Mbowe aachia shangingi la serikali; kupinga matumizi mabaya ya fedha

Jamii Africa

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ambaye pia ndiye kiongozi wa Kambi ya Upinzania Bungeni Bw. Freeman Mbowe ametangaza
kurudisha shangingi alilopewa na serikali kama kiongozi wa upinzani. Bw. Mbowe (HAI) amechukua msimamo huo kama ishara ya kuonesha mfano wa kutekeleza wito wa kubana matumizi.

Katika taarifa iliyotolewa na Bw. Mbowe jioni ya leo uamuzi huo umechukuliwa pamoja na maamuzi mengine kuonesha kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo hakihubiri tu bali pia kiko tayari kutekeleza ujumbe wake wa kubana matumizi. Taarifa ya CHADEMA iliyotolewa Bungeni imelalamikia serikali kwa kutokutekeleza baadhi ya mapendekezo ambayo yalitolewa na kambi hiyo hasa baada ya mapendekezo ya bajeti ya 2011/2012 kupitishwa na wabunge wa CCM.

Wabunge wa Chadema waliamua kupiga kura ya Hapana katika hoja ya kupitisha bajeti hiyo huku wakitoa sababu mbalimbali. “Katika kupitisha bajeti hiyo wabunge wa Kambi ya Upinzani na hususani wa CHADEMA tuliamua kupiga kura za HAPANA kwenye mapendekezo hayo ya Serikali” Ikielezea sababu zilizofanya Chadema kupinga bajeti ya serikali taarifa hiyo ilisema miongoni mwa sababu hizo ni:

1. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kuondoa posho za vikao (sitting allowances) kwenye mfumo wa malipo ndani ya serikali.

2. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kuhakikisha kuwa magari yote aina ya “Mashangingi” yanayotumiwa na viongozi na watumishi wa umma yauzwe kwa mnada ndani ya miezi sita na viongozi hao wakopeshwe magari kwa ajili ya kufanya majukumu yao mbalimbali.

3. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kufuta/kupunguza misamaha mikubwa ya kodi ambayo Makampuni ya Madini yanapata ili kuhakikisha kuwa serikali inapata mapato kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.

4. Serikali imekataa kuingiza pensheni kwa ajili ya wazee wote nchini ya shilingi 20,000 kila mwezi ili kuweza kuwapunguzia ukali wa maisha wazee wetu .

5. Serikali imekataa Kufuta/kuondoa misamaha ya kodi kwa kipindi cha miaka 10 kwenye maeneo maalum ya uwekezaji (EPZ).

Pamoja na na sababu hizo kambi hiyo ya upinzani iliamua kukataa bajeti hiyo baada ya serikali kutokubali kubadilisha mfumo wa usafiri ambao ulipendekezwa na Chadema ambao walipendekeza kuwa ni viongozi wa juu tu wa serikali ambao walipaswa kusafiri katika First Class huku viongozi wa kati wakisafiri kwenye Business Class na wale wengine wote wakiwemo wabunge kusafiri katika Economy Class.

Kutokana na hayo Chadema imesema kuwa “Tumeamua kumwandikia katibu wa Bunge barua ili aweze kutenganisha fomu kwa ajili ya mahudhurio na kwa ajili ya posho na wabunge wa
CHADEMA hawatasaini fomu za posho.” Pamoja na uamuzi huo Chadema ikatangaza kuwa Mwenyekiti wake ambaye ni kiongozi wa Upinzani Bungeni ameamua kurudisha gari lake la kifahari ambalo alilitoa lipigwe mnada.

Hata hivyo kwa vile hilo ni gari la serikali haijulikani kama serikali italipiga mnada au italihamisha kwenda kwa mtendaji mwingine wa serikali. Uamuzi wa Mbowe kurejesha gari hilo umepokelewa na baadhi ya watu kama ni wa kishujaa na wa mfano na unazidi kuiweka serikali katika mwanga mbaya.

Endapo uamuzi huo wa Mbowe hautaungwa mkono na serikali na baadhi ya viongozi wengine unaweza usiwe na mafanikio yoyote huku ukimfanya aonekane kama mtu aliyekuwa anatafuta umaarufu wa chee kama baadhi ya watu walivyotolea maoni baada ya taarifa hizo kuzuka hasa kwenye mtandao dada wa tovuti wa JamiiForums.Com

Mwandishi Wetu

5 Comments
  • This is what is required for a serious political party like CHADEMA. Mbowe has set an example to be emulated by all peoples of good will to Tanzania.
    It is the duty of the current government of CCM to emulate this and practice frugality on the part of government spending. Keep it up CHADEMA, the peoples power will eventually prevail.

  • Watanzania ni wakati wa kuwa nyuma ya viongozi watekelezaji. Tumuunge mkono Mbowe, Yeye ni maarufu wala hana sababu ya kutafuta kitu alichonacho, anachofanya ni kuonyesha njia ya kweli itakayo saidia kupuguza gharama zinazo epukika. Big up, aluta continue.

  • We need people who are ready to loose for the betterment of all Tanzanians however small or big! Why others not imitate regardless of political stand. Brethrends, commitment is important and seriousness of everything however trivials they are, imagine power issue, road traffic jum and endless others one can mention! Whop!

  • SASA KUJUA KWAMBA HAO NI MAAMUZI YA KISHUJAA.
    AKIRUDISHA SHANGINGI PINDA NAACHA POMBE NA KUTUMIA INTERNET ITAKUWA MWISHO.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *