Matapeli ‘wawaliza’ wanaotaka ajira TRA, baadhi wakamatwa

Jamii Africa

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA)kwa kushirikiana na vyombo vya dola, imewakamata matapeli wanaolaghai watu kuwa wanawapatia ajira katika mamlaka hiyo huku wakiwatoza fedha nyingi, Fikra Pevu imebaini.

Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya

Habari za ndani ya TRA na polisi, zimethibitisha kwamba mamia ya vijana katika maeneo mbalimbali nchini ikiwano Dar es Salaam, wamekuwa wakitapeliwa kuwa kuna ajira TRA lakini wanatakiwa kutoa fedha kabla ya kupatiwa ajira hizo.

“Kumeibuka wimbi la utapeli kuhusu ajira za TRA. Utapeli huo unafanywa na watu wanaojifanya kuwa watumishi wa TRA “matapeli” ambao hutumia barua zenye nembo ya Mamlaka na saini bandia ya Afisa Mkuu wa Rasilimali Watu,” inaeleza sehemu ya taarifa ya TRA iliyosambazwa  Jumatano Juni 20, 2012.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ambayo FikraPevu imeiona, matapeli hao wamefanikiwa kuwatapeli hadi wahitimu kadhaa wa vyuo vikuu nchini.

“Kinachofanyika ni kuwashawishi wananchi wanaotafuta kazi hususani waliohitimu vyuo kutoa fedha taslim ili wapatiwe ajira ndani ya TRA,” inaeleza.

Hadi sasa kuna wananchi kadhaa ambao wamefanyiwa utapeli huu.

“Hata hivyo TRA imefanikiwa kuwakamata baadhi ya matapeli hao na hivi sasa wanashikiliwa na vyombo vya dola,” inaeleza taarifa ya TRA na kuongeza;

“Tunaomba ushirikiano zaidi kutoka kwa jamii ili kufanikisha zoezi hili la kuwanasa watu hao kwani nia yao ni  kuchafua taswira nzuri ya TRA na kuwaibia wananchi.”

TRA imeeleza kwamba ajira za TRA zinafuata taratibu na kanuni za Ajira za Utumishi.

“Utaratibu ambao ni wa uwazi kabisa unaozingatia haki na uwezo wa mwombaji.  Baada ya hapo waombaji wenye sifa hushindanishwa  kwa njia ya mitihani na si vinginevyo,” inaeleza taarifa hiyo kutoka  Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA Makao Makuu.

4 Comments
  • Kwanza kabisa nashangaa sana kutokana na utaratibu uliofanywa na tra uliofanyika novemba mwaka jana pale msimbazi centre katika interview.tuliopata marks za juu wote ndio tuliokosa kazi zile post za preventive assistant,sasa kuna haja gani ya kuweka mitihani au mnatuzuga tu?

  • nawaomba TRA wapunguze upendeleo katika ajira zao maana sisi wenye vigezo vya elimu na uzoefu tunakosa ajira katika mamlaka kwa vigezo vya kujuana au fedha wakati tunamchango mkubwa sana kwa TRA jamani.

  • Jamani suala hili USALAMA mnalidharau lakini ni kiini cha uvunjaji wa amani humu nchini. Humu vyuoni kuna makundi yame anzishwa na vijana wa kiislamu na wanasaidiwa na wanafunzi hasa waliotokea Zanzibar, wana lishana na kuchochea imani za chuki uhasama dhidi ya dini nyinginezo, na tayari utaona wanaanza kutengana na baadhi ya waumini wa dini nyingine, Tatizo hapa si hofu ya vita bali ni hatma ya TZ na kizazi kijacho. Inakubalika kuwepo na vikundi vya kidini na vinginevyo lakini haviruhusiwi kuvunja sheria na taratibu zilizopo. Uislamu na Ukristo ni dini tu! Tena zililetwa na waarabu,wazungu pia tunaweza tukawaita wakoloni

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *