Shamba darasa, teknolojia mpya kuwahakikishia wakulima usalama wa chakula

Jamii Africa

Wakazi katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania wamekuwa wakitegemea kilimo cha mazao ya chakula kama chanzo cha kipato na kuendesha familia zao. 

Licha ya juhudi za wakulima kuwekeza nguvu zao kwenye uzalishaji wa mazao, bado baadhi yao hawajafaidika kutokana na changamoto za uhaba wa teknolojia na kukosekana kwa soko la uhakika.

Kwa kutambua hilo serikali za Afrika kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa, wameendelea  kutekeleza miradi inayolenga kuongeza uzalishaji wa mazao kwa kusogeza karibu teknolojia kwa wakulima.

Juhudi hizo zinahusisha uagizaji na matumizi ya teknolojia mpya ikiwemo mbolea, mbegu zenye ubora; kutoa huduma za ushauri na mafunzo kupitia shamba darasa na kuongeza maeneo ya kilimo.

Teknolojia mpya imetumika kwa sehemu tu kwasababu wakulima wengi bado hawajafikiwa na wataalamu wa kilimo ambao wanawajibika kutoa mafunzo ya kiufundi kwa wakulima waliopo vijijini. 

Katika maeneo ambayo wakulima wadogo wamewezeshwa kiteknolojia na kupata mafunzo kwa vitendo uzalishaji na tija vimeongezeka.

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya ScienceDirect mwaka 2014 juu ya Usalama wa chakula na Umaskini kwa wakulima, ulibaini kuwa wakulima wakipata mafunzo kwenye mashamba darasa wanauwezekano mkubwa wa kufaidika kiuchumi kuliko wakisimamiwa kwenye vijiji vyao. 

Katika utafiti huo uliobeba jina la RIPAT (Rural Initiatives for Participatory Agricultural Transformation) ulihusisha wakulima 2,041 kutoka katika vijiji 36 vya Wilaya za Karatu na Arumeru ambao waliingia katika mradi wa majaribio wa  mwaka 1 ili kupata mafunzo ya vitendo na teknolojia mpya kwenye shamba darasa. 

Baada ya kumaliza mradi huo wa majaribio matokeo yalionyesha kuwa zaidi ya  nusu ya wakulima walipata stadi muhimu za kilimo cha kisasa.

Mtafiti aliyehusika na mradi huo, Anna Larsen anaeleza katika ripoti yake kuwa wakulima hao waliporudi katika maeneo yao walipata matokeo tofauti ikilinganishwa na wale waliopata mafunzo  vijijini kutoka kwa wataalamu wa kilimo.

Anaeleza kuwa wakulima hao waliweza kutumia teknolojia mpya kwa ufasahaa ambapo uzalishaji uliongezeka na kubadili maisha yao kiuchumi.

Pia walihakikishiwa usalama wa chakula katika familia zao ambapo ubora wa chakula uliongezeka;watoto walipata virutubisho muhimu kwa afya zao. 

Watafiti hao wanaeleza kuwa katika kufuatilia matokeo ya uchunguzi wao kwa wakulima waliopata mafunzo ya majaribio ya teknolojia mpya walibaini kuwa njaa katika kaya za wakulima hao imepungua kwa asilimia 24. Familia zilikuwa na uwezo wa kupata Milo mitatu kwa siku na ikilinganishwa na famili ambazo hazikushiriki mafunzo.

Ripoti ya utafiti huo inapendekeza wakulima waliopata teknolojia mpya  wawaelimishe wakulima wengine ili kuongeza mazao ya chakula katika ngazi ya familia.

Kutokana na umuhimu wa teknolojia, serikali na wakulima wanashauriwa kuunda na kuongeza mashamba darasa yenye vifaa muhimu vya mafunzo. Pia huduma hiyo isogezwe karibu na wakulima ili ushiriki wao use katika kiwango cha kuridhisha.

Hata hivyo, matumizi ya teknolojia katika kilimo yaende sambamba na kupatWakazi katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania wamekuwa wakitegemea kilimo cha mazao ya chakula kama chanzo cha kipato na kuendesha familia zao.

Hata hivyo, matumizi ya teknolojia katika kilimo yaende sambamba na kupatikana kwa soko la uhakika la mazao ili wakulima wadogo wafaidike kiuchumi.ikana kwa soko la uhakika la mazao ili wakulima wadogo wafaidike kiuchumi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *