Mawaziri wanane watakiwa kung’oka, wamuandikia barua Kikwete

Jamii Africa

MOTO uliowashwa bungeni na wabunge kuibana serikali baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG), sasa umewalazimu mawaziri wanane kutakiwa kupima uzito wa makosa yao na kufanya maamuzi ikiwa ni pamoja na kutakiwa kung’oka.

Alhamisi usiku, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alitoa wito kwa wabunge wote kujiorodhesha kwa nia ya kupata saini za wabunge 71 ambao wangewasilisha kutimiza matakwa ya kisheria kupata asilimia 20 ya wabunge kwa ajili ya kumuondoa Waziri Mkuu.

Katibu wa Kamati ya Wabunge wa Chama cha Mapinduzi, Jenista Mhagama, akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kikao ambacho kimewashauri mawaziri wanane kujiuzulu.

Mawaziri ambao usiku huu tayari wamejipinda kumuandikia barua Rais Jakaya Kikwete, kwa ushauri wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuikoa serikali ya chama hicho isianguke kutokana na mpango wa wabunge kujirodhesha kutaka kumuondoa Waziri Mkuu,Mizengo Pinda.

Wanaotakiwa kuondoka ni Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),George Mkuchika, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushurika Jumanne Maghembe na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.
Hata hivyo, baadhi ya Mawaziri hao, wameelezea kuwa wataandika barua kwa Rais Kikwete kuelezea uozo wote uliosababisha kusakamwa kwao, baadhi wakidai kwamba hawahusiki kwa lolote na mambo wanayotuhumiwa nayo, huku baadhi wakiona mambo ni mazito na kuamua kujiondoa usiku huu.

19 Comments
  • Shame.Kwanini tumefika hapa tulipo?? What factors compeled this. Where is the authority?? Ni mpaka Kamati za Bunge zione uozo huo?? Kwanini CAG mapendekezo ya hayapewi uzito??? Its time CCM kuachia madaraka ili walioonyesha njia (UPINZANI) waweze kuongoza. Shame on them

    • Kwani kamati za Bunge kazi yake nini? Look kwa TZ kazi bado hakuna atayekuja kuwa clean. Tusijaribu. ukisema upinzani unakusudia muungano wa vyama au chama fulani? Hebu angalia uozo ndani ya upinzani (ubadhirifu wa kulipana maposho hadi wake zao, ukabila, ubadhirifu na baadhi ya wakuu kuhodhi madaraka). Kama tofauti ipo kati ya vyama pinzani na CCM ni kwa majina ya chama vyama tu. Watanzania tatizo kubwa ni “mind set”.

      Tunajuana na tunaona yanayofanyika makazini mfano TRA,makanisani kwetu nk tupadilike na tuache kusubiri kutafutiwa ajeda ndiyo tuanzishe malumbano katika blogs nk. hilo bunge lenyewe (CCM na wapinzani wote ni wachumia tumbo). Its a cultural question.

      Shame to TZ

  • Kikwete anatakiwa kuyaona haya, kwani madaktari walimshauri awatimue kazi waziri wa afya na naibu wake yeye akaona hamna mana, na imeshauriwa sana kuwa baraza lake ni uozo mtupu amepuuzia, huyo pinda mwenyewe anamapungufu kibao kwani kila lifanyikalo kwa mawaziri anaona na anachukulia poa, ngeleja tumepigia kelele muda mrefu lakini wamechuna tu. sasa hawa wasijiuzulu wasubiri Pinda akataliwe na mwishowe baraza zima livunjwe. Mimi ni mwana ccm ila kwa maelezo ya wabunge kwakweli nimechoka

  • mbona kwa mawaziri kumenoga hapo,HAKUNA MAREFU YASIYO NA NCHA,hata sem za kale nazo wanazipuuzia,haya sasa.!!!!!!!!!!!!!!!

    • Mambo yamekuwa magumu kujivua gamba kwa mawaziri waliotajwa ni muhimu sana ilikuonyesha uwajibikaji.

  • Kwani issue ni mawaziri tu? Mbona hatujaelezwa juu ya hao wabunge waliopata misamaha iliyosababisha serikali kupoteza zaidi ya trilioni 1? Ni vyema hao wanaotoa tuhuma kwa serikali nao wajiangalie, au ndio ule usemi wa “Nyani haoni …….”

  • Tatizo sio CCM wala political parts. Ni baadhi ya wanasiasa wasio na uchungu na taifa letu. Jingine ni kulindana/kuoneana aibu.
    Tunapowekana ktk nafasi inakuwa vigumu kuwajibika.
    Sasa watanzania tuamke tusikamane tutawarekebisha tu.
    NAUNGA MKONO WOTE WALIOPENDEKEZWA WANG’OKE

  • Baraza la mawazirI lote halifai wapo wachache sana wameturudisha nyuma sana kwa rasilimali tulizonazo hatustahili kuwa ombaomba nachukizwa sana na kaulimbiu TUMETHUBUTU,TUMEWEZA NA TUNASONGAMBELE AU TUNARUDI NYUMA

  • Nadhani watanzania hawajaambiwa ukweli wa matatizo, nawahakikishieni kuwa hata mawaziri wote wakaondolewa na wakawekwa wapya bado kashfa za ufujaji zitajendelea na wewe unayesoma comment hii hata wabadilishwe vipi hutaona ahueni katika maisha yako ya kila siku.

    Kwa sababu tatizo ni mfumo na ugomvi wa kibiashara na maslahi. Karibu 80% ya wabunge wote ni wafanya biashara wanamiliki au kuwa na hisa katika makampuni mbalimbali. hili halisemwi na watanzania hawajui kabisa. Wanapiga kelele mpaka mishipa inawatoka Bungeni kwa kujifanya wanatetea wananchi kumbe maslahi yao yameshikwa pabaya! Nadhani imefika mahala katika katiba mya kiwekwe kipengele wazi kuwa viongozi hasa wa kisiasa wasiwe wafanya biashara. Waamue kimoja.

    Angalia suala la korosho, pamba na kahawa. Tatizo ni wanasiasa wamejiingiza kwenye biashara hizo na wanataka kuwanyonya wananchi.

    Napata uchungu sana!

    • hapo kweli umenena ndugu
      vyama vya ushirika vimekufa, RTC zimekufa, reli ya kati is no longer kisa ni wawekezaji katika sekta husika, hao hao tunategemea watetee maslahi ya wote Vs yao binafsi, NI NGUMU sana.

  • hongera wanane wenye busara za kuikomboa nchi ,nawe muheshimiwa rais usiwe na shingo ngumu ya kuwakatalia mawaziri hawa matakwa ya barua zao kwani ni moja ya kulitatua suala la kikulacho kinguoni mwako.

    Maelezo ya barua zao ni muongozo wa kulitatua hili la kikulacho,maelezo ni njia bora ya kujua ukweli wa tatizo hususa ila tusibaki kugandisha mawazo kwenye hawa wanaomba kujiuzulu bali kwa watakao kuja wazibitiwaje kwa kutoshawika na tamaa ama kutumika kama njia za kuwaibia wapenzi wananchi wa tanzania. Kwanza nadhani mali zao zichunguzwe na kubainika ili watokapo madarakani takmini zipigwe kubashiri uhalali wa walicho chuma.

    Chengine, kujiuzulu kusiwe tiketi ya msamaha kwa wezi wetu kwani hata kama sio wezi sababu zao zaweza kutupa njia zenye nia.

  • KATIKA HILI MIMI BINAFSI SIJUI NIESEMJE,,ILA NINACHOTAKA MIMI NI MABADILIKO TU,,NANUKUU MANENO YA EINSTERN(THE GREAT GENIUS)..”THE PROBLEMS CAN NOT BE SOLVED BY THE SAME LEVEL OF THINKING THAT CREATED THEM”..HAPA INABIDI MFUMO WOTE UBADILKE, NA KUHUSU SUALA LA WATU BINAFSI,,NAONA MABADILIKO SANA KWA RAIA,,KWANI WENGI WAMESHAJUA HAKI ZAO,,NA HILI NDILO LA MUHIMU SANA KATIKA MAPINDUZI,,
    MUNGU UBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRICA..

  • THE ONE AND ONLY SOLUTION FOR THIS MATTER IS ‘REGIME CHANGE’, KILA SEHEMU IMEOZA. UTABADILISHA MARA NGAPI.TUPA PEMBENI CHUKUA CHATA INGINE NZIMA.

  • Ccm imepitwa na wakati.waheshimiwa mawaziri wanapaswa kuwajibika kwa tuhuma za ufisadi.chadema wajipange vizuri 2015 tuichukue nchi,wenzetu ccm waone wanaume tunavyopiga kazi. RIP ccm.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *