Senegal yataka Gaddafi aondoke; yatambua serikali ya Waasi

Jamii Africa

Serikali ya Senegal ambayo kwa muda mrefu ilikuwa na uhusiano wa karibu na serikali ya Muammar Gaddafi imeamua kuvunja uhusiano na kiongozi huyo na kutambua serikali ya waasi yenye makao makuu huko Benghazi. Akizungumza na waandishi wa habari jana Rais wa Senegal Bw. Abdoulaye Wade amesema kuwa ni itakuwa bora kwa Gaddafi kuachia ngazi “Mapema”.

Bw. Wade aliyasema hayo kutoka makao makuu ya wapinzani huko Benghazi ambako alizungumza na mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Taifa la Libya Bw. Mustafa Abdul-Jalil. Baraza hilo la mpito ndicho chombo ambacho kimetambuliwa na mataifa kadhaa sasa kuwa ndio serikali halali ya Libya kinyume na serikali ya Gaddafi.

Akitumia maneno makali Bw Wade alizungumza moja kwa moja kumuelekea Kanali Gaddafi na kumwambia kuwa “kwa maslahi yako na maslahi ya wananchi wa Libya uachie madaraka na usifikirie tena kurudi kwenye madaraka”. Rais Wade alidai kuwa katika nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika ni yeye pekee anayeweza kumuambia ukweli kani hamdai chochote. Katika wito wake huo Rais huyo wa Senegal ambaye aliongoza upinzani kwa muda mrefu nchini mwake na hatimaye kuingia madarakani alimuambia Kanali Gaddafi kuwa “uliingia madarakani miaka 40 kwa mapinduzi, hujawahi kuwa na uchaguzi, na unajifanya unazungumza kwa niaba ya watu wako lakini kila mtu anajua ulichotengeneza ni udikteta”.

Taifa la Senegal ni taifa ambalo linasifiwa kwa demokrasia iliyokomaa na ambalo licha ya kuwa lina Waislamu wengi mfumo wake unahakikisha taifa hilo linatawaliwa kwa kanuni za kisekula.

Bw. Wade ambaye amekuwa kiongozi wa kwanza wa kitaifa kutoka nje ya Libya kutembelea eneo la waasi amesema kuwa Baraza hilo la Mpito linahitaji kuweka utaratibu wa uchaguzi ili liweze kuingia na kukubalika kidemokrasia na hivyo kuweza hata kufungua mlango wa kujiunga na Umoja wa Afrika. Rais huyo wa Senegal ambaye amewahi kuwa karibu na Gaddafi  amesema kuwa yuko tayari kumsaidia mahali pa kwenda endapo Kanali Gaddafi ataamua kuondoka.

Pamoja na wito wake wa kutaka Kanali Gaddafi aondoke Rais Wade ametoa mwaliko kwa serikali ya mpito ya waasi huko Benghazi kufungua ofisi zao nchini Senegal ili kuweza kuendesha mambo yao na kuwa na wawakilishi.

Hadi hivi sasa ni nchi za Ufaransa, Italia, Qatar na Hispania ambazo zimeshatambua Baraza hilo la mpito kama wawakilishi halali wa wananchi wa Libya. Hadi hivi sasa serikali ya Tanzania ambayo imepata misaada mbalimbali kutoka kwa Gaddafi ikiwemo misaada ya magari yanayotumiwa na Rais bado haijaweza kuchukua uamuzi wa kutambua serikali ya mpito. Utata huu wa serikali ya Tanzania unadaiwa kuzikumba nchi nyingine za kiafrika ambazo zimekuwa zikipata misaada mbalimbali kutoka serikali ya Libya.

Mwandishi Wetu

4 Comments
  • Ghaddafi na Mugabe ndiyo viongozi wa Afrika pekee walio na sauti ya kupiga vita “ukoloni mamboleo”ifahamike wazungu hawataki wa Afrika wajikomboe kifikra ndiyo maana wa mechakachua mitaala ya elimu kwa nchi nyingi zinazoendele pitia sera za I.M.F na Bank ya dunia,ukiangalia watu wengi wasiowasomi na waliowasomi wengi wa Africa hawajui nini maana ya ukoloni mamboleo na jinsi gani unafanya kazi Africa pitia viongozi wasio wazalendo na wasio na Hofu ya Mungu.Sasa hapo kwanini mamluki wasitumike ku haribu harakati za viongozi wazalendo?Watu waelewe wakina Gaddafi na Mugabe shida yao si madaraka bali ni nchi ilisipelekwe tena mikonono mwa vibaraka wawazungu kama akina Kiwete,Mwaikibaki,Tshivangirai…….. wakati wao kwa meichukua nchi kwa mkono ktk mkono wa chuma iweje wairudishe tena kwa adui?Ghaddafi anahofia rasirimali,tamaduni,dini,jamii,siasa kuvurugwa na wazungu kwa matakwa yao.KNWANE NKURUMAH alisema”Nchi iliyo huru ni nchi inayo jiamulia mamboyake bila kuingiliwa huku pia ikijitegemea kiuchumi,kisiasa,kijamii bila kutegemea misaada yoyote toka popote”Sasa kwa hali kama hiyo Afrika nchi nyingi hazipo huru ila zina uhuru wa bendera,Ambao wanao weza upinga ni Mugabe na Ghadafi:Huyu raisi wa Senegal WADE yawezekana yeye ni mmoja ya mapuppet na yawezekana alisaidiwa na wazungu kuingia ikulu.ukweli utabaki wazi tu.Udikteta uangaliwe kwa pande mbili si ya ubaya tu hata uzuri ili kulinda tu maslahi ya wananchi na kudhibiti raia mamluki.

    • Pamoja na kuwa Gaddafi alimsaidia Idd Amin kuipiga Tanzania vita vya kagera 1978 kisiwe kigezo kwa watanzania kumchukia, hayo yamepita, cha msingi tuangalie gaddafi amewafanyia nn watu wake, kwa taarifa tulizonazo wananchi wa Libya wanaishi maisha ya raha kabla ya huu mtikisiko, miundo mbinu safi na huduma za afya safi, ss leo wahamtaki, hii ni nguvu kutoka magharibi, kuna kitu kinatafutwa pale chenye maslahi kwa wenzetu wa magharibi. sijui ss waafrika tutajikomboa lini. Huu ni uvamizi wa wazi kwa taifa la libya.

  • ya libya waachie walibya, siyo nato wala nani . kwangu mimi naona Gadaffi hana kosa hata moja nikilinganisha maisha or life expectancy yao sema kweli hamna nchi yoyote barani Africa ambayo watu wake walikuwa wakiishi kama walibya hapo mwanzo,.

  • Nilicho jifunza wandishi wa habari wa Tanzania! wanatumika na hao washenz kutoka magharib,,,,walioivamia LIBYA takatifu,,ambayo wananchi wana pata,Elimu BURE,,MAJI,,BURE,,MAKADHI,,UMEME,,AFYA,,,vyote ivi nibure na zaidi kila mwisho wa mwezi kunakitu kinaitwa grant..hii hata AFRIKA KUSINI..ambapo vijana wengi wa Tanzania wanakimbilia na kupasifia hakuna…grant na makazi ya kutolea mfano ni yale ya soweto tu.kwa libya i vitu yva kawida sana.

    HIKUMBUKWE GHADAF sio rais kama huyo mtwana WADE…GHADAF NI KIONGOZI WA LIBYA….SIO RAIS l>kama tatizo ni urais watapewa ghadaf atabaki kiongozi tunaona IRAN,UK, na sio lazima kufata mpango mpya wa ulimwengu NEW WORLD ORDER{ NWO}..HAO magaidi walioko BAGADHI alisha waelezea na kutoa talifa zao tangu 2006…FREE MANSON WOOOOOTE HAO NA MA BWANA ZAO MAREKANI NAWOTE MSIO JUA MNATUMIKA NAFRIMASON NAWAMBIENI…..
    GADAF NI MTU SAFII HAJAUA RAIA ana mpambana na magaidi wandani toka bagadh na wengine wana itwa NATO…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *