Huyu binti Lucy Mkondya (chini) anaishi katika kijiji cha Itaka wilayani Mbozi mkoani Mbeya,hapa ndiyo sehemu ambayo ni tegemeo kwa ajili ya maji ya kunywa kwa wakazi wa kijiji hicho, matone ya maji yanayotoka katika chemchemu iliyopo juu ya ndoo hizo yanachukua kati ya nusu saa hadi dakika 45 kujaza ndoo moja.
Tatizo la maji limetajwa kuwa limetokana na wakazi wa kijiji hicho kuharibu vyanzo vyote vya maji na hivi sasa kimebakia chanzo hicho pekee ambacho nacho kimeanza kuharibiwa
Hapa ni kitongoji kingine katika kijiji cha Itaka wilayani Mbozi mkoani Mbeya ambapo wanannchi wametengeneza mfereji na kuvuta maji kutoka katika chanzo cha mto hadi maeneo ya jirani ya kijiji ili kujipatia maji kwa matumizi mbalimbali kama unavyowaona katika picha.Hata hivyo njia hii ya kuvuta maji kutoka chanzo cha maji hadi nyumbani kunaelezwa na watalaamu kuwa kunachangia kusababisha kukausha vyanzo vya maji.