Mwanga wa tochi na chemli watumika kuzalisha wajawazito Rufiji

Stella Mwaikusa

Mganga mkuu wa Zahanati ya Ndundunyikanza Dollo Victor, anasema kukosekana kwa umeme katika zahanati  hiyo kunamfanya afanye kazi katika mazingira magumu, hasa kwa wajawazito wanaofika hapo kwa ajili ya kujifungua.

Anasema yeye ni mhudumu pekee katika zahanati hiyo, inayopatikana katika kata ya Kipugira wilaya ya Rufiji,  kutokana na hali hiyo hujikuta katika hali ngumu katika kumzalisha mama mjamzito hasa pale taa yake ya chemli inapoisha mafuta.

Victor anaelezea hali ngumu anayokumbana nayo pale mjamzito anapomfikia,  na akiwa hana mafuta ya taa kwenye chemlii, ambapo hulazimika kutumia tochi yake ya nyumbani ili kuhakikisha anamsaidia  mjamzito.

DOLLO

“Niko peke yangu kwa hiyo nalazimika kumuomba mlinzi msaada wa kumlikiwa ili angalau nifanye kazi yangu vizuri, hali ambayo kimaadili si sahihi  ila nakosa namna ya kufanya” analalamika Victor.

Zahanati hiyo haina umeme tangu mwaka 2008 mpaka sasa, na kuwafanya wajawazito kujifungua kwa mwanga wa chemli au tochi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *