Serikali yadai vigezo vyote vya Kitaifa na Kimataifa vinaonyesha Hali ya Uchumi ni nzuri

Jamii Africa
Huku kukiwa na malalamiko ya ugumu wa maisha na kukosekana kwa fedha mifukoni, Serikali imesema kwa kutumia vigezo vyote vya Kitaifa na Kimataifa, hali ya mwenendo wa uchumi nchini ni nzuri. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha, Dkt. Philip Mpango akizungumza katika mkutano wa 18 wa taasisi za fedha nchini. Pamoja na hayo, Dk. Mpango alisema Serikali inaendelea kufuatilia mwenendo wa uchumi kila mara kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa kimataifa. Amesema kuwa tayari Taasisi ya Utafiti na Kupunguza Umasikini nchini (Repoa), imeshafanya utafiti wake na kuonyesha viashiria vinavyoonyesha mwenendo mzuri.

Serikali imesema kuwa japokuwa kuna malalamiko ya kukosekana kwa fedha mifukoni na ugumu wa maisha hali ya uchumi sio mbaya kama baadhi ya watu wanavyotaka kuiaminisha jamii.

Serikali imesema tayari imeshaitumia Taasisi ya Utafiti na Kupunguza Umaskini nchini(REPOA) na taasisi hiyo katika utafiti wake inaonyesha kuwa mwenendo wa uchumi nchini uko vizuri.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Fedha, Dkt. Philip Mpango akiwa jijini Arusha katika mkutano wa 18 wa taasisi za fedha nchini.

Dkt. Mpango amesema kuwa kwa vigezo vya Kimataifa kupitia Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ambao wametoa uchambuzi wa hali ya uchumi nchini takribani wiki tatu zilizopita, wametanabaisha kuwa hali ya uchumi ni nzuri.

img_8887

Pichani ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, akifafanua jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani-IMF, Kanda ya Afrika, Bi. Chileshe Mpundu Kapwepwe

Pia Dkt. Mpango amesema kuwa maneno yanayosemwa mtaani kuwa hali ya uchumi ni mbaya na fedha zimepungua katika mzunguko ni maneno ya wapiga dili.

Dkt. Mpango amesema kitu kinachoiogopesha Serikali kwa sasa ni ukame unaonyemelea nchi ambao unaweza kusababisha upungufu wa chakula katika baadhi ya mikoa. 

Katika hatua nyingine Gavana wa Benki Kuu(BoT), Prof. Benno Ndulu amezitaka Benki na taasisi za fedha kuhakikisha zinawafikia Watanzania wengi walio kwenye maeneo ya vijijini ili ziweze kukuza mitaji yao na kuchangia kukuza mzunguko wa fedha.

Mnakasha/mjadala kuhusiana kauli hii ya Serikali juu Hali ya Uchumi Unaendelea JamiiForums

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *