Ubora: Fukwe za ziwa Nyasa zinaongoza

Albano Midelo

Pichani ni fukwe za kuvutia ambazo zinapatikana katika eneo la Lundo ziwa Nyasa wilayani mpya ya ziwa Nyasa mkoani Ruvuma. Ziwa Nyasa limebarikiwa kuwa na fukwe bora  ulimwenguni, lakini katika hali ya kushangaza fukwe hizo hadi sasa bado hazijatambuliwa na kutangazwa ili kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuziendeleza. Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu ameahidi kuziendeleza fukwe hizo ili kufungua milango ya utalii katika mkoa wa Ruvuma.

Hiki (juu) ni kisiwa cha Lundo ziwa Nyasa ambacho kina utajiri wa vivutio vya utalii wakiwemo wanyamapori, ndege, mimea ya aina mbalimbali na viumbe wengine ambao wanaishi ndani ya kisiwa hicho ambacho kipo  takribani meta 400 kutoka ufukweni. Kisiwa hiki inanadaiwa tayari kimeuzwa kwa mwekezaji.

9 Comments
  • tanzania, tanzania nakupenda kwa moyo wote! tulinde mipaka yetu, tuimarishe mshikamano ulioasisiwa na baba wa Taifa

  • tulinde hifadhi zetu watanzania,kwa nguvu zote.kinachoendelea Lundo kisiwani ni habari kwa huo mkoa kupoteza malihasili na taifa kwa ujumla.hebu watanzania wote tumuunge mkuu wamkoa wa Ruvuma katika kupigani kile ambacho babu zetu wametulithisha.

  • Ama kweli Tanzania ni nchi tajiri ispokuwa sisi wa Tanzania ndo masikini wa fikra kwani tuna vivutio vingi saaaaaaaaaana vya utaliiiiiiiiiii lakini baaadhi yetu huvialibu kwa kuvichoma moto; jamaaaaaani! ebu tubadilikeni

  • Nalikumbuka sana eneo lote la kisiwa cha Lundo,enzi zetu tulikuwa tunaenda kuvua samaki na tunapiga kambi hata wiki mbili kama vile tupo Field.Nilipoenda likizo pale nyumbani (Lundo) nikasikia eti kisiwa amepewa mwekezaji na analipa kijiji Tsh 400,000/= kwa mwaka, nikawauliza viongozi wakawa wanatoa majibu kama wana mapepo (ubabaishaji)mtupu. Lakini hiyo ndiyo Tanzania tusishangae sana!!!!!

  • Kule Lundo na ukanda wote wa ziwa haufai. Kuna mamba wengi sana na uchawi mkubwa. Ukigusa maji tu umeliwa. Ukitaka kuoga mpaka uombe ruhusa kwa kizee kimoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *