Watoto wa Trump, Clinton ‘damudamu’

Jamii Africa

URAFIKI wa Ivanka, mtoto wa Rais Mteule, Donald Trump na Chelsea, binti wa mpinzani mkubwa wa baba yake, kwenye kinyang’anyiro cha urais wa Marekani, Hillary Clinton, “hautakufa.”

Wote wawili; Ivanka na Chelsea, kwa nyakati tofauti, baada ya kupatikana kwa ushindi wa Trump, Novemba 13, 2016, wamewaeleza waadishi wa habari kwamba, uhusiano wao, bado mzuri na hauwezi kuhitimishwa na matokeo ya siasa.

Uchaguzi wa Marekani uliomuibua Trump kuwa mshindi, ulifanyika Novemba 8. Rais mteule ataapishwa Januari 20, mwaka  kesho, 2017.

Ivanka amesikika akisema kwamba urafiki wake na Chelsea, ni zaidi ya undugu na kwamba marafiki hao hawafichani kitu, kinachopaswa kufahamika kwa mwingine miongoni mwao.

https://www.youtube.com/watch?v=Uf5rbezYWUo

Anasema  siasa haikuwa chanzo cha kufahamiana kwao na hata kujenga urafiki, hivyo haiwezi kuwa chanzo cha kuwatenganisha.

“Tumefahamiana na Chelsea miaka mingi iliyopita, tunaheshimiana na kupendana kwa dhati. Bahati kubwa nyingine ni kuwa familia zetu; waume zetu ni marafiki pia,” anaongeza Ivanka.

daughters

Chelsea akizungumza urafiki wake na Ivanka, anasema kamwe hakuwahi kufikiri siasa inaweza kuwa chanzo cha kushindwa kuelewana kwao.

Anasema amekuwa akiheshimu msimamo wa siasa wa Ivanka, huku rafiki yake huyo akiheshimu mtazamo na ufuasi wake kwenye siasa.

Ni wazi kuwa Chelsea ni shabiki wa chama cha familia yake, Democrat, huku Ivanka akiaminika kuwa mfuasi na mpenzi wa chama cha baba yake, Republican.

https://www.youtube.com/watch?v=2PvZqGbA-5c

“Mtu akituona leo tuko pamoja anadhani tumeanza urafiki karibuni, hapana, tumekuwa pamoja kwa muda sasa, tukishirikiana kwa mambo mengi ya msingi, yakiwamo ya familia zatu, hivyo, tuko pamoja sana na huenda urafiki wetu ukaimarika baada ya uchaguzi,” anadokeza.

Katika kampeni za uchaguzi wa Marekani, Trump na Hillary ndiyo walikuwa “mahasimu” wakubwa katika kinyang’anyiro cha kupata ridhaa kuongoza taifa hilo kubwa, tajiri na lenye nguvu kubwa za kivita.

Wagombea wengine kwenye uchaguzi huo walikuwa ni Jill Stein wa Green Party na Gary Johson wa Libertarian.

Trump ana watoto watano, huku Hillary akiwa na mtoto mmoja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *