Makaa ya mawe yanakwenda wapi?

Albano Midelo

Hapa ni katika bandari  ya Ndumbi ziwa Nyasa mkoani Ruvuma. Hii ni meli ambayo kila wiki inasafirisha tani 600 za makaa ya mawe ambayo yanachimba katika eneo la Ngaka Luanda wilayani Mbinga ambako kuna mamilioni ya tani za makaa ya mawe ambayo watalaamu wanadai yanaweza kuchimbwa kwa miaka 100. Makaa hayo husafirishwa hadi katika bandari ya Itungi wilayani  Kyela mkoani Mbeya na tani nyingine za makaa zinasafirishwa nje ya nchi .

Hata hivyo eneo hili  la Bandari halina  ofisi za watu wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA,ofisi za uhamiaji wala kituo cha polisi hali ambayo inatishia usalama wa Taifa pamoja na kuhujumiwa maliasili yetu.Hali hiyo ndiyo ambayo imemsukuma mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu kuangiza ofisi zote hizo zifunguliwe katika bandari hiyo.

Makaa ya mawe yakiwa katika bandari ya Ndumbi ziwa Nyasa mkoani Ruvuma yakisubiri kusafirishwa kwa njia ya meli  kupelekwa sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi.

1 Comment
  • hii ni hatari sana kwa taifaletu ukizingatia ndotuna jaribu kuendelea…kwa mtindo huu hatuwezi kufika

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *