Wasomali wamlipa Lowassa milioni 450, wampa hisa

Jamii Africa

WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu kwa kutajwa katika kashfa ya mdadi wa umeme uliohusisha kampuni tata ya Richmond Development LLC, Edward Lowassa, amelipwa mamilioni ya fedha na wafanyabiashara wa Kisomali, Fikra Pevu imethibitisha.

Uchunguzi wa muda mrefu wa Fikra Pevu umeonyesha kwamba Wasomali hao kupitia kampuni ya Integrated Properties Investment (T) Limited walimlipa Lowassa Sh milioni 450 kupitia kampuni yake ya Barare Limited. Malipo hayo yalielezwa kuwa ni deni ambalo Lowassa kupitia Barare alikua akiidai kampuni hiyo ya Integrated ambayo kwa Tanzania imekuwa ikijihusisha na uwekezaji katika majengo.

Uchunguzi wa Fikra Pevu umethibitisha kwamba malipo hayo yalifanyika miezi michache kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2010, na Lowassa na mkewe Regina Mumba Lowassa, walikubali malipo hayo kwa kupewa hisa 7,500 zikiwa na thamani ya Sh 60,000 kwa hisa moja.

Uchunguzi wa muda mrefu wa Fikra Pevu umeonyesha kwamba Wasomali hao kupitia kampuni ya Integrated Properties Investment (T) Limited walimlipa Lowassa Sh milioni 450 kupitia kampuni yake ya Barare Limited. Malipo hayo yalielezwa kuwa ni deni ambalo Lowassa kupitia Barare alikua akiidai kampuni hiyo ya Integrated ambayo kwa Tanzania imekuwa ikijihusisha na uwekezaji katika majengo.

Waraka wa Bodi ya Integrated iliyoidhinisha malipo kwa LowassaWaanzilishi wa Barare Limited

Sehemu ya nyaraka zinazohusiana na Barare Limited

Kampuni ya Barare Limited inamilikiwa na Lowassa na Regina kwa wanaoishi Mtaa wa Mahando namba 407, Masaki, Dar es Salaam, wakati Integrated ikiwa inamilikiwa na kundi la Wasomali, akiwamo Omar Abdi Ali, ambaye ni mfanyabishara na mchumi wa Kimataifa.

31 Comments
  • PCCB imchunguze Lowassa kwa tuhuma za ufisadi. Sheria inasema kuwa kiongozi yeyote wa umma akiwa na utajiri wa mashaka (unexplained wealth) anatakiwa kupelekwa mahakamani kujibu mashitaka ya ufisadi. Je, Lowassa amedeclare mali hizi kwa Tume ya Maadili ya Uongozi? Je, Lowassa amepata wapi mali za mabilioni ya shilingi alizojilimbikizia wakati yeye ni kiongozi wa umma na si mfanyabiashara?

    • MBUNGE WA BABATI-MJINI Bwa.KISYERI CHAMBIRI NI FISADI MKUUKUU
      Jinsi ambavyo Ksyeri Chambiri ameupata Ubunge wa Jimbo la Babati-Mjini ni kwa mtindo ule ule uliowachosha wapiga Kura wa Mkoa wa Mara na wakamkataa na Jimbo likawa limetwaliwa na upinzani. Mbunge huyo alifuja fedha alizolipwa na Serikali kwa ajili ya ukandarasi wa ujenzi wa Barabara ya kuunganisha Makao Makuu ya Mkoa wa Manyara-Babati Mjini na Makao Makuu ya Wilaya za Kiteto na Simanjiro. Fedha hizo alizitumia kununua ukoo wa ki-Iraqw na akapewa jina feki la Orondi na vivyohivyo akaununua ubunge wa Jimbo la Babati-Mjini kupitia wakandarasi wa rushwa akina mzee Sagdai, Mwenyekiti wa CCM -Wilaya ya Babati-Mjini Bwana Mtatuu Ihucha anayejiita ASKOFU pamoja na wasaliti wengineo wa demokrasia.
      Tunapenda kuitahadharisha TAKUKURU kwamba fedha za Halmashauri ya Mji-Babati zitaibwa kupita mizungu ya ndugu huyu. Tangia ameingia Bungeni hajawahi kuzungumza mahitaji ya wana-Babati Mjini kwa ulimi wake na wala hajawahi kuchangia kwa maandishi! Hajawahi kufanya ziara ya kushukuru tangu alipochaguliwa walau katika kata anayoishi kwa hoja kwamba anajua mbinu za kupata KURA za watu wa mjini Babati na sana sana atafanya ziara zake za kuwatembelea wananchi ifikapo nusu ya pili ya mwaka 2014. Kwa maneno yake mwenyewe, wakati huo ataanza kugawa fedha kwa kuwa anajua kiwango cha watu wa Babati kuwa hawataweza kumaliza Milioni 15. Huu ni ukweli kwa kuwa hivi sasa anajizatiti katika kuzikusanya kupitia njia anazozijua kwa kuwa kandarasi zimeota mgawa kwa upande wake kwa kupoteza uaminifu. Wakati akiwa katika shughuli zake nje ya Jimbo lake, vikao vya Halmashauri vinapoitishwa, yeye hupokelewa posho ambazo hakuhudhuria vikaoni kupitia kwa Mpenzi wake-Diwani wa Viti Maalum aitwaye Zainabu Dodo ambaye pia ni Mwenyekiti wa UWT-Wilaya ya Babati Mjini. Huu ni ufisadi mbaya kuwahi kufanywa na kiongozi mwenye wadhifa kama wa Chambiri. Tafadhali Bwana Hosea fuatilia orodha za malipo ya vikao vya Halmashauri ya Mji-Babati na utahakiki wizi huo wa wazi. Fanya utafiti kupitia madiwani wa Halmashuri hiyo ili uzikomboe fedha za Serikali.

  • Hii ndio Tanzania, viongoz wanajilimbikizia mali huku watoo wanakaa chini shuleni,.Lowasa amekuwa akituhumiwa kuwa na utajiri wa mashaka. mimi nashuri afilisiwe pamoja na viongozi wengine waliopata utajiri kwa njia za kifisadi.

    • Nakubaliana na wewe lakini kwa serikali ya ccm swala hili la kuwafilisi hailiwezi.
      Watu mbona wanasahau RICHMOND waliyopiga na mkuu wa kaya mpaka wakaanza kuumbuana kwenye vikao halafu wakaizima hoja ghafla.
      Alikuja pia na mvua ya kutengeneza akashtukiwa.
      Vile vile alikuwa akifuja pesa za miradi ya maji.

  • Kujihusisha na “Biashara” za namna hii ndiko kunakopelekea viongozi wetu kujiingiza katika ufisadi unaoliangamiza yaifa letu sasa. Kiongozi huyu ni mtuhumiwa wa miduara kadhaa ya rushwa na ufisadi. Ameliingiza taifa katika hasara kubwa na bado anaendelea kwani hakuna wa kum “tame.”

    Ingawa tatizo ni la uroho wa utajiri wa Lowassa, tatizo kubwa zaidi hapa ni kuondolewa kwa Azimio la Arusha na miiko ya uongozi ambapo sasa viongozi wamegeuka wezi na vibakauchumi wa mchana kweupee! Hebu ona sasa, kujiingiza kwake kwenye kampuni ya Vodacom kama shareholder wa moja ya kampuni tanzu zao kunalisababishia taifa hasara kwa wahuni wale kulindwa wasilipe kodi. ]

    Wakati huko Kenya na Uganda Kampuni za Safaricom na MTN zinaongoza kwa kuchangiapato la mataifa hayo hapa kwetu makampuni ya mawasiliano yamegeuka kichomi kwa uchumiwa taifa letu kwa ushirikiano na viongozi wasio na aibu kama hawa tulio nao sasa. Kamwe haiingii akilini kuona kijikampuni kama Group5 Security kuwa juu ya Vodacom, Tigo, Airtel au Zantel kwa kuchangia pato la taifa.

    • viongozi wanamna hii ndio wanaoendelea kuipeleka nchi shimoni nakuwauwa raia wao, sasa kama sio ukatili uliopita kiasi unaweza kuachia makapuni makubwa kama hayo yafanye biashara bila kulipa kodi wakati unajua kabisa kwamba ndio moja ya vitu vikubwa vinavyochangia kuustawi kwa uchumi then unaacha vifanye kazi bure? badala yake wanakandamiza wananchi kulipa kodi ya ju tofauti na kipato na kusabisha mifumuko ya bei na uchumi kuzid kudidimia kwa tamaa za viongozi mafisadi wasiokuwa wazalendo wala huruma kwa wapiga kura wao, ndo haohao wanaojifanya ni waumini na watoa michango mikubwa ya ujenzi wa makanisa eti kwa kujionyesha kuwa wao ni wasafi na watakatifu wakati wanachi wao wanakufa kwa umasikini kwa kukosa huduma za msingi kama vile hospilali na vifaa vya matibabu,mishahara duni na posho kwa madakitari na waalimu.

  • Sioni tatizo mtu kudai haki yake. Kama ni ya wizi basi tusubiri uchunguzi ufanyike then tutajua ukweli wa mambo!! LAKINI SIO BUSARA KUMHUKUMU MTU KWA KUDAI HAKI YAKE!!! Acheni wivu jamani..

    • Mi ninashangaa sana kwa mtu kama mbowe kusema eti haoni sababu ya mtu kama lowasa kudai haki yake.Haki ipi anayoweza kudai lowasa? uchunguzi fanywe nanani wakati wafanya uchunguzi wenyewe ni mafisadi. huu sio wivu bali ni kutaka kujua uhalali wa kumiliki pesa nyingi kiasi hiki kwa kiongozi, wakati wananchi wanakufa njaa.Watanzania tuamke na tuachane na kukubali majibu mepesi kutoka kwa wanasiasa.

  • Siyo suala la wivu au Lowassa kudai haki yake. Hapa suala ni maadili ya uongozi. Maisha yake yote, Lowassa amekuwa ni mtumishi wa umma. Wala hajapata urithi wowote wa utajiri kutoka kwa wazazi wake. Swali la msingi la kujiuliza ni kuwa, kiongozi wa umma kama Lowassa amewezaje kujilimbikizia utajiri mkubwa namna hii? Ni biashara gani anaifanya kwa kutumia ofisi ya umma? Hapa bila shaka Lowassa amejilimbikizia mali nyingi mno kwa njia zinazotia mashaka na kuna uwezekani mkubwa kuwa mali hizi wala hajaziorodhesha kwenye Sekretariat ya Maadili kama ilivyosemwa. Ingekuwa si siasa za kulindana na kuogopana hapa Tanzania, TAKUKURU ingempeleka Lowassa mahakamani kujibu mashitaka ya ufisadi kwa kuwa na utajiri wa mashaka. Kama hizo mali kweli kazipata kwa njia halali, itabidi athibitishe hilo mahakamani. Njia pekee ya kumsafisha Lowassa ni kumpeleka mahakamani, si kwa kutumia makanisa na kununua waandishi wa habari wamwandike vizuri

    • Lowassa ni mtoto wa tarishi enzi za kikoloni na mara baada ya uhuru. wanaomfahamu tangu utoto familia yake walikua watu maskini tu pale Monduli. Kwa historia yake utajiri mkubwa aliyonao ilibidi awe mrithi wa mali nyingi toka kwa wazazi wake. Kwa kuwa maisha yake yote amekua mtumishi utajiri wake mkubwa bila shaka unatokana na rushwa na ukwapuaji mkubwa wa fedha za umma.

  • Sasa hapa tatizo ni nini? Kufanya biashara siyo dhambi, wanasiasa wengi wanfanya biashara na tena za kujificha, hii biashara inafanywa kwenye makaratasi yote ya serikali. Nini tatizo? Je hao wanaopelekewa mamilioni ya dola kwenye briefcases majumbani mwao za tenda za barabara na dili chafu za waarabu kama Gaddaffi?

  • Kufanya biashara si dhambi, wala kuwa tajiri si kosa. Tunachohoji sisi Watanzania ni kuwa Lowassa amepataje huo utajiri wake wakati hajarithi mali yoyote na maisha yake yote amekuwa ni kiongozi wa umma? Kuna biashara gani kwenye ofisi za umma? Je, amejilimbikiziaje hizo mali zake zote? Swali la msingi zaidi ni kuwa hizi mali zote hizi Lowassa ameziorodhesha serikalini kama inavyotakiwa?

    Mali zake ni pamoja na hekalu la thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1 London, Uingereza, mradi wa kujenga gorofa kwenye kiwanja cha nyumba ya sanaa, Alphatel, Alpha House, Alpha Schools, pamoja na nyumba na viwanja vyake Masaki, Arusha, na nje ya nchi. Kiongozi wa umma anapataje mali zote hizi kwa mshahara wa serikali? PCCB fanyeni kazi yenu!

  • Sitegemei mfanyakazi wa serikali kuwa maskini bali wale wanaotumia madaraka yao vibaya na baadae kusema walikuwa safi huyu ndugu anafanyabiashara za wazi kwani angekuwa mwizi basi isngeliwezekana kujua kuwa ni mmiliki wa kampuni bila kuficha.

    Heri ya huyu, wanzake wengi wantumia watu na wao kujificha pale wanapostaafu ndio wanajionyesha kaka edo weka mambo wazi kwani wenzio wanajificha ile tender zote wajitumie wao kupitia vivuli vyao na pia ukiwa nazo basi hautatuibia au hautakopa kwamba ukishinda uzirudishe kaza buti tusonge mbele tunahitaji watu kama wewe tajiri na mchapakazi bila kuangalia alichonacho si kukaa tu kwenye kiti cha kuzunguka na kutembelea shangingi lenye thamani ya madawati ya shule za sekondari 4 kaka unatakiwa kumalizia ile ndoto yako ya ujenzi wa mashule kupitia nguvu za umma.

    Sasa ni kuzalisha walimu na kununua vitendea kazi,maabara ,umeme wa jua ,umeme wa kinjesi cha wanyama, nk tanakuombea ili litimie kwani TANZANIA BILA WAJINGA INAWEZEKANA AU TAZANIA NA WASOMI INAWEZEKANA TENA KWA GHARAMA NDOGO -TUKISHIRIKISHWA TATATENDA HONGERA KAKA HONGERENI WATANZANIA WOTE!!!!!!!!!!

  • TANZANIA BILA WAJINGA INAWEZEKANA AU TANZANIA NA WASOMI INAWEZEKANA TENA KWA GHARAMA NDOGO – TUKISHIRIKISHWA TUTATENDA HONGERA KAKA HONGERENI WATANZANIA WOTE!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  • tanzania tunaelekea wapi, sisi vijana na watoto wetu tutapata nini kilicho baki miaka 20 ijayo?????
    Haya mambo yana tia hasira sana……..

  • jamani siku hizi mtu akifanikiwa lazima ataitwa FREEMASON au FISADI. Mimi nasema tutofautishe wivu wa kutojituma na ufisadi. tutofautishe uvivu wa kufikiri na ufisadi. tutofautisha mawazo finyu ya kijamaa ya kupewa kila kitu na serikali na mawazo chanya ya kibepari ya RIZIKI YA MBWA IKO MIGUUNI MWAKE! watanzania hatujitumi na ni wavivu sana! hatutaki kazi ila tunataka maneno. Ukishapata kidogo unajisahau unaanza umalaya na kamari! Bosi akiondoka kazini hakuna moyo wa kujituma mpaka ufuatiliwe. Ni mara ngapi wachezaji wa YANGA na SIMBA wanafukuza kocha eti kwa sababu ya mazoezi magumu! TUSIPOKUWA MAKINI WATANZANIA WOTE TUTAKUWA KAMA HARUNA MOSHI BOBAN ASIYEONA NAFASI NA KUITUMIA KWA KULEWA MASIFA NA BAADAE TUTABAKI KULAUMU WALIOFANIKIWA! HEBU KILA MTU AONDOA WAZO LA UFISADI WA LOWASA NA AWEKE KWENYE JUHUDI ZA KUFANIKIWA BINAFSI!!

  • Tunakwenda pabaya. Tunatafutana na kuchokoana. Vijana kweli tutafika. Basi na turudishe nchi yetu kwenye Ujamaa ili tuanze foleni za sukari, chumvi, petrol na hata maji ya kunywa. Jamani wakataa pema pabaya pawaita.

