Uchafuzi wa mto Ruvuma na athari za kimazingira

Albano Midelo

Uchafuzi katika mto RuvumaPicha inawaonesha wananchi wa kijiji cha Liganga wilayani Songea mkoani Ruvuma ambao hutumia maji ya mto Ruvuma kwa kunywa, kuoga, kufulia, kumwagilia katika bustani na kuvua samaki wanaopatikana kwenye mto huo ambao unamwaga maji yake katika Bahari ya Hindi. Watumiaji wa mto huo wapo katika hatari ya kupata maradhi na athari za kimazingira kutokana na mto huo kuchafuliwa  na kemikali zinazotumika katika migodi ya madini picha na maelezo na Albano Midelo.

2 Comments
  • Mr. Midelo
    Umechukua hatua gani kama mwandishi wa habari juu ya kuwaelimisha hao watu wa migodini juu ya athari za kemikali kwenye mto Ruvuma na mazingira kiujumla?

  • Nakushukuru Mr.Midelo kwa kuliona hilo maana linahatarisha maisha ya watu wa eneo hilo, hivyo naomba Serikali ichukue hatua haraka iwezekanavyo kuponya afya za wananchi wa kijiji cha Liganga Wilayani Songea Mkoani Ruvuma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *