Uhaba wa waganga na manesi Nachingwea

Mariam Mkumbaru

"Nimeanza kazi ya kutibia wagonjwa mbalimbali katika zahanati ya Kiegei mwaka 2004, nikiwa peke yangu mpaka mwaka 2012 ndio nimeletewa msaidizi, huku nikiwa nimepanga chumba kimoja ambapo nimekaa kwa miaka sita ," alisema Olafu Chinguile

Chinguile alisema kuwa kipindi alichokuwa anafanya blia ya kuwa na nesi alikuwa anatibu wagonjwa wapata 6,000, wakazi wa kutoka katika kijiji cha Kiegei na vijiji vya wilaya ya Tunduru na Liwale.

"Miaka tisa nafanya kazi bila ya kuwa na msaidizi akifika mjamzito kliniki nampima, akija mgonjwa wa malaria nasimamisha kupima wajawazito naenda kumpima mgonjwa wa malaria, ni ngumu sana kutoa huduma peke yako kwa kijiji kama hiki kilichozungukwa na machimbo ya madini," alisema Chinguile

Mwaka 2012, aliletewa msaidizi ambaye ni nesi wa kuwapima wajawazito, watoto wa chini ya miaka mitano na kuwazalisha wajawazito, hapo ndio alipata nguvu zaidi ya kutoa huduma kwa jamii, kwa sababu nilikuwa na msaidizi.

kiegei four

Chinguile alisema kuwa bado kunahitajika wasaidizi maana kwa sasa kijiji kimeongezeka wakazi kutoka 6,000 mpaka kufikia 15,500 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, idadi ya watu ni kubwa ukilinganisha na wahudumu tunayotoa.

Changamoto kubwa iliyokuwepo katika zahanati ya kiegei ni ukosefu wa madawa mbalimbali ambayo wanaagiza bohari ya dawa, kutofika muda uliopangwa na kusababisha wagonjwa kuzidiwa na wengine kwenda katika tiba za miti shamba.

Sio tuu upatikanaji wa dawa hata kifaa cha kumsafisha mjamzito kama mimba imeharibika kijulikanacho (Kiureta) hakuna, na imesababisha wajawazito wawili kupoteza maisha kwa sababu kifaa hicho hakipo na ikabidi apelekwe katika kituo cha afya cha Kilimarondo, ni zaidi ya kilometa 25.

Alipofika katika kituo cha afya alifariki baada ya nusu saa kwa sababu ya barabara ni mbovu na usafiri tegemeo kwa kiegei ni pikipiki, pia mwaka jana zaidi ya mimba 10 ziliharibika kwa sababu mbalimbali ikiwemo ya magonjwa ya ngono, lakini wote tulishindwa kuwasafisha na kuwapeleka kituo cha afya.

Mwaka 2011 kulikuwa na wagonjwa wa Gono na Kaswende wapatao 48 na mwaka 2012 tulipokewa wagonjwa wa magonjwa hayo wapatao 38, hii inatokana na muingiliano wa wachimbaji wa madini kutoka katika mikoa mbalimbali ya nchini kuja kwenye machimbo ya dhahabu na rubi.

Zaidi ya wajawazito 123 walifika kupima ujauzito mwaka jana na 52 kati ya hao wamejifungua katika zahanati hiyo, ila katika jengo la kriniki hakuna umeme wa jua na wanazalisha wajawazito usiku kwa kutumia tochi ya simu.

Kwa upande wake Kaimu mganga mkuu wa wilya ya Nachingwea Dk. John Sijaona alisema kuwa, tatizo la wahudumu wa afya katika zahanati mbalimbali za wilaya hiyo ni kubwa sana ukilinganisha na mahitaji halisi.

Kwa sasa kuna watumishi 234, walitakiwa kuwa 500,  mahitaji ni 266, kuna daktri wa meno wawili, afisa tabibu 30, msaidizi wa madawa tisa pamoja na wahudumu wa afya wako 100.

Dk. Sijaona alisema kuwa zahanati nyingine zinaongozwa na wahudumu hao wa afya, kwa sababu ya uhaba wa waganga na manesi, hali hiyo inachangia vifo kwa wajawazito na kuchelewa kwa upatikanaji wa dawa kwa muda muaafaka kutokana na wahudumu kutojua kujaza fomu za biama ya afya kwa kingereza.

"Serikali wanazifahamu changamoto za upungufu wa wataalamu wa kutoa huduma za afya katika wilaya ya Nachingwea, ila tunaiomba serikali kutuongezea wataalau mbalimbali wa kada hii ya afya katika wilaya yetu," alisema Dk. Sijaona.

kiegei five

Pichani ni Zahanati ya Kiegei

Kwa sasa wamefanya maombi katika chuo cha uuguzi na utabibu kwa wanafunzi wanaomaliza mafunzo, kwenda katika wilaya hiyo ili kupunguza uhaba wa wataalamu na wamepata matabibu 34, Nachingwea kuna zahanati 32, vituo vya afya viwili na hospitali tatu.

Katika suala la upatikanaji wa dawa mbalimbali, Dk. Sijaona alisema kuwa tatizo la ucheleweshaji wa dawa linatokana na bohari ya dawa kutoleta dawa muda muafaka, muda ambazo dawa hizo zinakuwa zimeobwa katika zahanati, kituo cha afya na hospitali, pia  unaweza kuletewa dawa sio ulizoagiza kwa mfano phenobabitone.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *