DODOMA: Watu wanne, wakiwemo watatu wa familia moja, wapoteza maisha katika mafuriko Mpwapwa

Daniel Mbega

WATU wanne, wakiwemo watatu wa familia moja, wamepoteza maisha katika mafuriko yaliyotokea wilayani Mpwapwa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo, FikraPevu inaripoti.

Taarifa kutoka eneo la tukio zimeeleza kwamba, maiti zote nne zimepatikana na zimehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya Mpwapwa.

Marehemu wa familia moja wametajwa kuwa ni Martha Mbega (62), na wajukuu zake wawili wa kike Shukuru Donald Chinyanya (16) na Bernadeta Mabula (6).

Wajukuu wengine wawili wa marehemu, Beka Ulanga (11) na Joseph Mabula (8) walinusurika baada ya kufanikiwa kukimbia, ambapo inaelezwa kwamba, Joseph alikutwa akiwa amekwea mti yapata kilometa mbili kutoka eneo la tukio huku mwenzake akikimbilia  kwenye nyumba ya jirani umbali wa meta 800.

Maiti nyingine ya nne haikuweza kutambuliwa mara moja.

Akizungumza kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Mpwapwa (OCD) Mohammmed Rama Mhina, akithibitisha kutokea kwa maafa hayo na kusema bado wanaendelea kupokea taarifa zaidi.

“Kwa sasa tunaweza kusema ni vifo hivi vinne tu pamoja na nyumba ya Mzee Mabula (mume wa marehemu Martha Mbega) ambayo imesombwa, lakini bado hatujasikia zaidi ya hayo,” alisema kamanda Mhina.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *