakani kiongozi anayeshindwa kusimamia wajibu wake kama inavyotakiwa! ila kwa kuzembea kwetu, ndo hayo tunayashudia kwamba viongozi kwa maslahi yao binafsi tena bila aibu watumia kodi ya mwananchi kawalipa mpaka majina ya marehemu na watu waliokwishastaafu……NI JINSI GANI VIONGOZI WANAVYOTUCHEZEA AKILI ZETU!! Sasa kwa hili nalo mpaka tusubiri tume????

      Ebu tusiwafaidishe hawa watu wachache!!!

  • Hakuna nguzo nzuri yenye kuusimamisha uongozi kama KUMUHESHIMU MWANANCHI aliye kuamini na kukupa hiyo dhamana ya kuongoza.

    Ni dharau ya hali ya juu pale kiongozi huyo huyo ALIYEFADHILIWA NA MWANANCHI, anapoibuka na kusema eti “wananchi wamekuwa wakilalamika kuhusu ugumu wa maisha na kupanda kwa bei ya vyakula”……..hivi ina maana nyinyi hamuoni?? Na mnashikilia madaraka ya nini wakati hata wajibu wenu hamuujui na utendaji wenu unasubiria mpaka wananchi walalamike tena kwa muda mrefu???

    Ni miaka mingapi tangu JK aingie madarakani….hata mjidai kutaka kuleta mabadiliko leo?? Kila mara tumekuwa tukishuhudia mawaziri, watumishi wa umma na watendaji wale wale wakijirudia kwenye madaraka bila kutuletea mabadiliko yoyote zaidi ya kuwa tunawaona wanabadilishiwa tu sekta…………leo hii wapinzani wamewaumbua ndo mwajifanya kukumbuka kwamba kuna wananchi twafa kwa ugumu wa maisha???

    Anyways….mabadiliko ya chama chenu yafanyeni tu ila kwa huo mwendo wenu wa kukumbatia mafisadi mtaishia kuitishana vikao kila uchao na msiambulie la maana!!

  • CCM wamechoka na hawawezi kugundua mapungufu waliyonayo wakiwa madarakani hivyo 2015 tuwaweke pembeni ili wajifunze namna ya kumtumikia mwajiri wao, hapo wananchi tutaheshimika na kuthaminiwa.

  • CCM OYEEEEE!!!!! CCM OYEEEEEE!!!!
    KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI KIDUMU NAAM KIDUMU
    KWANZA NAMSHUKURU MUNGU MUUMBA MBIGU NA ARDHI
    ASANTENI SANA NDUGU ZANGU MABII NA MABWANA
    AWALI YA YOTE……
    Apanaaa nilikuwa naota tu, Hawa jamaa wana sema,tuna shida pia kuna matatizo , wana jadili na kujipanga kuziondoa baadhi ya kelllllo zenu mimi simo jamaani mimi sim…….
    kwanza nasema nchi hii ni ya amani na utulivu sasa shida hizi zimeanza lini tena lini Hawa CHADEMA sasa wanataka kuleta propaganda ndani ya chama chetu sisi sera zetu wananchi wametukubali sasa shida zipi eeeee shida gani weweeee wachaaa propaganda CCM OYEEEEEEE
    KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
    sisi wananchi tupo pamoja nanyinyi viongozi wetu shupavu
    wale wote wenye mawazo ya chadema ndani ya chama chetu wavuliwe gamba haraka bila kujali cheo chake sera zetu safi mwaka 2015 tuta shinda kwa kishindo eeeee kwa kishindo mmesikia eeeee hakuna mtu menye shida Nape usikubali hata kama utabaki pake yako sisi sisi tuta chagua
    CCM MUNGU IBARIKI TANZANIA

  • Namshukuru na kumpongeza sana Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa uamuzi wake wa kufanya mabadiliko makubwa katika chama, lakini je ni mabailiko yatakayoweza kubadilisha sura ya chama au kukiangamiza kabisa? Changamoto kubwa tuliyonayo ni kwamba wapinzani wanatumia sana udhaifu uliopo katka chama na kuutumia kujiimarisha wenyewe. Naomba haya mabadiliko yaweze kutusaidia kujipanga na kujiandaa vizuri kwa uchaguzi ujao wa 2015. Ninaamini “Tutashinda kwa kishindo”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *