Upigaji kura Igunga – Matatizo yaripotiwa – Update 1

Jamii Africa

Zoezi la upigaji kura limeanza huko Igunga huku maelfu ya watu wakijitokeza kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua mbunge wao. Zoezi hilo limeanza katika hali ya utulivu huku dosari ndogondogo zikionekana na kushughulikiwa mara moja. Mojawapo ya dosari ambazo zimeonekana ni ile ya wananchi kufika na kuanza kutafuta majina yao kwa muda kidogo. Baadhi ya wananchi hawakufika mapema kuangalia majina yao na kusubiri hadi asubuhi ya uchaguzi na hivyo kujikuta wanapata usumbufu hasa wakikosa majina kutoka kwenye vituo walivyodhania ndivyo vituo vyao.

Wapiga Kura kwenye sekondari ya Igunga

Matatizo mbalimbali madogo madogo yameendelea kuripotiwa kwa kadiri upigaji kura unavyoendelea. Baadhi ya matatizo hayo ambayo yameripotiwa na ITV/Radio One ni pamoja na baadhi ya watu kukosa majina yao vituoni, makabrasha ya upigaji kura kusafirishwa kwa baskeli kutokana na magari kukwama sababu ya mvua na vile vile baadhi ya watu kukataliwa kupiga kura kutokana na tofauti ya namba kwenye kadi za kupigia kura na zile rekodi zao kwenye vituo vya kupigia kura.

Sikiliza: Hali ya Upigaji Kura Igunga

FikraPevu itaendelea kukuletea taarifa kutoka Igunga.

Wananchi wa Igunga wakiangalia majina yao kwenye orodha ya wapiga kura kwenye shule ya Sekondari ya Igunga.

1 Comment
  • Shukrani sana kwa taarifa za upigaji kura Igunga kwa tusioweza kufuatilia kwa karibu.
    Tafadhali endeleeni kutufahamisha kadiri mtakavyoweza.
    Asanteni!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *