JUMLA ya wanafunzi 630, sawa na robo tatu ya wananafunzi 832 wanaosoma katika shule ya msingi Pamba B Jijini hapa wanaketi sakafuni kutokana na upungufu mkubwa wa madawati unaoikabili shule hiyo.
Taarifa hiyo ilitolewa 0ktoba 10 mwaka huu na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Sophia Iboni wakati akipokea msaada wa madawati 40 yaliyotolewa na Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma (PPF).
“…Kwa kweli tunaushukuru uongozi wa PPF kwa msaada huu wa madawati 40; ingawa kweli bado tunaupungufu mkubwa kwa sababu tunayo madawati 102 tu!” alisema mwalimu Iboni.
Kwa mujibu wa mwalimu Iboni, zaidi ya wanafunzi 630 wanaketi sakafuni shuleni hapo.Mwalimu Iboni alifafanua kwamba shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa madawati 127.
Alisema pia kwamba shule hiyo inakabiliwa na uhaba mkubwa wa walimu wa kike. Aliendeea kufafanua kwamba shule hiyo ina jumla ya walimu 17, wote wa kike.
“ Ombi letu kwa wadau na taasisi zingine ni kwamba bado tunahitaji msaada zaidi a madawati” alisema Mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo, Mashaka Baltazar wakati akimkaribisha Meneja wa PPF kanda ya ziwa.
Baltazar aliyataja matatizo mengine yanayoikabili shule hiyo kwamba ni upungufu wa matundu ya choo. Mwenyekiti huyo alisema shule hiyo ina matundu manne tu ya choo; matundu ambayo uwiano wake hauendani na wingi wa wanafunzi.
“ Tumesikia maombi yenu, na kikubwa ni kwamba bado shule hii inahitaji madawati zaidi. Hata hivyo, nitalipelekeka ombi hili katika Menejimenti ya Mfuko” alisema Meneja wa PPF kanda ya ziwa, Meshach Bandawe na kuongeza kuwa amekabidhi msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mfuko huo.
Alisema ni sera ya PPF kutoa misaada katika jamii; lengo likiwa ni kusaidiana na serikali kuu. Bandawe alisema madawati yaliyotolewa yana thamani ya shilingi milioni 2.1.
Habari hii imeandikwa na Juma Ng’oko, Mwanza
Hapo ndiyo utaona serikali ya kiwewe imeshindwa kuwa na maono kwa maendeleo ya taifa inaenda kwa upepo,Tz si nchi ya kufanya Ukuajia kiuchumi(Economic Growth)kwani ni hatari kwa taifa la kesho mfano,wanafunzi 300 wanaokaa chini au 300 walio kosa mlo wa mchana shule wakakimbia vipindi,au waliochoka kutembea kilomita 18 kwenda shule wakafeli darasa la saba,halafu wazazi wao hawana pesa ya kuwa endeleza na sekondari,inabidi waishie kwenye ajira mbaya za umalaya,uuzaji mifuko,uuzaji baa na migahawa,migodini n.k halafu wanaishia kufariki,kupata magonjwa hatari,kubakwa n.k kisa ni serikali imeshindwa fanya elimu ya sekondari bure na pili hakuna mipango ya kuwapeleka waliofeli ktk vyuo vya ufundi wasome bure,hapo kuwapotezea ramani ya masha watoto wasio na hatia ni uhaini serikali inastahili kufunguliwa mashitaka makubwa tu.
Nachotaka kusema kwanini tusi thibiti idadi ya watu kwa sera nzuri?halafu tufanye Maendeleo kiuchumi yani ECONOMIC DEVELOPMENT ambapo ni kuongezeka kwa kiasi na ubora wa huduma za kijamii,Mfano kuloko kujisifia umejenga shule za kata 4000 zisizo na walimu wakutosha,madawati,maabara n.k jenga shule 2000 zenye walimu wa kutosha,madawati na maabara n.k.
Serikali yetu inafanya vitu kuridhisha wahisani ambao pia ndiyo waporaji rasirimali zetu pitia ukoloni mamboleo,haiwezekani mkoa una dhahabu au Tanzanite au Misitu ya mbao n.k halafu hapohapo wanafunzi wanakaachini huku mbao zinavunwa na kuuzwa nje kama Iringa ilivyo,ni aibu serikali kuwa kichwa cha mwendawazimu.Ila mimi naamini malipo yao wahuni ni moto wa milele tu.