Bi. Mwajuma asababisha TBC1 kukatiza matangazo ya Igunga

Jamii Africa

Mwanamama mmoja Bi. Mwajuma Shaaban wa huko Igunga amezungumza kwa hisia kali kwenye TBC1 ya Taifa ambapo alionekana kukanusha uvumi wa kuwa alikuwa ametangazwa amekufa na hivyo asingekuwa na haki ya kupiga kura. Mwanamama huyo ambaye alijionesha kuwa ni shabiki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CDM) alizungumzia jinsi gani balozi wale wa nyumbi kumi kumi alivyojaribu kutaka apewe namba ya kadi yake ya kupigia kura kitu ambacho mama huyo alikataa.

Kutokana na kukataa kwake huyo maam huyo alidai balozi huyo akaanzisha visasi na hata kumzulia kuwa amekufa ili asije kupiga kura. Mama huyo alidai kuwa balozi huyo alikuwa anatumia mbinu ya kuwa anamsaidia mama huyo chakula na hivyo angetakiwa arudishe fadhili kwa kukiunga mkono chama cha balozi huyo.

Mazungumzo hayo ya mwandishi wa TBC1 na mama huyo yawezekana yalivuta usikilizaji wa watu wengi na hasa akionesha mbinu ambazo huenda zimetumika kuzuia watu wengine kupiga kura au hata kuwashawishi kwa kutumia vitisho ili waunge mkono chama cha kisiasa. Mama huyo ambaye ameonekana kujiamini aliapa kuwa hakuwa tayari kununuliwa na alitumia muda wake kwenda kuhakikisha jina lake lipo na hatimaye aliweza kupiga kura kinyume cha matarajio ya wale waliomzulia kifo.

Baada tu ya kurusha mahojiano hayo ya moja kwa moja na licha ya juhudi za mwandishi kujaribu kumzuia mama asitaje vyama vya siasa madhara yalikuwa yamekwishafanyika. Matangazo ya moja kwa moja ya TBC1 kuhusu Igunga yakakatishwa karibu dakika kumi kabla ya muda wa saa na Televisheni hiyo ya taifa kuanza kurusha matangazo ya taarab.

Mama huyo alidai pia kuwa kutokana na msimamo huo maisha yake sasa yako hatarini na hata alipoulizwa itakuwaje kama chama alichokitaka kitashindwa alijibu kwa kujiamini kuwa ‘haijalishi kishinde au kisishinde” ataendelea kuwa pamoja naye. “Kwani babako akiwa maskini utamkimbia? Si utakuwa naye labda hata yeye siku moja atafanikiwa” alisema mama huyo kwa sauti ya ujasiri iliyojaa uchungu.

10 Comments
  • Hakuna jambo muhimu duniani kama uhuru wa binadamu kujiamulia anachokitaka. Bi. Mwajuma wewe ni chanzo cha ukombozi igunga, umenikumbusha yule bibi wa marekani aliyekataa kumpisha kiti kijana wakizungu kwenye daladala miaka mingi ilopita anakumbkukwa leo kama mwanaharakati wa mwanzo kabisa wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi huko marekani. nikirudi kwaupande wa TBC wameonesha udhaifu na kusema kweli hayo ndio matunda ya kuweka watendaji vibaraka kwenye vyombo vinavyotakiwa kuwa huru kama TBC. wazime matangazo ama kufanya lolote lile muda wa mageuzi umefika na hakuna anayeweza kuyazuia. asiyejua kifo na achungulie kaburi, hamkuona zambia Rupiah Banda alirushiwa kampeni kwenye chombo cha umma kama ninyi TBC lakini King Cobra akashinda, someni alam za nyakati mtaimbuka ninyi.

  • Hakuna jambo muhimu duniani kama uhuru wa binadamu kujiamulia anachokitaka. Bi. Mwajuma wewe ni chanzo cha ukombozi igunga, umenikumbusha yule bibi wa marekani aliyekataa kumpisha kiti kijana wakizungu kwenye daladala miaka mingi ilopita anakumbukukwa hadi leo kama mwanaharakati na mwanamapinduzi wa mwanzo kabisa wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi huko marekani. nikirudi kwaupande wa TBC wameonesha udhaifu na kusema kweli hayo ndio matunda ya kuweka watendaji vibaraka kwenye vyombo vinavyotakiwa kuwa huru kama TBC. wazime matangazo ama kufanya lolote lile muda wa mageuzi umefika na hakuna anayeweza kuyazuia. asiyejua kifo na achungulie kaburi, hamkuona zambia Rupiah Banda alirushiwa kampeni kwenye chombo cha umma kama ninyi TBC lakini King Cobra akashinda, someni alama za nyakati mtaumbuka ninyi.

  • kama mtu anatoa hizia za kweli na kueleza uma mambo ya kweli tupu kwanini adhulumie haki yake kama mtanzania?
    Angalieni sana muda wenu ukiisha kuongoza hii nchi mtaenda wapi? au ndo maan amnalilia Uraia wa nchi mbili ili baada ya mambo kuwa mabaya kwenu mkimbilie nchi ya piti kiuraia? Mmama huyu kaeleza ukweli nda maana Shaban Kisu ameamua kukatiza matangazo… Huenda Kisu amegopa ajikute kama yaliyomtokea TIDO MHANDO!
    au Yaliyomtokea RPC wa Arusha kipindi cha uchaguzi uloopita Basilio Matei…. kisa walifanya kazi kwa maslai ya taifa ndo maana wakafutwa kabisa katika anga la kusikika vyomboni……..chunga ninyi watu ……

  • mama umeonyesha mfano bora,uko tayari kuufia ukweli hata kama utawaumiza wabaya wako….jipe moyo mama unapigania haki ya kizazi kilichopotoka…polepole tutafika kwani tayari kuna mwanga wa matumaini.

  • huyo mama ni mfano wa kuigwa, ni mtu anayeweza kuusimamia ukweli wa anachokiamini, watu wengi tunaamini katika uozo wa waliotutangulia katika madaraka tuliyo wakabidhi kwa kura zetu, lakini hatuna ujasiri wa kuwaambia ukweli ingawa tukiwa hoi kwa maumivu na tukiwa nao tunawachekea na kujinafikisha kwao.

  • Hatujui kwa nn mama amekuwa na msukumo wa Ujasiri kiasi hichoo hatujui hakupata nafasi ya kueleza mengi katika habari, tunampongeza kwa Ujasiri wake ila wito wangu ni kumtafuta na kueleza chanzo cha ujasiri tuliouona kwake natumaini akipata nafasi ya kujieleza atawajaza wanawake wengi zaidi ujasiri na zaidi tutafika haraka sana ile safari yetu ya Mabadiliko.

    Ongera Bi. Mwajuma Shabani!

  • Mimi ni rais mtarjiwa wa nchi hii mama kama huyo katika utawala wangu lazima nimfuge ikulu anipe mbinu za kupambana na mafisadi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *