Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai, DCI, Robert Manumba, ameondoka jioni hii kuelekea Afrika Kusini, kwa matibabu zaidi baada ya hali yake kuwa nafuu kidogo.
Habari za uhakika zilizoifikia FikraPevu zimeeleza kwamba Manumba ameondoka kwa ndege maalum ya kampuni ya AAR kwenda Afrika Kusini akitokea hospitali ya Agakhan ya jijini Dar alikokuwa amelazwa baada ya kupelekwa Uwanja wa Ndege kwa gari la kubebea wagonjwa (ambulance) maalumu.
"Hali yake imetia matumaini sasa japo bado hajitambui, na Mungu akimsaidia kufika salama, tutakuwa tumeokoa maisha yake," anasema mtoa habari wetu.
DCI Manumba alilazwa katika Hospitali ya Agakhan ya jijini Dar es Salaam kwa ambapo hali yake imekua ikiriporiwa kuwa mbaya.
Taarifa iliyothibitishwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso ilisema kuwa Manumba alilazwa hospitalini hapo baada ya kuhamishwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Taarifa za ndani ya jeshi hilo zilisema pamoja na matatizo mengine aliyonayo, amekuwa akisumbuliwa na malaria.
==============
UPDATE 1:
FikraPevu imeweza kufuatilia na kubaini kuwa DCI Manumba amelazwa hospitali inaitwa Hill Park, Johannesburg, Afrika Kusini
Atapona
Mungu amsaidie apone haraka
eee mungu leo ni siku nyingine naombea wagonjwa mahodini tanzani hata na nchi nyingine uwatakase na kuwaponya AMEEN,atap
Wangenunua vifaa hivyo vilikuwa vinatakiwa asingepata usumbufu na serikali kuingia garama kubwa kutibiwa Africa Kusini, Natumai watajua mgomo wa madaktari ulikuwa unamaanisha nini.
Mungu amsaidia na kumponya arudi salama
God bless him
yaani nchi hiii bwana very funny!!!!ugonjwa uliotajwa ni malaria, ugonjwa huu ni maarufu zaidi hapa tz kliko ulivyo huko south africa!!!na je ni lini watanunua vifaa na kuheshimu hospitali zetu ili wao wenyewe kina manumba watibiwe hpahapa????tena bwana dci toka day oned kalazwa aga khan wala sio muhimbili!!!!