  • hiyo ni haki yake na it seems mh lowasa si fisadi kamawanavyodai bali ni mjasiliamali,kumbe ana biashara zake nzuri tu

  • watanzania mnaonaje mchawi tukamkabidhi mtoto amlee(LOWASA tumpe uraisi wa nchi 2015) manake imesha kuwa kero sasa kila kukicha unasikia habari za lowasa na zote ni za kifisadi na za kujilimbikizia sii pesa tu bali mamilioni ya pesa pamoja na kushika viwanja vikubwa sehemu za mijini.Labda siku moja itatokea miujiza na tutaweza kujua hawa viongozi wetu wanatupeleka wapi watanzania.

  • Nipe namba ya Rowasa niongee naye ili anipe uwazi kwani sina uhakika kama kweli yanayoandikwa hapa anayasoma au la!

  • Mheshimiwa Luluhasa alikwishafahamika tangu mbio za kumtafuta mgombea Uraisi kwa tiketi ya CCM(1995) kuwa ana utajiri usioelezeka chanzo chake. Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alimkataa.Sisi leo tunamfagilia.
    Ilisadikika kuwa yawezekana ukwasi aliokuwa nao ulitokana na nafasi zake za uongozi alizoshika katika utumishi wa umma.
    Tangu hapo hajaacha kutafuta nafasi za uongozi kwa kuwa ndiyo kiini cha ukwasi wake pia kizingti chake kiliishatoweka na hakuna mtu mwingine anyeweza kumwambia kwa ujasiri kuwa” Eee bwana tupishe kwakuwa ukipewa nafasi utaitumia kwa manufaa yako binafsi kutumia rasimali unazopaswa kuzitumia kwa wote”. Akiacha uongozi hawezi tena kupata fedha au hata kuendesha biashara zake. Angalikuwa ni mjasiriamali kweli angalijivua gamba kama Rice Tamu.
    Kuwa mjasiriamali si kosa na mjasiriamali mara zote huangalia fursa ( opportunity to exploit) na kuitumia mara moja. Luluhasa amekuwa akiona fursa na kuutumia kwa faida yake na Taifa kidogo.
    Watu wa aina hii wapo katika kila taaluma mfano wanasiasa, madaktri, waalimu, waandishi wa habari usalama wa Taifa orodha ni ndefu. Wakati mwingine watumishi wenye jukumu la kuzuia wamekuwa wakitoa ushirikiano mzuri kufanikisha nia mbaya. Ukimwangalia Luluhasa ni mjasiriamali hatari sana, ikiwa aliweza kuona fursa wakati wa uongozi wa awamu ya kwanza, wakati wa Azimio la Arusha itakuwaje leo wakati wa uongozi holela. Hoja hapa ni kuzidiana tu, lakini kama kutumia fursa kwa manufaa binafsi asiye na kosa na awe wa kwanza kutosa jiwe. Mwalimu alitosa jiwe kwa Luluhasa kwa kuwa alikuwa huru. Hakuwa na mzigo. Viongozi wa sasa wanamizigo wanaogopa kubebeshwa mara wakimgusa Luluhasa.
    Lakini, kwa upande wa pili kazi ya serikali, yenye vyombo vya usalama na ulinzi wanakuwa wapi mpaka mtumishi wa umma anapata mwanya wa kutumia nafasi yake vibaya katika utumishi wa umma? Jukumu kubwa la serikali yoyote duniani ni kusimamia watumishi wake vizuri na kuona hawakiuki sheria na maadili ya kazi zao. Kushituka baada ya mtumishi kuwa tayari amejilimbikizia mali ni sawa na mlinzi wa benki kuacha benki yake wazi ili mwizi aibe na baada ya kuanza kuzitumia pesa halafu mlinzi ananza kumtilia shaka kuwa huenda aliiba katika benki ninayoilinda. Jambo hili halitakuwa na maana sana.
    Tatizo hili ni kubwa mpaka hapo tutakapotenganisha biashara na utumishi wa umma na kuwasimamia vizuri watumishi.Tukisema wasipewe uongozi kwa sababu wana mali, hili pia litakuwa Taifa la wabaguzi kwa misingi ya mali na katiba yetu inakataza kubagua watu wake kwa misingi ya aina yoyote ile. Hoja watu wapewe uongozi lakini waangaliwe na kusimamiwa ili wasitumie vibaya madaraka yao. Wakigundulika wachukuliwe hatua kali

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *