MwanaHalisi lawasha moto Chuo Kikuu kuhusu DOWANS

Jamii Africa

WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo wamejawa na hamasa baada ya kusoma habari zilizochapishwa leo na gazeti la MwanaHalisi likimtaja moja kwa moja Mwanasiasa na mfabiashara maarufu, Rostam Aziz kwamba anahusika moja kwa moja na kampuni tata ya Dowans inayotajwa kutaka kuchota mamilioni ya fedha za walipa kodi.

Habari kutoka UDSM zinaeleza kwamba baada ya kusoma MwanaHalisi, wanafunzi walisikika wakisema wako tayari kwenda kumsaka na kushughulikia Rostam popote alipo kumzuia asipokee malipo kutoka serikalini kwa kisingizio cha kushinda kesi .

“Jamani twendeni tukamkamate Rostam na kumhukumu wenyewe. Sisi tunahangaika na mikopo hapa yeye anajichotea tu mapesa, ameanza na BoT na sasa anakuja Tanesco, alizopata zinatosha sasa na tuone atakayemlipa,” alisikika mmoja wa wanafunzi hao.

7 Comments
  • Huu ni muda mwafaka kwa watanzania kurudi nyuma na kuona kuwa azimio la arusha lina manufaa kwetu, chini ya utawala wa mwalimu Nyerere miiko ya uongozi ilikataza kiongozi kuwa na mishahara miwili,kuwa mwanasiasa na pia mfanyabiashara lakini sasa hivi wanfa biashara wengi wako bungeni nashangaa hizi awamu mbili za kikwete zimejaza wafanya biashsara.Nadhani kutakuwa na siri behind.watanzania tujiulize akina Mansoor,Rostam Aziz,salmu, na wengine wameingia bungeni kufanya nini? kuwasaidia watanzania kwa kuwaibia? Mansoor yuko tayari watu wa kwimba au ameingia kwa ajili ya manufaa ya biashara yake? tufike kipindi tuseme kuwa nasi tunaweza

  • Jama huyu Rostan ni nani kati ya watanzania zaidi ya million 35? Tusifanywe makondoo!!

  • Ukicheza na nyani, utavuna mabua. Hili la kucheka na mafisadi ni kuendelea kuwa Taifa ombaomba. Watanzania hebu tuamke na kukataa kuwaona mafisadi yakitunyonya.

    SOMA KITABU CHANGU CHA ”ANGUKO KUU TANZANIA” Utaona hasara ya kufuga mafisadi. Asante

  • Hivi sisi ni watanganyika au wadanganyika au watanzania maana sioni tofauti kati ya wadanganyika na watanganyika nadhani sasa umefika muda mwafaka kusimama imara na kusema hatumlipi huyu mjanja mapesa anayojifanya anatudai

  • tatizo serikali yetu ya jamhuri ya Tanzania ni ya kishikaji mno mpaka inafikia kipindi viongozi wanaona kama hakuna wa kuwafanya kitu,tuamke na tuwaondoe madarakani

  • Mnyika yupo sahihi kabisa kwaini tunaongozwa namalaika tunaongozwa na mwanadamu hivyo CCM wachikue hatua kujinasua katika uongozi ni wazee kifikra kimawazo nahata kimtazamo. Ni NGUVU YA UMMA TU kiboko yao

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *