Wanaotaka Urais 2015 wakerwa na UVCCM, wapania kuivuruga Dodoma

Islam Mbaraka
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UVCCM, Ridhiwani Kikwete

JOTO la kisiasa linazidi kupanda na sasa wanaotajwa kuwania Urais kupitia CCM 2015 wanatarajiwa kuanza kuonyesha misuli yao katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM) Jumamosi Machi 19, 2011 mjini Dodoma ambako imeelezwa kunatarajiwa kuibua mambo mazito.

Habari za ndani ya UVCCM na ambazo zimeripitiwa katika mtandao wa jamiiforums.com zimeeleza kwamba, kauli ya vijana  wa umoja huo mkoani Pwani hivi karibuni imewachefua wazee hususan wale wanaojipanga kuwania uraia 2015.

Kwa mujibu wa habari hizo zilizoripitiwa pia JamiiForums, upo uwezekano wa baadhi ya viongozi wa UVCCM kung’olewa akiwamo Kaimu Mwenyekiti wake, Benno Malisa.

Mbali ya Malisa pia Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM nayo inatarajiwa kuvunjwa. Miongoni mwa wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM yumo Ridhiwani Kikwete, mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, ambaye naye anaonekana kuwa mwiba.

Imeelezwa kwamba mwanasiasa aliyekerwa zaidi ni Edward Lowassa, Waziri Mkuu aliyejiuzulu baada ya kutajwa katika kashfa ya mradi wa umeme wa dharura uliokabidhiwa kwa kampuni tata ya Richmond ambayo katika mazingira tata ilihamisha umiliki kwa kampuni ya Dowans Tanzania Limited.

“ Hatua hiyo imekuja baada ya kutajwa na UVCCM na sasa anatafuta mchawi maana anasema baada ya kina Mwakyembe kumtaja katika kamati teule, hajawahi kutajwa tena ndani ya vikao rasmi vya CCM na popote na ndio maana akapita na kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama bila kupingwa. hata Bungeni hakuna mwenye ubavu wa kumtaja, na ndio ameshangaa na kushitishwa sana na UVCCM tena Pwani kumtaja hadharani tena kwa jina. Ameshangaa wamepata wapi hizo nguvu,” inaeleza sehemu ya taariga ndani ya Jamiiforums.

Wengine waliotajwa na UVCCM mkoa wa Pwani ni Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, ambaye alielezwa kukikosoa chama chake nje ya vikao wakati Lowassa alielezwa kukosa chama na serikali baada ya kutaka serikali iongeze mishahara kupunguza makali ya maisha. Walisema yeye alikuwapo serikali ya kwanza ya Kikwete.

5 Comments
  • hivi kama muda mwingi tunabaki kujadili uchaguzi wa 2015 je muda wa kuwatendea kazi wananchi unapatikaneje na kama chama chetu kimefikia hatua ya kutafuta mgombea miaka mitatu kabla hatuoni kwama tuna muanika adharani je hatuoi kwamba endapo atawakosea wananchi kabla ya uchaguzi tutakuwa tuna wapa mwanya wapinzani

  • what is happening now in ccm has reached a bad apex,,
    everybody looks on his interest,,so how to get that interest is ..to fight for the position,,coz posts are few this is making conflict of interest,,,
    we tanzanians we need to open our eyes then,,,to vote for those whom they ‘ll curb our protocols perspectively,,,

  • informal groups in any organization/association has two impact,
    1. to support change effectively and efficiently
    2. to go against the top management,,,,,this is what is eating CCM now

    My advise is that let those who real Tanzanians with authority not hestate to support the x-CCM members to form new political parties,,,this is for the essence of all Tanzanians ,,where dev is to come.

  • Kwa vyovyote vile ufisadi ni dhambi ambayo itaendelea kuwatafuna wahusika na watoto wao kwa vizazi ikiwa mtu anadiliki kufanya ufisadi nakushindwa kujitthimini niwazi anajiwekea vidonda ambavyo hataisha mpaka ametubu hata nabii sulemani alitafuna na dhambi ya kutembea na mke wa ulia baada ya kumtanguliza ulia vutani aka uawa ni hayo si sisiemu wa UVCCM watakao salia bila kubadili uelekewa na mfumo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *