Zitto aibuka sakata la Urais 2015, asema ukweli utaanikwa

Jamii Africa

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe (pichani), ameibuka na kuzungumzia sakata la urais mwaka 2015 alilohusishwa nalo na wabunge wenzake mjini Kigoma na hatimaye wabunge hao kukanusha baada ya kuibuka kwa mjadala mkali dhidi ya kauli zao.

Zitto ambaye amekuwa akiandamwa mara kadhaa na wanasiasa ndani na nje ya chama chake, baadhi wakimtuhumu kuwa mamluki na wengine wakimuekezea kuwa ni mwanasiasa mwenye malengo makubwa hapo baadao, amesema:

“Katika gazeti la Mwananchi la tarehe 23 Julai 2012, kulikuwa na habari yenye kusomeka ‘Wabunge wamsafishia Zitto njia ya Urais 2015’. Habari hii imeleta mjadala mara baada ya kutoka na kusomwa. Mjadala umekuzwa zaidi baada ya Wabunge ndugu Halima Mdee na ndugu Joshua Nassari kukanusha maneno waliyonukuliwa kusema. Napenda kusema masuala yafuatayo.

“Moja, Waheshimiwa Wabunge Halima Mdee, Joshua Nassari, Kangi Lugola, Esther Bulaya, Deo Filikunjombe, Raya Ibrahim, Amina Mwidau na David Kafulila walihudhuria tamasha la vijana wa Kigoma All Stars kwa kualikwa na Mratibu wa kundi hilo Mwasiti Almasi. Wabunge wengine walialikwa lakini hawakutokea wakiwemo Joseph Mbilinyi, David Silinde, Amos Makala, Vicky Kamata na Peter Serukamba. Wabunge hawa hawakualikwa na mimi na wala sikufanya mazungumzo nao yeyote ya awali au kuwaambia au kukubaliana nini cha kuzungumza au hapana. Tamasha lilikuwa la muziki na halikuhusika kabisa na siasa.
“Waheshimiwa wote walipewa nafasi ya kusalimia na wote walizungumza. Wabunge waliozungumza kwa muda mrefu kidogo ni ndugu Halima Mdee, Joshua Nassari, Deo Filikunjombe na Kangi Lugola.

“Hotuba za Wabunge wote zilirekodiwa kwenye video neno kwa neno na video hizo zitawekwa wazi kwenye blogu yangu kama sehemu ya documentary ya tamasha lile la kihistoria.

“Pili, sikuhusika kwa namna yeyote ile na kuandikwa kwa habari hii iliyozusha mjadala. Wala sikujua kama habari hii ingeandikwa maana katika ziara ile sikuita mwandishi hata mmoja maana nilitaka liwe tukio la Kigoma tu.

“Kama mwandishi kaandika ambayo wabunge hawa hawakuyasema basi itaonekana kwenye videos hizo. Wabunge wenyewe wanajua kwenye nafsi zao nini walisema Kigoma na kipi kiliwasukuma kusema walioyasema Kigoma. Nisingependa kuhusishwa kwa njia yeyote ile na matamshi yao, habari iliyowanukuu na hata makanusho yao. Maana mwisho wa siku ukweli ndio utasimama.

“Suala la Urais lisitupotezee muda kwani kuna mambo mengi sana ya kujadili kuhusu nchi yetu. Taharuki ambazo watu wanazipata masuala ya urais yanapotajwa zinashangaza sana.

“Chama changu bado hakijatangaza rasmi mchakato wa kupata mgombea Urais. Hivi sasa chama hakina mgombea Urais mpaka hapo mchakato utakapotangazwa ambapo wanachama wataruhusiwa kuomba kupeperusha bendera ya chama. Mwanachama wa chama chetu atakaye kubalika na jamii na wajumbe wa mkutano wa uteuzi ndiye atakuwa mgombea wetu. Kwa sasa hayupo na hivyo tusipoteze muda kujadili jambo hili.

“Mzee Thabiti Kombo alituachia usia tunapokuwa tunazungumza. Alisema ‘weka akiba’ sio akiba ya fedha, bali ya akiba ya maneno. Tuweke akiba ya maneno. Tusimalize yote.”

Taarifa yake kamili na majibu ya baadhi ya wachangiaji.

http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/297173-urais-halima-nassari-na-kigoma.html

15 Comments
  • Kwa namna mambo nchini mwetu sasa, yawezekana ni kweli huyu bwana ni mamluki ingawa ni kweli kuwa huyu bwana ukimlinganisha na JK, huyu anaonyesha uwezo wa kuongoza nchi upo.

    Lakini kwanini anakimbilia na kulilia Ikulu? Ana biashara gani anaenda kuifanya? Namshauri, asubiri kwani yeye bado mdogo, kama ni Ikulu ataikuta kama ni bahati yake.

    • Nami nafikiri Mh. Zitto asubiri haswa wakati husika maana kama atakuwa na haraka ya kutaka kufika ikulu basi anaweza kuwa na lake jambo moyo yaani kuwatumikia wananchi vizuri au kutowatumikia wananchi kabisa na kufanya biashara kama watangulizi wenzake kasoro JEMBE la ukweli Mwl. J. K. N

  • Mi nadhani kwa suala la Mh. Zitto kuwania au kutowania kugombea urais 2015 ni vema aachiwe mwenyewe hadi hapo atakapoweka wazi. Na hili la kujaribu kuzungumzia sana kuhusu nia yake Mh. Zitto kugombea urais hali wakati mwenywe hajatamka nafikiri hizi ni hofu za baadhi ya wanasiasa kwani wanaona kuwa Mh. Zitto anakubalika.

    Watanzania tuwe na subira kama Mh. Zitto alivyokuwa na subira kuweka wazi nia yake.

  • Swala la urais wa Zitto hayo ni majungu ambayo hayana mashiko yoyote licha ya kwamba sio dhambi mtu kuutaka urais na kuna taratibu zake kuna taratibu zake chamsingi tukuali kwamba Mh.zitto anaweza kuwa rais wa nchi hii kwani ni viongozi wangapi wako madarakani kwa kubebwa? Habari za kuwa mamluki lita julikana tu kwani anakuwa mamluki kwa faida ya nani hakuna Mh. zitto naye ni mwanadamu mwenye mapungufu kama binadamu yoyote hukosea na kuhitaji ushauri kama m2 yeyote kikubwa ni kwabwa anastrength kuliko weakness,

  • Jamani kwani kuna kosa gani Mh. Zitto kuwa Rais wa Nchi hii? Naona kama imekuwa gumzo sana. Mimi nawashauri wote wanaolizungumzia suala hili waone kwamba ni jambo la kawaida sana na wala sio issue sana kwani kila Mtanzania anaekidhi vigezo vya kuwa Rais anaweza kuwa Rais kwa mujibu wa sheria za nchi hii. Hivyo tuachane na suala hilo kwa sasa kwani si wakati wake. Wakati ukifika mambo yatawekwa hadharani. Kwa sasa tufanye masuala mengine ya maendeleo ya nchi yetu.

  • INAWEZEKANA HAYO MANENO YAKAWA NA UKWELI NDANI YAKE LAKINI UTHIBITISHO ZAID NTAMTAFUTA MH ZITO APATE KULIONGELEA ILO

  • Mi nashauri Mh Zitto angesubiri kwanza mpaka 2020,ingekuwa vizuri sana na angekubalika zaidi kuliko agombee mwaka 2015 kwani mwaka huo kutakuwa na ushindani mkubwa sana ndani ya chama cha Chadema

  • Nampenda zitto lakini uraisi asubiri kwanza zitto anatakiwa awe waziri mkuu badae ndipo awe raisi

  • Zitto ajipime kwanza, siuoni uwezo wake. hatukuwahi kumsikia Dr. Slaa akiongelea kuutaka uraisi mpaka wakati ulipofika. mbona yeye ana kimbelembele hivyo. Hana uwezo wa kuongoza nchi. Yeye na Mkwere wote ni sawa tu

  • Zitto ajipime kwanza, siuoni uwezo wake. hatukuwahi kumsikia Dr. Slaa akiongelea kuutaka uraisi mpaka wakati ulipofika. mbona yeye ana kimbelembele hivyo. Hana uwezo wa kuongoza nchi. Yeye na Mkwere wote ni sawa tu.
    Angoje Muda na aendelee.

  • ni vizuri zito anapoonyesha nia ya kugombania, manake mpaka 2015 ifike tutajua aina ya mtu anayetaka urais. kimsingi sina imani na zito kwenye suala la urais, nijuavyo rais bora ni yule anaejifunza kutoka kwa watu mwishowe watu wanamkubali hata yeye(zitto) anao muda wa kutosha kutushawishi kama anastahili, the same applies to lowassa.tofauti na kama angetushtukiza siku za usoni, tungepata shida kumwelewa. siasa ni mchezo wa kubadilika.

  • mh. zitto anapoonyesha nia ya kuwa rais yeye pamoja na Lowassa ni jambo zuri kwani tunao muda wa kumchunguza kuanzia sasa mpaka ifikapo 2015 tutajua kama anafaa ama la, na hii ingekuwa tofauti kama angekuja kutushtukiza kipindi hicho. jambo linalonipa hofu ni uwezekano wa chadema kugawanyika na hii itapelekea ushindi mkubwa kwa ccm kwani hatujui kama chadema inataka zitto agombee nafasi hiyo muhimu ama la. sidhani kama zitto anakubalika kama anavyodhani yeye mwenyewe au ndani ya chama chake,manake viongozi wa chama wanatoa kauli tofauti na za zitto wanaposema bado hawaja amua namuda ukifika watapitisha kama chama wakati zitto yeye ameamua na ameshawaambia wapiga kura wake wa kule kigoma kwamba atakaporudi tena atakuja kama mgombea urais, lakini bado najipa matumaini kwamba siasa ni mchezo unaobadilika.

  • Jamani Mh. Zitto kasema maneno kwa hekima ebu tujikite katika siasa zenye kuleta maendeleo tujadili mambo na kupendekeza masuluhisho kwa kadiri tufikiriavyo ili kujenga taifa letu, mimi binafsi namfahamu Mh. Zitto tangu tukiwa wote katika Asasi ya NYF pia Mh.Halima Mdee namfaham pia kweli Mh. Joshua simfahamu vizuri japo nilifutilia kampeni zake na kuona ishara njema ndani yake wote wana busara ya kutosha,

    Millengo J,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *