Mlipuko Arusha: Idadi ya Watuhumiwa yafikia 12

Olympia Martin

IDADI ya watuhumiwa wa tukio la kulipua kanisa la mtakatifu Joseph Mfanyakazi kwa bomu, Mkoani Arusha, imezidi kuongezeka toka tisa hadi kufikia 12, kati yao majina tisa yametajwa na matatu bado ni siri kwa ajili ya uchunguzi, yumo mwendesha bodaboda.

Aidha jeshi la Polisi nchini kupitia Kamishana Mkuu wa jeshi hilo,(IGP) Saidi Mwema, wametangaza donge nono la shilingi milioni 50 kwa mtu yoyote atakayefanikisha kufichua mtandao wa kigaidi nchini.

Kauri hiyo imetolewa na Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Arusha, Liberatus Sabasi, wakati alipokuwa akitoa taarifa juu ya hatua walizochukua tangu kutokea kwa mlipuko wa bomu hilo Mei 5 mwaka huu,majira ya saa 4.30,ambapo watu watatu walifariki dunia na 66 walijeruhiwa.

Alisema kuwa siku ya tukio kulikuwa na uzinduzi wa kanisa hilo na mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Vatican nchini Tanzania, Askofu Mkuu Francisco Padilla na alipokuwa akibariki maji na kujiandaa kukata utepe kama ishara ya uzinduzi, ghafla mtu mmoja aliyejificha kwenye choo cha jirani, upande wa kaskazini mwa kanisa hilo, alirusha bomu hilo.

Kamanda Sabas alisema kitu hicho kilirushwa umbali wa mita 20 na kilikuwa na ukubwa wa ngumi ya mtu mzima, kuelekea kwenye mkusanyiko wa wauminina kilipotua chini ulitokea mlipuko mithiri ya bomu na kusababisha watu 66 kujeruhiwa ambao kati yao watatu walipoteza maisha.

Kamanda Sabasi aliwataja majina ya watuhumiwa tisa kuwa ni Victor Ambrose Kalisti (20) mkazi wa kwa Mrombo Arusha na mwendesha boda boda, Joseph Yusuph Lomayani (18) mwendesha boda boda na mkazi wa kwa Mrombo Arusha.

Wengine ni George Bathoromeo Silayo (23) mfanyabishara na mkazi wa Olasiti, Mohamed Sulemani Said (38) mkazi wa Ilala   Dar Es Salaam na huyu ndiyo mwenyeji wao aliyewafuata kwa gari binafsi uwanja wa ndege Dar Es Salaam na kuwachukua hadi Arusha Hoteli ya Aquline.

Wengine wametajwa kuwa ni Said Abdallah Said (28, ambaye raia wa falme za kiarabu, eneo la Abudhabi, Abdulaziz Mubarak (30) mkazi wa falmae za kiarabu, eneo la Saudi Arabia, Jassini Mbarak (29) mkazi wa Bondeni Arusha, Foud Saleem Ahmed (28) raia wa falme za kiarabu na Said Mohsen, mkazi wa Najran falme za kiarabu.

Alisema kuwa watuhumiwa hao bado wanaendelea na mahojiano na tayari jalada la mashtaka yao limepelekwa kwa mwanasheria Mkuu wa serikali, kwa ajili ya maamuzi ya kisheria.

Kamanda Sabas alisema katika mahojiano na waandishi wa habari, alisema kuwa katika hatua za awali zinaonyesha bomu hilo siyo la kienyeji na pia wageni hao walikuw ana VISA halali ya kukaa nchini, kwa madai walikuja harusini.

Alisema Watuhumiwa hao kutoka falme za kiarabu  baada ya kuwahoji walidai wamekuja harusini.

Aidha alisema ulinzi umeimarishwa katika kanisa lilikotokea mlipuko la mtakatifu Jospeh Mfanyakazi, Olasiti, ili kuhakikisha hakitokei kitu chochote kabla na baada ya mazishi hayo

3 Comments
  • suala la mripuko arusha lifanyiwe kazi haraka ili kuzuia uharibifu wa mali na maisha ya watu. poleni wahanga wote wa mlipuko na mungu awape ujasiri na nguvu ktk kipindi hki kigum

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *