Mwalimu Salvius Nindi (40) wa shule ya msingi Mkenda iliopo mpakani wa Tanzania na Msumbiji akiwa katika moja ya nyumba zake za kitalii anazojenga kwaajili ya kuboresha kipato chake.
mwalimu huyo haonyeshi masikitiko wala kusita pale alipopangiwa kufundisha katika mazingira ya porini kama ambavyo walimu wengine hukumbia na kuacha kazi wakipangiwa katia maeneo yenye mazingira magumu. yeye anadai kuwa ukiyazoea mazingira magumu na kuyakubali yatakubadirisha maisha yako kama ambavyo yeye alitumia mapori kwa kilimo na sasa ni mfanyabishara mkubwa na anaipend akazi yake.
yeye anawashauri walimu wenzake kutokwepa mazingira magumu kwani kazi ni popote kinachotakiwa tu kuwa wabunifu kulingana na mazingira na kujishughulisha na kazi za ziada badala ya kutegemea kipato cha kazi pekee.
Hata hivyo mwalimu huyu anaishauri serikali kuwafikiria zaidi kwa posho walimu wanaofanya kazi katika mazingira magumu ili kuwatia moyo.
aisee watanzania tuige mfano wa huyo mwalimu ameweza kukabiliana na challege za maisha.ni mbunifu anajipatia kipato kizuri kupitia hizo nyumba nzuri kabisa
hakuna maisha magumu mbele ya kujituma kaza buti tazama unapokwenda
safi sana