POLISI wadaiwa kumuua mfanyabiashara wa Dhahabu,wapora mamilioni ya shilingi

David Azaria

HALMASHAURI ya serikali ya kijiji cha Kanembwa Runzewe wilaya ya Bukombe mkoani Geita,imelituhumu jeshi la polisi wilayani humo kujihusisha na rushwa na ujambazi kutokana na askari wake wa kituo cha Runzewe kudaiwa kuhusika na mauaji ya mfanyabiashara wa dhahabu Yemuga Fugungu(48).

Mfanyabiashara huyo mkazi wa kitongoji cha Masota anadaiwa kuuawa na polisi hivi karibuni baada ya kumvamia nyumbani kwake na kulipua nyumba yake kwa mabomu na risasi baada ya kumtuhumu kumjeruhi askari mwenzao kwa risasi na kisha kuondoka na mamilioni ya fedha.

Pia askari wawili kati ya 20 waliovamia nyumbani kwa mfanyabiashara huyo wanadaiwa kumfanyia kitendo cha udhalilishaji mke wa marehemu Lucia Kilaza(23)baada ya kumpekua kwa nguvu hadi kwenye sehemu zake za siri na kumvua nguo za ndani kisha kuzichana na kuondoka na sh.1.2 milioni.

Kilaza alikuwa ameficha fedha hizo baada ya askari hao kufika kwenye familia hiyo kisha kuanza kufyatua risasi hewani na kusababisha kifo cha mumewe kilichotokea alhamisi iliyopita.

Awali kamanda wa polisi mkoa wa Geita,Bw.Leonard Paul alisema mfanyabishara huyo alijiua mwenyewe baada ya kumjeruhi askari wa Runzewe Fortunatus Beatus kwa bastola kutokana na askari wa kituo hicho walipokamata gari lake lililokuwa na kokoto zinazodaiwa kuwa ni za wizi.

Madai ya kamanda huyo yamepingwa na ndugu wa marehemu pamoja na viongozi wa serikali ya kijiji hicho ambao wamedai serikali isiwafumbie macho askari hao waliotumia nguvu kupita kiasi na kusababisha kifo na uporaji wa zaidi ya sh.370 milion.

Kauli ya serikali ya kijiji hicho inakuja kufuatia askari hao kwenda kijijini hapo bila kutoa taarifa kwa viongozi wa eneo hilo kitendo ambacho kinadaiwa ni kinyume cha taratibu na sheria,na kimetafasiliwa kuwa ni kujenga mahusiano mabaya kati ya polisi na raia.

Viongozi wa halmashauri hiyo wamesema kitendo cha askari kuingia kijijini hapo bila kutoa taarifa kwa viongozi hao kisha kufanya uharifu, kusababisha kifo na upotevu wa mali hawatofautiani na majambazi.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Masota,Bw.Evarist Mandwa,akizungumzia tukio hilo alisema taarifa za tukio hilo alizipata siku iliyofuata ingawa usiku alisikia milio ya bunduki iliyowashitua wananchi na kushindwa kujitokeza kukabiliana na hali hiyo.

"Hatukuwa na taarifa kama askari wanakuja eneo hili,ndipo kesho yake tulisikia askari wameua na wamepora fedha za marehemu.Hapa kijijini hatuna historia ya marehemu kujihusisha na uhalifu"

Alisema sheria ya serikali inasema kunapokuwa na uharifu eneo husika askari wanapaswa kuonana na uongozi wa mtaa kwa taarifa,kitendo hicho kina hatarisha mahausiano kuwa mabaya kati ya raia na askari.

Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho,Bw.Peter Kuhanda alisema,halmashauri ya kijiji itakutana na kamati ya ulinzi na usalama ya kijiji ili kuandika maelezo kwenda serikali ya mkoa kuitaka iingilie kati kuchunguza nguvu iliyotumiwa na askari hao.

Bw.Kuhanda Alisema tukio hilo limegubikwa na mianya ya rushwa na hivyo kuitaka serikali kuingilia kati suala hilo kwa kuunda tume kuchunguza undani wake ili kuepusha uvunjifu wa amani unaweza kujitokeza kutokana na jazba za wananchi.

Naye diwani wa kata ya Runzewe,Bw.Yusuph Fungameza,alisema serikali isimame kubaini kama nguvu iliyotumika ni halali sambamba na kutoa taarifa sahihi kuhusiana na uchunguzi tukio hilo.

Alisema kwa hali hiyo wananchi watakosa imani na jeshi la polisi ambalo limekuwa likihasisha ulinzi shirikishi jamii kutokana na askari badala ya kulinda haki za raia na mali zake wamegeuka na kuwa wauaji na waporaji wa mali za raia.

"Sikubaliani na kauli ya kamanda wa mkoa wa Geita,kwamba marehemu alimjeruhi askari na kujiua.Kama marehemu alimjeruhi askari kituoni kwa bastola.kwa nini walimruhusi kutoka pale kituoni..tena kwa kutembea,kisha usiku wakamfuata nyumbani kwake,polisi wamehusika moja kwa moja niko tayari kutoa ushahidi"alisema Diwani huyo.

Kutokana na kuwepo kwa hisia tofauti kwa wakazi wa Runzewe kuhusiana na tukio hilo,diwani Fungameza amewataka wananchi wa kata hiyo watulie wakati uchunguzi unaoendelea kabla ya kwenda kudai taarifa ya uchunguzi wa tukio hilo.

Katika hatua nyingine serikali ya mkoa wa Geita,inatuhumiwa na ndugu wa marehemu kukalia ripoti ya uchunguzi wa jopo la madaktari walioufanyia uchunguzi mwili wa marehemu jumatatu iliyopita.

Mkuu wa mkoa wa Geita,Bw.Said Magalula,ndiyo alipaswa kuitoa ripoti hiyo lakini amekuwa kimya licha ya baadhi ya madaktari walioufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kudai kwamba taarifa hiyo kuwa tayari.

Jumamosi iliyopita ndugu wa marehemu walisusia kuzika mwili wa ndugu yao kwa lengo la kushinikiza majibu ya taarifa ya Bukombe pamoja na kupisha uchunguzi wa mara ya Pili uliofanyika katika hospitali ya wilaya ya Geikta chini ya jopo la madaktari sita kutoka Geita, Bukombe, Mwanza na Dar es Salaam.

2 Comments
  • Ukweli Seriukali ya Tanzania kama isipokuwa makini tunakoelekea siko maana leo hii unyanyasaji ,wizi na ukatili unafanywa na watu walioshika madaraka na nafasi za kusaidia wananchi sasa wananchi waende wapi walie na nani?

    Baba wa nyumba kama hawezi kuona udhalili huu na tishio la kuvunjika kwa amani lililoko mbele siku zinazokuja hata hizo tme zinazoundwa kwa maslahi tu ya watu hazitokuwa na maana kwa WatanzaniaLeo hii watu wanaripoti uharifu Serikali inakaa kimya siku yakiwa yametokea eti tuunde tume tume ya nini wakati mmesaaisha ninyi?harafu ninyi hao hao ndo wajume wa tume?

    jueni hakuna goti na mguu wote unaitwa mguu sasa kwa Mabaya yanayotupata Watanzania Serikali na watu wenye vyeo ili mradi hayawagusi mmeyakaria kimya ipo siku mtaulizwa na Mungu maana mauaji ya Kimbali ya Rwanda ni chuki kama hizo mnazozilimikiza sasa Suirieni wote mlio kwenye sisteem yatakapotokea Mungu atusaidie/

  • Kwa ufafanuzi wa tatizo tulilo sisi ni wapangaji wa jengo la CCM Mkoani Kigoma Ambalo ni uwanja wa mpira Lake Tanganyika.

    Tulikuwa na msimamizi wa uwanja kwa muda mwingi hakukutotekea tatizo ila kuazia mwezi wa tisa 2013 ndipo kumeanza kutokea taswira tofauti.

    Kamati ya siasa ya mkoa kilimtoa kimya kimya meneja wa uwanja huu Ndugu Adallah Kashushu na Msaidizi wake Ndugu Saick .Kitu cha ajabu kilichotokea meneja huyo aliyeteuliwa bwana Shabani Muhoza Buti na msaidizi wake Bw.Athumani Ninja.

    Kilichofata meneja huyo na msaidizi wake walianza kutemea chuma kwa chuma kujitamulisha.Baada ya kujitabulisha siku mili mbele walileta kwa wapangaji wote barua yenye kichwa cha habari kuwa ni Mpango mpya wa upangishaji,Viwango vikuwa vya ajabu na barua ikitutaka tulipe kodi hizo mpya kuanzia 01oct 2013 toka kwa barua yake meneja huyo ya 21/09/2013.

    Tuligomea kodi hiyo kwa kumwita na kumweleza kwa nini tunaikataa kodi hiyo iliyoongezwa kwa zaidi ya asilimia 300 na pengine 700 wakati jengo lina mapungufu mengiUwanja ambalo ndo jengo halina vyoo,vyuma vinavuja,milango mibovu na kitu kingine wanaoongeza kodi au kufanya maadiliko yoyote huwa ni wamiliki wa jengo amba ni Bodi ya wadhamini wa chama cha mapinduzi ndio wanaomiliki mali zote za chama na ni mfumo wa tasisi zote kubwa zenye mali. Lakini hakutuelewa alichoamua ni9 kutushitaki Baraza la Ardhi na Nyumba la kata lilipo jengo.

    Kilichofanywa na Baraza hilo wapangaji tulihukumiwa ila kujitetea au kusikiliza maelezo yetu ya msingi kwenye ugomaji wa kulipa kodi hizo zilizoongezwa na meneja kwamba tulipe tu ama tuhameTulikata rufaa katika Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ya Kigoma na tarehe Sita Mei 2014 hukumu ilitoka iliyofutilia mbali hukumu ya baraza la kata ya Buzebazeba na kutoa maelekezo kwa meneja huyo kwamba yeye hana mamlaka ya kuongeza kodi, kushitaki wapangaji au kuwafukuza bali wamiliki wa jengo ndo wenye mamlaka hayo.

    Kilichofata baada ya hukumu hiyo kesho yake tu tulipokea barua ya Notisi toka kwa kampuni ya Madalali ikitutaka tulipe kodi mpya iliyotangazwa na Meneja ikiwa na ongezeko la gharama za kuwalipa madalali asilimia 10 na usafiri wa madalali elfu therathini na tano kwa kila mpangaji.sivyo tutatolewa kwa nguvu na kulipa kwa nguvu pia.

    Kwa kuwa hukumu nakala tulikuwanayo tulipuuza siku 14 tulizopewa, baada ya siku hizo tulipewa notisi nyingine ya siklu 7 nayo hatukuijali. Kilichofuata kiaya ndo hicho cha tarehe saba mwezi wa sita Madalali hao na Meneja hao wakiwa na Wanamgamo wapatao 30 hadi 40 walikuja na kuingia majumbani mwetu na kuchukua vitu vyote na sisi bila kuwapo hali tunayoitaja kuwa tuliibiwa maana hakuna kibali wala sheria yoyote iliyowaruhusu kufanya hivyo.

    Watanzania wenzetu hasa ninyi wanasheria hapo tufanyeje? Maana tumepewa vitu vyetu baadhi kwa amri ya mahakama(Baraza la Ardhi na Nyumba WilayaKigoma)Hata hivyo kwa kiuri walichonacho wamerejesha vitu na kufungua vyumba vyetu tulivyokuwa tunakaa kwa amri tatu za Mahakama hiyo(Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya Kigoma)Na aliweza kusema kwa muda uliopita siku 32 tukiwa tunaishi kwa kusaidiwa na jamii tu na kulala ovyto nsisina watoto wetu kuna vyuma amavyo wengine hawakupata eti vimeshapangishwa,lakini pia vitu vingine kama Pesa,nguo na vifaa (vyomo vya nyumbani na vitendea kazi vimepotea)(Vimeibiwa na waliotekeleza oparation hiyo ya kiuharifu kwetu)Tunaomba wananchi na serikali na wanasheria mtoe msaada wenu wa mawazo nini tufanye ili kujiona na sisis ni watu katika jamii ndani ya Nchi yetu?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *