MLIMA Mtiro uliopo kijiji cha Busekela chache kutoka Musoma mjini ni mlima wenye hifadhi ya maajabu ya vyungu.Maajabu haya ni sehemu ya ibada zinazofanywa na watu wa ukoo Ambarwigi.
Ibada hizo za matambiko ambazo hufanywa na ukoo huo wa Ambarwigi pekee huusisha kazi ya kukabili ukame , ama ugomvi kati ya kijiji na kijiji na wakifanya hivyo mvua huwa inanyesha,kwani wapo watengeneza mvua (ambagimbi) na waliokuwa wakigombana hupatana.
Aidha wapo watu ambao si wa ukoo ule, wasioruhusiwi kwenda pale, husaidiwa na wenye mamlaka kwenda kutatua matatizo yao .
Kupanda mlima huu kunahitaji uangalizi wa wenye ruksa kwani ni mlima wa tambiko na mara zote utasindikizwa nao kutokana na sababu za kiusalama.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Busekela Emmanuel Eswaga ambaye aliniwezesha kukutana na Mzee Paulo Mgaywa (68) ambaye ni mmojawapo wa wazee wa ukoo wa Ambarwigi unaofanya tambiko katika mlima Mtiro.
Mzee Mgaywa ili kunipa uelewa mkubwa alikubali tuambatane pamoja kupanda mlima huo huku akituasa tuchukue maji ya kutosha na fimbo za kupandia milima.
Tukiongozwa na mwenyeji wetu mzee Mgaywa tulianza safari majira ya saa 3 asubuhi na kufika kileleni saa 6 mchana .
Mandhari ya kilele ya Mlima Mtiro unaokadiriwa kuwa na urefu wa mita 383 ni ya kuvutia kwani kwa upande wa kusini mwa mlima utaweza kuona ufukwe wa ziwa ulioko katika kitongoji cha Burungu,(Burungu Beach) na kijiji cha Bukumi.
Pia utaona visiwa vya Songe, Nyakarango, Ilela, Burwa, Chenyele Kwigari,Bwenyi kubwa, Bwenyi ndogo,Nyakarango,Bugurani na Mahome.
Utaona pia Wilaya ya Bunda milima ya Igunda na kijiji cha Sikilo na Mkoa wa Mwanza pia visiwa vya Ukerewe.
Ni hapa kileleni mzee huyu alinionesha sehemu maalumu ya kufanyia tambiko kwa ukoo huo.
Eeneo hili lina miti mikubwa mitatu ambapo mti mmoja umejizungusha kwenye mti mwingine. Juu ya mti katikati kunawekwa mtungi,chini ya mti katikati vinawekwa vyungu vidogo vidogo viwili.
Mzee Masole Kokorome Misana(90) ambaye kwa sasa ndiye Mkuu wa tambiko anasema matambiko ni sehemu muhimu sana kwenye maisha ya binadamu.
Mzee Masole Kokorome Misana (90) wa kijiji cha Burungu, Wilaya ya Butiama, ambaye ni Mkuu wa tambiko aliyeshikilia kofia akiwa na mwanae Magomba Masole (68) aliyemrithisha kufanya kazi ya tambiko wakiwa katika picha ya pamoja nyumbani kwao.
Anasema dharau ambazo vijana wa sasa wanazifanya kwa kujiona wasomi ni kitu kibaya kwani yapo madhara nda ni yake.
“Dunia ya sasa vijana wamekuwa wasomi wanasema haya mambo ni ya zamani na hivyo wamekuwa wakipata madhara makubwa wanapofika pale na kuvunja mtungi na vyungu kwa majaribio” anasema na kuongeza kuwa ameshudia vijana wengine wakiwa vilema mpaka sasa na mmoja kufa kutokana na dharau zao na kuvunja mtungi uliokuwa hapo kwenye eneo la tambiko.
Alisema: “Wakati Baba yangu akiwa hai, Kokorome Misana, kuna kijana alikuwa mwalimu Shule ya Msingi Busekela,mwalimu Sirila alikwenda kupeleka watoto kujifunza,kufika hapo kwenye mtungi akadharau akasema hizi ni imani potofu, akachukua mtungi huo na kuuvunja na akapata ulemavu wa mguu, lakini yeye aliomba radhi.
Aliongeza kuwa: “Yeye aliomba atoe fedha ila baba yangu alikataa kwani tambiko halifanywi kwa fedha bali kwa ng’ombe aina ya nyandege kichwa chake kikiwa cheusi katikati ya kichwa anakuwa na baka jeupe na mabaka meupe na meusi, uwepe ukiwa umezunguka tumboni pamoja na mtungi” alitoa na walikwenda mpaka sehemu ya tambiko wakamchinja na kumla wote kwa pamoja na hadi sasa yuko hai ila alipooza kiuno.
Eneo la tambiko ni sehemu tu ya vivutio vilivyopo Kwani ukiachia mbali eneo hilo kuna vivutio ambavyo vinatamkwa lakini havijulikani na wala hakuna mtaalamu yeyote ambaye amefika kuchunguza.Mfano, jiwe linalosemekana linazungumza ambalo lipo kijiji cha Chitare linalojulikana kwa jina la Nyamwasya.
Pia kuna michoro ya watu wa kale ambayo pia haijulikani ni ya miaka ipi.
Inasemekana pia kuwa maeneo ya Nyegina, katika Manispaa ya Musoma kuna unyayo wa mtu wa kale ambao pia hakuna mtaalamu yoyote ambaye amefika hapo kuthibitisha.
Mkuu wa wilaya ya Butiama Angeline Mabula anavunja ukimya, akisema watendaji wanapenda kufanya kazi kwa kusukumwa hawewezi kujituma.
Alisikika akizungumza kwa njia ya simu,"jamani mbona mnafanya kazi kwa kusukumwa, tumekwenda Dar kuhamasishana utalii wa ndani lakini wenzangu mlipofika tu mkatupa makablasha chini mpaka nipige tena simu jamani?" alilalamika Mabula.
Michoro ya watu wa kale ipo Nyabhirungu, Chitare. Tafadhali tuwasiliane kwa maelezo zaidi.
Inatia moyo kuona Makala inayokumbusha historia ya Majita na hasa mlima mtiro. Maajabu haya hayatangazwi kuwafikia watanzania wengi na hasa watalii. Nashauri tuwafikishie Precision Air habarihizi wazitangaze katikajadia lake kuvutia watalii na wao kupata wasafiri
Makongo
Kweli nakupongeza xn dada Mpendwa kwa kutukumbuka wanamajita kwa historia yakipekee ubarikiwe MAJITA KWETU
dada hongera kwa kuiandika hii makalla,una mpango gani kwa tz tourism industry?hasa hizi un-advartised destinations?wish you the best
Nimepata kujua nisiyo yajua, ahsante kwa kutuhabarisha