Watanzania 108 warudishwa toka Afrika Kusini

Jamii Africa

Watanzania 108 wamerudishwa Nchini wakitokea Afrika Kusini baada ya kukamatwa huko wakiishi kinyume cha sheria.

Habari zilizothibitishwa na maofisa Uhamiaji wa Tanzania, zimeeleza kwamba Watanzania hao wamewasili leo na hadi usiku huu walikua wanakaguliwa kuthibitisha uraia wao.

“Wamekamatwa kwa kukaa bila kibali na wengine walikua na vibali lakini vimeisha muda na wakaendelea kufanya biashara. Mara nyingi wakiwa na pasport wanaacha kuomba muda wa kuongeza vibali vyao,” anasema mmoja wa Maofisa wa Uhamiaji Dar es Salaam.

Hata hivyo, Watanzania hao hawatashitakiwa na badala yake wataachiwa baada ya kuthibitishwa kuwa ni raia halali, pamoja na kupewa onyo.

Kwa mujibu wa Ofisa huyo gharama za kuwaleta nchini zitafidiwa na serikali ya Tanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *