WAKILI maarufu Medium Mwalle anayetuhumiwa za kukutwa na kiasi kikubwa cha fedha kwenye akaunti zake na kisha kupandishwa kizimbani amelazwa kwenye Hospital ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru akidaiwa kuumwa.
Mwalle alirejeshwa tena mahakamani jana, lakini Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Arusha Charles Magessa hakuweza kusikiliza shauri hilo na badala yake aliamuru mtuhumiwa huyo akapatiwe kwanza matibabu.
Akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi wa upelelezi na maofisa Usalama wa taifa, wanaotumia gari dogo maalumu walimpeleka Hospital ya Mount Meru majira ya mchana kwa ajili ya kuonana na daktari.
Mwandishi wa habari hizi aliyekuwapo hospitalini hapo alishuhudia Wakili Mwalle akitolewa kwenye jengo la kuona wagonjwa wa nje na kisha kupakizwa kwenye baiskeli ya wagonjwa waliozidiwa na kuanza kupelekwa wodini.
Mara baada ya kukaa kwenye kibaiskeli hicho Mwalle alionekana kuwa mwenye huzuni, machoni huku machozi yakimtiririka na kuonekana akitikisa kichwa.
Huku akiwa amezungukwa na maofisa wa usalama muda wote aliokuwa akisukumwa kwenye kibaiskel na muuguzi wa kike wa Mount Meru alikuwa ameinamisha kichwa chake huku amekisha kwa mkono wa kushoto.
Muuguzi wa Wodi ya VIP Hospitalini hapo ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake alititisha kulazwa kwa wakili huyo.
“Nikweli huyu mtu amelezwa hapa kwani nimepewa taarifa mapema ya kuandaa chumba kwa ajili yake,” alidai
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Thobias Andengenye alipoulizwa alisema kuwa Mwalle alianza kulalamika kuwa anajisikia kuumwa hivyo aliomba kupelekwa hospitalini.
“Wakati wanaondoka hapa kwenda Mahakamani alikuwa akilalamika kuwa anaumwa kwa hiyo nadhani baada ya kutoka mahakamani watakuwa wameenda hospitalini, kwa sasa sina taarifa kamili,” alisema Kamanda Andengenye.
Mwalle alifikishwa mahakamani jana na kusomewa mashitaka 13 likiwamo la kukutwa na kiasi kikubwa cha fedha ambazo hazikuwa na maelezo sahihi (Money Loundering).
Hata hivyo mashitaka hayo hayakupokelewa na mahakama kutokana na kuwapo kwa makosa ya kisheria ya namna ya kuyafungua, hatua ambayo mahakama iliuamuru upande wa Serikali kuandaa upya hati ya Mashitaka.
Kwa discussion fuatilia hoja hii katika JamiiForums
Ni vizuri haki inapochukua mkondo wake bila kuwaonea haya Mapapa na Manyangumi wa nchi hii. Kwa mambo yanavyobadilika msemo huu utatimia “nchi ya ahadi tutaifikia tu”.
Mwalle pole sana na jua hiyo ni presha na uwogo ndiyo ugonjwa unaweza ukawa unakusumbua kama ilivyo kwa MUBARAKA ila kwanini ulipo kuwa unakula njaa na majasho ya watu ulikuwa huogopi wala kutetemeka leo unajiliza ya nini?
Kutoka labda uhonge mawakili wenzako wenye tabia zako na wapo wengi kwani wasomi wa tz ni wasomi pumba na mapovu, yani hawamna faida kwa masikini hasa wasiowajua, wasomi tumbo wa tz wametokana na mtaala mchafu/kipofu wa elimu tumepata wasomi wezi na waigaji mabaya.
Mwalle pesa ulizo chukua zingeweza jenga zaidi ya shule 1000 na hospitali 60 zenye kila kitu na ubora wa hali ya juu, au kulipia ada watoto zaidi 19000, ambao kwa kukosa ada wanauza baa na wanahatari ya ukimwi, wengine wameajiriwa kwenye ajira mbaya sana achilia watoto wa5 wanao kufa kila siku kwa kukosa huduma za afya bora na kwawakat.