Mbunge apigwa mawe na wananchi akiwa mkutanoni

Jamii Africa

MBUNGE wa Muleba Kasikazini (CCM) Charles Mwijage juzi alijikuta katika wakati mgumu baada ya kupigwa mawe na wananchi katika mkutano wa hadhara akidaiwa kuikimbia ofisi na kupindisha maamuzi ya vikao.

Hali hiyo ilitokea katika eneo la Izigo ambapo aliposimama kuhutubia wananchi walioonekana kuwa na jazba walianza kutawanyika huku mawe yakivurumishwa kuelekea jukwaani.

Miongoni mwa malalamiko ya wananchi ni kuisusia ofisi iliyoachwa na Ruth Msafiri na kukosa sehemu ya kupeleka kero zao,na kudaiwa kupinga eneo hilo kuwa makao makuu ya Wilaya ya Kamachumu ambayo mapendekezo yako katika hatua mbalimbali.

Katika hali iliyoonekana kuwepo kwa mgawanyiko ndani ya chama kabla ya kurushwa mawe wenyeviti wa vijiji ambao wanatokana na chama hicho waliwaongoza wananchi kumsusia mbunge wao.

Wenyeviti hao walidai wao ndiyo walitumika kuwashawishi wananchi ili apate kura na kuwa hivi sasa wanashangaa kwa kuonekana kuanza kuwasaliti kwa kile alichodai kuwa hata bado hakujapambazuka.

“Tunataka uitambue na kuitumia ofisi ya mbunge iliyojengwa hapa Izigo, tunataka uendeleze maamuzi mema ya watangulizi wako lakini tumeanza kupoteza imani hata kabla hakujapambazuka”alisema George Merkiory Mwenyekiti wa kijiji cha Itoju kabla mkutano huo haujavurugika.

Pia Mwenyekiti huyo alimweleza Mwijage kuwa wananchi walianza kumtilia shaka pale alipodaiwa kutamka kuwa ofisi ya mbunge wa zamani itumike kwa matumizi mengine na yeye hayuko tayari kuitumia.

Fikrapevu ilipomtafuta mbunge huyo kwa njia ya simu ili kujua kama amepeleka malalamiko polisi baada ya kupigwa mawe mkutanoni simu yake iliita mara kadhaa bila kupokelewa.

4 Comments
  • Huyu jamaa huwa si mtu mzuri wananchi walimchagua kwa kurubuniwa na ccm. Hata ndugu zake aliwasambaratisha. Hawa ndugu nu watoto wa baba mkubwa wake amabao ilitokea kuwatambua akiwa na miaka ya ujana. Huyu siasa zake ni za kitapeli.Hawakumtambua mapema. Huyu huwa mfitini na mwenye kujigamba sana.

  • ndio siasa za bonqo jaman …sema inabidi wananchi tuwe makini sana tukitaka kuamua jambo.,hasa kama jambo lenyewe ni la kimaendeleo….lol

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *