Mwalimu na nyumba mbovu

Albano Midelo

Mazingira ya kufanyia kazi ya walimu walio wengi hasa kwenye maeneo ya vijijini yanakatisha tamaa,wakati wabunge wanadai posho zaidi,hali za walimu zinazidi kutia huruma .

John Komba Mmoja wa walimu katika shule ya msingi Liwundi iliyopo mwambao mwa ziwa Nyasa wilayani Mbinga mkoani Ruvuma akiwa amekata tamaa ya kufundisha  kutokana na kuishi kwenye mazingira magumu.

Hapa ni nyumba ya kuishi ambayo imeezekwa kwa nyasi.wakati walimu wanaishi kwenye mazingira haya ,wabunge wamepitishiwa posho kutoka  70,000 hadi 200,000 kwa siku,je huu ni uungwana kweli,katika mazingira haya tunatarajia elimu bora au bora elimu?

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ndingine mwambao mwa ziwa Nyasa Aidan Milinga akionyesha nyumba yake ya kuishi ambayo imeezekwa kwa nyasi, haina sakafu, ina madirisha na milango ambayo haina ubora, hivyo kumkatisha tamaa ya kufanyakazi kwenye mazingira hayo.

Shule hiyo yenye walimu watano ina nyumba mbili tu  zote za nyasi, pia inakabiliwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa kutokana na shule kuwa na wanafunzi zaidi ya 400.

4 Comments
  • Ni hivi huu ufisadi haujaangaliwa
    kotekote.Mradi wa MMEM umejenga mahekalu mengi sana ya maafisa elimu wilaya.pesa hizo zingejenga madarasa mazuri na nyumba nzuri za walimu.

  • Mradi wa MMEM umejenga mahekalu mengi sana ya maafisa elimu wilaya.pesa hizo zingejenga madarasa mazuri na nyumba nzuri za walimu.

  • hi ni hatari kwa kweli. Walimu hawathaminiwi. katka mazingira kama hayo mwalimu ahwezi kuwa na mori ya kufundisha. tutazidi kulalamika matokeo mabovu ya wanafunzi wetu. serikali ifikirie kwa kina swala hilo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *