Ili Chadema kiweze kuwa Chama mbadala, kinahitaji major overhaul ya kiuongozi na utendaji. Matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2010, yamoenyesha wazi kuwa safari ya Chadema kuinga Ikulu na kushika hatamu ya kuongoza Tanzania ama ni ya kufikirika sana au ni mdadi ambao umejaa kwenye mioyo ya watu na wapenzi wa Chadema lakini hawaelewi kwa undani ni namna gani ya kujikit ndani ya mfumo wa siasa.
Sitarudia sana nilichosema kenye zile mada nilizoichambua Chadema kabla ya uchaguzi, lakini kama wana masikio safari hii na ni wasikivu mpaka ndani ya mioyo yao, basi wafanyie kazi sasa hivi mapendekezo ya Mchungaji.
La Kwanza, Mwenyekiti wa Chadema na Uongozi wote wa Chadema unahitaji kubadilishwa. Freeman Mbowe ajiuzulu Uenyekiti na focus yake iwe Bungeni na si kwingine.
Pamoja na hili la Freeman kujiuzulu, aidha Wabunge wote wa Chadema wajivue majukumu ya kuongoza Chama kama Watendaji wa Chama na nafasi ndani ya Chama na wawekeze nguvu zao ndani ya Bunge na kuachia safu mpya ya Uongozi wa Chama.
Freeman, kama mwenyekiti, hakuweza kukijenga Chama kikawa imara ipaswavyo na hata kukiandaa kikamilifu kwa ajili ya Uchaguzi Mkuuu huu uliopita. Freeman bado hajawa Mwanasiasa mwenye mvuto na uwezo wa kufikisha ujumbe wa kuuza Itikadi na Sera za Chadema kikamilifu kwa Watanzania. Atafaa sana kwenye utendaji wa Kiserikali Bungeni na itambidi aachie Uenyekiti kama ana ndoto ya kuona Chadema inapewa dhamana ya kuongoza nchi.
Binafsi, ningependelea Dr. Slaa awe Mwenyekiti wa Chadema na asiwe mbunge au kuwa na kazi ingine yeyote bali kukijenga upya Chama. Tumeona ni jinsi gani alivyo na uwezo wa kuvuta watu na akipewa nafasi hii na nyenzo za kutosha, anaweza kukijenga Chama kikawa imara sana na hata kuongeza wigo wa kuuzika kwa Chadema mpaka kila kona ya Tanzania.
Sambamba na Dr. Slaa kama Mwenyekiti, Chadema na Dr. Slaa vinanahitaji mtu mwenye uwezo kama Willy Lwakatare kama Katibu Mkuu kuratibu shughuli za Chama na kusaidiana katika kukijenga na kukiongoza Chama.
Hawa wawili wakipata mtu mwenye ushawishi na nguvu kama Makamu kutoka Zanzibar, watakuwa na uwezo wa kuwekeza nguvu za kukijega upya Chadema mithili ya Mzee Malecela na Mangulla walivyofanya kazi pamoja ya kukiimarisha CCM na kuchukua TAMISEMI 2004 na kuleta Tsunami ya 2005.
Pamoja na kubadilisha safu ya uongozi na hata kuubadili mfumo wa kiuongozina kiutendaji, Chadema inapaswa kupitia upya Sera na Itikadi zake kwa kubainisha na kuyaelewa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2010.
Chadema ni lazima kiwe na taswira na mfumo mpya ambao haufanani na CCM, CUF, TLP au NCCR na uwe wenye kujenga demokrasia ya kweli kwa kutumia sauti za wanachama na kuwaelewa Watanzania na mahitaji yao. CCM wamejifunza makosa ya kutokusikiliza maamuzi ya wanachama wake katika ngazi za majimbo wakati wa kura za maoni na ndio maana KInana leo analalamika na anasahau ni wao katika ngazi ya Taifa waliamua kubadilisha zile sauti za wanachama wake.
Pili, katika kujijenga upya huku kwa Chadema, ni lazima kijijenge kikamilifu katika maeneo yote ya Tanzania na hasa Zanzibar. Sijali watakaodai kuwa mbona CUF kiko Zanzibar pekee, bali ni lazima Chadema kiwekeze nguvu kubwa sana kupata uhalali na kukubalika Zanzibar kama kinadiriki kuongoza Serikali ya Muungano na si Tanganyika pekee.
Aidha katika tathmini ya uchaguzi wa mwaka huu, Chadema kianze leo hii kujijengea mazingira mazuri ya kushinda tena majimbo yote waliyoshinda mwaka huu, waanze kujenga mazingira ya kujijenga kichama na wanachama wenye uwezo wa kuweza kusimama na kugombea katika chaguzi wa TAMISEMI 2014 kwa kuhakikisha wanakuwa na watu wenye uwezo wa kushinda Udiwani na kuwa na uwakilishi wa kutosha katika Serikali za mitaa na mikoa.
Chadema ni lazima kifanye tathmini ya udhaifu wa kiutendaji na kiuongozi ambao kulikifikisha Chama ama kukosa wagombea au watendaji na pia kukosa kuungwa mkono kwa kutosha na Wananchi hasa vijijini.
Hii ina maana kuwa Chadema ni lazima ijisuke upya katika kila kata, tarafa, wilaya na hata mkoa na kuhakikisha kuwa kina jenga ushawishi wa kukubalika leo na si kungojea kesho kutwa!
Pamoja na jitihada za kujikita Zanzibar, Chadema inahitaji kuwekeza nguvu kubwa kwenye maeneo mengine ya Tanzana bara ambayo kura zao zilikuwa dhaifu mno. Mikoa kama Mtwara, Lindi, Ruvuma, Dodoma, Singida, Morogoro, Tabora, Shinyanga, Kigoma, Rukwa, Mbeya, Tanga na Pwani, iwe ni mijini au vijijini, ni lazima kijijenge upya na kwa haraka sana na si kusubiri 2015 na kuuza hoja ambazo hazieleweki sawasawa kwa Watanzania. Pia itakuwa muhimu kwa Chadema kuwekeza katika ujenzi wa ofisi kuu katika kila Wilaya na Mkoa.
Tatu, ujumbe wa Chadema uwe ni kuleta mabadiliko kwa Tanzania. Kipaumbele kiwe kwenye kuondoa Umasikini, Ujinga, Maradhi nakupunguza deni la Taifa. Bungeni, kina Mbowe, Mnyika, Zitto, Shibuda waungane na wenzao wa CUF, NCCR na TLP kujenga vyema upinzani wa kuiratibu Serikali hata kama idadi yao ya kura ni ndogo. Wote wawe na ushirikiano kwa ajili yamanufaa ya Watanzania na si kujitenga kwa manufaa ya kichama kama CCM.
Dr. Slaa, Lwakatare na wengine kwenye safu ya uongozi wa kichama, kazi yao iwe kunadi Itikadi na Sera za Chadema, kuelimisha Wananchi kwa nini Chadema ni chama bora na kitafanya nini kwa Watanzania. Pamoja na kujiuza kisera na kiitikadi, Uongozi mpya uwe mstari wa mbele kwenye suala la kudai Katiba mpya na Tume mpya ya uchaguzi. Hili liwe ni shinikizo la kuanza siku Kikwete anaapishwa kuwa Rais na si kusubiri 2014.
Nne, umoja ni nguvu, utengano ni dhaifu, sasa ni wakati muafaka wa Chadema kukaa chini tena na Vyama vingine vya upinzani na kuanza kujisuka ama viungane au viwe na makubaliano ya kweli ya kuwawezesha kuiangusha CCM ambayo itarudi kwa nia ya kujisahihisha katika kipindi cha miaka hii mitano inayokuja, pamoja na kuwa na mvutano wa ndani kwa ndani wa madaraka na uongozi.
Ukifanya tathmini ya matokeo ya uchaguzi wa 2010, kwa haraka haraka kuna majimbo karibu 15 ambayo yangeweza kwenda kwenye upande wa upinzani kama kungekuwa na ushirikiano na muafaka wa kugawanyana na kuachiana majimbo ili kupunguza nguvu za CCM Bungeni kwanza. Lakini kutokana na kila Chama kutaka kushika hatamu na kufanya mambo dakika za mwisho, CCM imepata ushindi wa kubahatisha kutokana na kura kugawanyika.
Tano, Dr. Slaa pamoja na kazi yake hii mpya ninayoshauri, yeye na timu yake itabidi waanze kazi ya kujisuka kwa ajili ya Chaguzi zinazokuja kwa kuhamasisha kupata wanachama zaidi, kuhakikisha wanachama wao wanajiandikisha kupiga kura na kutoa elimu ya Uraia kwa Wanachama wake ili uchaguzi mkuu utakapofika, wanachama na wapenzi wa Chadema wawe tayari.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa na kile kitabu cha CIA, takriban asilimia 43 ya Watanzania ni chini ya miaka 14. Kati yao kundi hili, 30% watakuwa ni wapiga kura wapya 2015, hivyo Chadema ilenge kujijenga kwa Chipukizi na vijana ambao leo hii wana umri kati ya miaka 13 hadi 17 kwa kuwahamasisha kupitia elimu ya Uraia na kuwafundisha Sera na Itikadi za Chadema.
Aidha kwa kuwa kuna muelekeo wa Chadema kuwa na ufuasi mkubwa wa walioko vyuoni, basi hawa walio wasomi watumike ipaswavyo kukijenga Chadema katika majimbo yao, mitaa yao na mpaka kwenye kata kwa kuwafikia Watanzania naa kusaidiana na Dr. Slaa kukijenga Chadema na kunadi Sera an Ilani zake.
Kama Chadema watakuwa wasikivu na kufanyia kazi mapendekezo ya waliokishauri awali na hata sasa, watakuwa na nafasi nzuri ya kuongeza nguvu zao Bungeni hata kupita lengo lao la viti 70 bungeni ambalo hawakulifikia mwaka huu.
Uamuzi ni wao kujiimarisha na kujijenga upya, lakini wakae macho wakitambua kuwa CUF kinashika moto na matokeo ya muafaka Zanzibar, yataleta ushindani mkubwa kwenye Muungano na kuwa CCM sasa inajipanga kwa haraka mno kuhakikisha kuwa kinajisafisha na ikiwezekana Amani Iwe Nanyi,
Camerlengo
Plu Camerlenghi- Revolutionary Right Reverend Kishoka
Haya ni mapendekezo safi ya kufanyiwa kazi tena haraka sana.
Kuonyesha uelewa na ukomovu CDM kianzishe jumuiya ya vijana very strong kuanzia vijijini, kata,tarafa, wilaya, mikoa hadi taifa, bara na visiwani. Kujenga makada commited kwa chama watakao elewa malengo ya chama kuchukua dola kwa sanduku la kura, wawe trained kuelewa sera za chama na madhumuni ya chama. amabiu kuu ikwa ni kumkomboa Mtanzania toka makucha ya chama tawala kinacho lea mafisadi na wezi wa rasirima la za taifa letu.Vijana na makada wapitishwe semina za kuwajenga, isiwe moto wa juujuu tuu wa maandamano na mikutano, tujenge misingi imara ya makada wa chama, watu waelimishwe chama kushika dola!!!!!!!!
Thanks FikraPevu, ubarikiwe. Mungu anachukia wezi, hiyo inaleta laana kwa taifa letu.
Uko sawa Kaka!
Ila mchungaji anapopendekeza Dr Slaa kuwa Mwenyekiti wa Chadema – sikubaliani naye hata kidogo. Nafasi aliyo nayo Dr. Slaa kama Katibu Mkuu wa CDM ni nzuri kwani Katibu ndiye mtendaji mkuu wa Chama. Mwenyekiti sio mtendaji mkuu. Na tumeona Dr Slaa anavyozunguka nchi nzima kunadi chama na anawavuta watanzania wengi kujiunga na chadema.
Kwa wazo la Mbowe kujiuzulu, hiyo itategemeana na katiba ya chama inasemaje, kama iko wazi kwa nafasi ya Mwenyekiti wa chama kuwa katika kiti hicho kwa muda maalum ndo itakuwa suluhu ya yote, lakini kama haiko wazi – tuwasubiri wajumbe wa Kamati kuu ya CDM ndo watafanya maamuzi.
Kuhusu kuunda mtandao wa kiuongozi kutoka ngazi ya chini – nakubaliana na wewe kwa asilimia zote. Huku kwetu uongozi upo ngazi ya mtaa hadi mkoa – sijui penngine kuko vipi
guys you need to continue to be tough to liberate the country, tanzania which is almost sold by the recent government in power
I think what chadema should do is to invest in the rural areas by educating the mass who do not yet know the goodness of having a multiparty democracy. the rural mass is still in the cave. they need to be liberated by you, chadema.
CHADEMA can do all those things kwa kuwa naamini wana viongozi wasikivu na wapenda maendeleo,wakumbushe kuhusu umuhimu wa kuwatambua wanafiki wanaojidai wapigania haki na maendeleo ndani ya chama kumbe wametumwa,tunazifahamu siasa zetu jinsi zilivyo zakizandiki,wawatambue watu kama hao na wajue namna ya kuishi nao kwa utaratibu,kwa sababu in reality wako kwa ajili ya kuzima mema yatakayoanzishwa na CHADEMA ndio maana wanakubali kutekeleza kama walivyotumwa,hawataruhusu hayo mema kutendwa kwa sababu yataruhusu chama kukubaliwa zaidi na jamii husika kitu ambacho waliowatuma hawatakikubali.
Naomba wakati wa kutoana maoni watu watafakari kwanza hoja iliyoandikwa Freeman sio katibu mwenezi wa chama hivyo naomba mtu huyo mwenye dhamana ya kunadi sera na itikadi za chama afanye hivyo. Pia naomba nimpongeze mwenyekiti wangu kwa kufika hapo alipo maana kutoka wabunge 4 hadi 80 sio mchezo ndugu naomba tuwe tunatoa pongezi kwanza kwa viongozi wa chama hasa Dr Slaa ambaye alipeperusha bendera ya chama mpaka tukafika hapo.
Wachangiaji wanatoa fikra nzuri ila wanakaa pembeni na kunyoosha kidole kuwa CDM wafanye vile na hivi. CDM ni nani? mageuzi ya nchi hii hayawezi kuletwa na viongozi wachache wa CDM ilihali wapiga debe tuko nje tukishangilia tu. Tujiunge nao kisha tushinikize kufanya vile na hivi. Ni vyema Mchungaji aanze ili atoe maoni hayo vikaoni.
Mtoto wa Bata hafundishwi kutafuta Chakula, wala Mtoto wa Nyoka hafundishwi kuuma. Naaaniaaa hawa Jamaa walisha Jipanga Ambacho na dhani ni suala la Implimentation. BiG Up CDM Mnaweza.
Chadema wamfukuze SHIBUDA ndani ya chama mara moja yule ni shushu wa chama cha mapinduzi wafanye maamuzi magumu kama yale ya madiwani wa Arusha.
mchungaji katumia busara sn kuandika ujumbe huo
japo ni ngumu kufahamu makusudi yake. ila ujumbe wake una hoja za msingi kutafakari.
CHADEMA FANYENI YA KWENU
Ndiyo CHADEMA tunawategemea kwakuwa hamna mchezo na yeyoye hata kama ni Mheshimiwa kama mlivyofanya kwa Madiwani wa Arusha. Anaekwenda nje ya mstari mnammwaga, siyo wenzenu wa CHAMA CHA MAFISADI (CCM), wanaogopana. Wanapeana rushwa kila chaguzi mpaka chaguzi za vikao vya harusi zao, usiwaamini
Ninawapa hongera viongozi wa CDM kwa kuelimisha watu.Nawaomba wasikate tamaa na imani siku moja tutaongoza