Wagonjwa wanaolazwa Kinesi hatarini kumbukizwa malaria

Stella Mwaikusa

Wagonjwa wanaolazwa  katika kituo cha afya cha Kinesi  kilichopo kata ya Nyamunga wiayani Rotya, wako hatarini kuambukizwa malaria, kuytokama na kukosekana kwa vyandarua  katika wodi  mbili, zilizopo  katika kituo hicho.

Hayo yameelezwa na muuguzi mkunga  wa kituo hicho Nyakibore Bulenga, anasema vyandarua vilivyopo katika wodi ya akinamama na wanaume ni vidogo ikilinganishwa na  ukubwa wa vitanda vilivyopo kwenye wodi hizo.

muuguzi-NET

Muuguzi wa kituo cha Kinesi Nyakibore Bulenga, akionyesha chandarua

Anasema vyandarua hivyo huishia katikati ya kitanda  na kumfanya mgonjwa aliyelazwa kuumwa na mmbu na kuwa katika hatari ya kuambukizwa malaria.

“Kama unavyoona tuko karibu  na ziwa  kwa hiyo mmbu ni wengi, hii inatupa hofu kuhusu usalama wa wagonjwa wetu”.

Martha Mpandujii muuguzi katika kituo hicho anasema bado hawajatoa taarifa utawala kuhusu suala hilo, kutokana na matatizo mengi yanayokabili kituo hicho,  kama kukosa  umeme, maji na vifaa tiba.

Anasema kama kituo wameona kwanza washughulikie matatizo hayo na baadae suala la kukosekana kwa vyandarua vinavyokidhi litafuata.

Kituo hicho cha Kinesi kinahudumia vijiji vya Ruhu, Nyihara, Kinyamisana, Bitilio, Barack na Kibui.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *