ZAHANATI ya Bunda mkoani Mara, inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya chumba cha kuchomea sindano wagonjwa kukosa madirisha.
Hali hiyo imebainika baada ya waandishi wa habari kutembelea zahanati hiyo na kuzungumza na uongozi wa zahanati chini ya muuguzi mkuu wa hospitali ya wilaya ya Bunda Adelaida Masage.
Msaidizi wa mganga wa zahanati ya Bunda Victoria Awino alikiri kuwepo kwa hali hiyo na kusema kuwa hiyo ni moja ya changamoto wanazozipata wataalam waliopo kwenye zahanati hiyo.
alisema kuwa katika zahanati hiyo kuna tatizo la miundombinu na kubwa zaidi ni pamoja na kukosekana na kwa dirisha katika chumba hicho muhimu cha kuchomea sindano wagonjwa.
‘’Tatizo kubwa la miundombinu ni pamoja na chumba cha kuchomea sindano wagonjwa kutokuwa na dirisha na sehemu ya mapokezi pia hatuna dirisha na nyumba za watumishi ni tatizo’’ alisema Victoria Awino.
Zahanati hiyo ya Bunda inahudumia wagonjwa kati ya 30 mpaka 40 kwa siku.
Serikali aone changamoyo hayo nakuyafanyia kazi sekta ya afya