Matumizi ya ARV Mbeya yaongezeka

Gordon Kalulunga

MATUMIZI ya dawa za kurefusha maisha (ARV) kwa watu wanaoishi na VVU Mkoani Mbeya yameongezeka kwa kipindi cha miaka Nane.

Kaimu mratibu wa kitengo cha UKIMWI mkoa wa Mbeya Dkt.Francis Philly alisema kuwa mwitikio wa wagonjwa wanaotumia dawa za ARV kuwa ni mkubwa kwani takwimu zinaonesha kuwa kuanzia June 2004 hadi June 2012 wagonjwa waliojiandikisha katika huduma hiyo ni 106598 ambapo watu wazima ni 92085 na watoto ni 12889.

Alisema kuwa kati ya hao walioanzishiwa dozi ya ARV ni 52903 ambapo watu wazima ni 40701 na watoto ni 12202 na watu 13163 hawajulikani kama wamekatisha dozi ama wameacha.

''Katika hospitali ya mkoa wa mbeya watu 7675 wameandikishwa na 3539 wameanzishiwa tiba ya ARV na watu 1766 hawajulikani walipo na hali hii inaonesha wazi kuwa watu hawafuati maelekezo ya wataalamu wa afya''

‘’Kwa takwimu hiyo inaonyesha kuwa zaidi ya 50%ya watu wote ambao wameandikishwa katika huduma ya CTC wameanzishiwa dawa’’ alisema Mratibu huyo.

Kwa upande wake Afisa muuguzi wa kitengo cha CTC katika Hospitali ya mkoa wa Mbeya Mariam Mhanjo alitanabaisha kuwa katika sekta hiyo wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile ukosefu wa vitendea kazi, upungufu wa wahudumu katika sekta hiyo,miundombinu hususani vijijini  pamoja na masilahi kuwa duni.

Mhanjo ameiomba serikali kutatua changamoto hizo  ili waweze kufanya kazi katika mazingira mazuri na yanayorizisha.

2 Comments
  • jamani ninaiomba serikali iwe karibu sana na hawa wagonjwa na kujua tatizo ni nini la kuacha kutumia dawa

  • Nasikia mtu aachapo kutumia dawa hizi maisha yake yanakuwa mashakani sasa huko ikoje?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *