Hali ya Manumba bado tete! Sasa akimbizwa Afrika Kusini…

Islam Mbaraka

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai, DCI, Robert Manumba, ameondoka jioni hii kuelekea Afrika Kusini, kwa matibabu zaidi baada ya hali yake kuwa nafuu kidogo.

Habari za uhakika zilizoifikia FikraPevu zimeeleza kwamba Manumba ameondoka kwa ndege maalum ya kampuni ya AAR kwenda Afrika Kusini akitokea hospitali ya Agakhan ya jijini Dar alikokuwa amelazwa baada ya kupelekwa Uwanja wa Ndege kwa gari la kubebea wagonjwa (ambulance) maalumu.

"Hali yake imetia matumaini sasa japo bado hajitambui, na Mungu akimsaidia kufika salama, tutakuwa tumeokoa maisha yake," anasema mtoa habari wetu.

DCI Manumba alilazwa katika Hospitali ya Agakhan ya jijini Dar es Salaam kwa ambapo hali yake imekua ikiriporiwa kuwa mbaya.

Taarifa iliyothibitishwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso ilisema kuwa Manumba alilazwa hospitalini hapo baada ya kuhamishwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Taarifa za ndani ya jeshi hilo zilisema pamoja na matatizo mengine aliyonayo, amekuwa akisumbuliwa na malaria.

==============

UPDATE 1:

FikraPevu imeweza kufuatilia na kubaini kuwa DCI Manumba amelazwa hospitali inaitwa Hill Park, Johannesburg, Afrika Kusini

6 Comments
  • eee mungu leo ni siku nyingine naombea wagonjwa mahodini tanzani hata na nchi nyingine uwatakase na kuwaponya AMEEN,atap

  • Wangenunua vifaa hivyo vilikuwa vinatakiwa asingepata usumbufu na serikali kuingia garama kubwa kutibiwa Africa Kusini, Natumai watajua mgomo wa madaktari ulikuwa unamaanisha nini.

    Mungu amsaidia na kumponya arudi salama

  • yaani  nchi  hiii bwana  very  funny!!!!ugonjwa  uliotajwa  ni  malaria, ugonjwa  huu  ni  maarufu  zaidi  hapa  tz  kliko  ulivyo  huko  south  africa!!!na  je  ni  lini  watanunua  vifaa  na  kuheshimu  hospitali  zetu  ili  wao  wenyewe  kina  manumba  watibiwe  hpahapa????tena  bwana  dci  toka  day  oned  kalazwa  aga  khan  wala  sio  muhimbili!!!!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *