Godbless Lema ‘aichana’ Idara ya Usalama wa Taifa

Jamii Africa

MBUNGE wa Jimbo la Arusha Godbless Lema CHADEMA) ameionya na kuitaka Idara ya Usalama wa Taifa nchini kujifunza kutoka kwa Kiongozi wa Libya Muammar Gadaffi.

Mbali na kuinyoshea vidole Idara hiyo Lema pia amewataka Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha na Kamanda wa Polisi mkoani hapa kutambua kuwa kazi yao si kukitetea Chama cha Mapinduzi (CCM) bali ni kutetea maslahi ya taifa.

“Kama Idara ya Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi wanafikiri wao wana nguvu sana wanapaswa kujua kwamba wanajidanganya. Kama wanataka kujua nguvu zao zina uwezo kiasi gani, wasafiri kwenda kuiuliza Idara ya Kijasusi ya Libya kama ilimsaidia Gadaffi asipinduliwe kwenye nchi aliyoingoza kwa miaka zaidi ya 40,” alidai Lema.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana mjini Arusha Lema alidai taarifa za Kiintelijensia walizonazo zimedhibitishia pasipo shaka kuwa Idara ya Usalama wa Taifa mkoani Arusha inatumika kwenye mgogoro wa Meya.

godbless lema
Godbless Lema akiongea na waandishi

Alidai kuwa mtu anayetuhumiwa kuongoza mpango huo mchafu unaolenga kuwaangamiza viongozi wa kisiasa wa CHADEMA ni Msaidizi wa Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa wa Arusha.

“Vitisho ni vingi hatutaogopa nipo tayari kwa jambo lolote lile sitaacha harakati nipo tayari kufa hata sasa. Taarifa na ushahidi tunao kwamba kila kinachoendelea sasa kwenye siasa kinaratibiwa na Idara hii. Katika kutafuta ufumbuzi wa nchi kuna watu ambao watatolewa sadaka na sisi tupo tayari kutolewa sadaka,” alidai Lema na kuongeza:

“Kuanzia Jumatatu tutaendesha ‘movement’ ambayo hawajawahi kuiona na wakiendelea hivi pengine ukombozi wa nchi unaweza kuanzia Arusha,” alidai.

Katika hatua hiyo Lema aliyataja majina ya baadhi ya viongozi wa CHADEMA ambao wapo kwenye mkakati wa kuhujumiwa wakati wowote na vyombo vya usalama kuwa Ephata Nanyaro ambaye tayari amehojiwa, Joseph Kredo Katibu.

Wengine ni Emanuel Kombe ambaye naye amehojiwa, Hilary Mkonya Mhazina wa Chama, Odelo Odelo Mwenyekiti wa BAVICHA, Kamnde tayari amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kukutwa na silaha aina ya SMG na Bastola,Glory Shio Mwenyekiti wa BAWACHA, Happy Charles, Sarungi, na wengine.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Arusha Ephata Nanyaro kwa upande wake aklibainisha kuwa tayari ameandika maelezo polisi akikanusha kuhusika na kikao cha kupanga njama za kumuua Meya wa Jiji la Arusha Gaudence Lyimo.

“Nimehojiwa kwa zaidi ya Saa 7 tena ni Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha (RCO) akiwa na maofisa kutoka Dar es Salaam makao makuu ya Polisi.

“Katika maelezo yangu bado nilikana sina ugomvi na Gaudence, sijahusika na madai ya kupanga kumuua niliwaambia sintamtambua kamwe kwa nafasi  aliyonayo,” alisema Nanyaro na kuongeza:

“Tunaushahidi katika kuhojiwa kwangu kwamba Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi wanahusika kwani wameonyesha uwazi wa kuwatisha viongozi wa CHADEMA.

“Martine Luther King mwanaharakati wa Kimarekani aliwahi kusema; “Kama hakuna jambo lolote binadamu yupo tayari kufa kwalo huyo binadamu hastahili kuishi”. CHADEMA tuna amini uchaguzi wa Meya Arusha ulikuwa ni batili hilo tutaendelea kuliamini mpaka mwisho,” alidai Nanyaro.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo Arusha (ArDF) Elifuraha Mtoe kwa upande wake alithibitisha kupokea taarifa za kutafutwa na vyombo vya usalama.

“Nimepata habari na ujumbe kwamba ninatafutwa hivi chombo cha usalama kinapokuhitaji kama kina lazimika kumtumia Mwenyekiti wa wilaya CHADEMA. Kama kuna tuhuma zinazonihusu ambazo Usalama wa Taifa wanazo au jeshi la polisi nawaruhusu wanitafute waniulize hii nchi inaendeshwa kwa mujibu wa sheria,” alisema Elifuraha.

Mwenyekiti huyo wa ArDF aliendelea kubainisha kuwa kinachoonekana kwa sasa mkoani Arusha na nchini kwa ujumla ni Idara ya Usalam wa Taifa badala ya kuangalia usalama wan chi inaasimamia matakwa ya chama cha siasa.

“Kuna Kada wa CCM aliwahi kuniambia kuna mambo mabaya yanandaliwa dhidi yangu hivyo aliomba anikutanishe na Msaidizi wa Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa (Mombo) tukae tuzungumze tuyamalize. Kinachoonekana hivi sasa kuna wanasiasa wana nguvu kuliko Dola na Dola hiyo hiyo inajaribu kupambana nao ili kumaliza nguvu za wanasiasa. Sasa inapopambana kutafuta nguvu ya kupambana na wanasiasa hao inaanza kutafuta watu waliopo karibu na wanasiasa,” alidai Elifuraha.

19 Comments
  • Hawa wehu kweli, kama wanafanya ujinga huu basi kuna masuala meeengi sana.

    Jaman hebu tuacheni uzandiki, USALAMA WA TAIFA KWANI NDIO KAZI MLIYOJIFUNZIA NDIO HII? AAAARGH,

  • Mi nawashangaa sana kwa kuendelea kuwaita usalama wa taifa ili hali hao ni usalama wa ccm aka magamba

    • achene ku suport ujinga hivi ni lini tuta pigana na maradhi, umaskini, na ujinga kama kila siku ni sisi wenyewe kwa wenyewe kama tumempa ubunge bac afanye kaziyake na tuone maendeleo ya kiuchumi siasa na jamii na si maandeleo ya machafuko vifo vya maskini na migomo isiyo na msingi….hivi inamaana sisi chadema kila mtu kwetu ni mbaya sasa tutaleta maendeleo kwa nani kama kila anaye fanyakaz serekalini ni mbaya siasa ni sera so vita matusi migomo na ushawishi kwa wasojua wanachoifanya

  • hakuna mwenye nguvu zaidi ya mungu..ccm waendelee na mchezo wao wa kutumia vyombo vya dola wataona mwisho wake.na hao usalama wa taifa wataweka wapi sura zao siku upinzani wakichukua madaraka?

  • We lema acha unafiki mbona unaamua kuyasema hayo baada ya kutuhumiwa kuhusika na mtandao wa wizi wa magari? Tushawashtukia nyote wanafiki tu.Waacheni usalama wa taifa wafanye kazi zao

    • tena pia mimi ni chadema lakini viongozi wa chadema wasi sahau kuwa pia mabaya wanao yafanya yanaonekana live na tulio wachagua kwaiyo usalama wafanye kazi yao tena kwabidii ili tutambue maovuyenu ambayo mnayasiriba na siasa chafu na migomo isiyo na msingi

  • Ninyi chadema wachoyo wa madaraka wakati mkishapewa mwaanza kugombana wenyewe.Mfano mzuri ni ugonvi kati ya madiwani wenu wa mwanza dhidi ya meya wa jiji la mwanza ambaye hata hivyo ni mwana chadema.Acheni kucheza na akili za watanzania,hiyo saikologia mbaya itawaponza hapo baadae

  • Unaonekana ni mmoja wa magamba ambayo tunahitaji kuyavua kwa nguvu , Mwisho wenu umefika we Uishie kutegemea dola ukinyanyasa wananchi subirini muone kama una akili kimbia.

  • Greetings,

    hehehehhehe hii habari kidogo inasikitisha na hii ni dhahiri kuwa serikali na CCM inatumia dola kisiasa zaidi kuliko kiutendaji. Inakuwaje jeshi/ usalama wa Taifa kuhusika na ugomvi wa siasa?

    Mm nafikiri tatizo ni ufahamu mdogo na mfumo duni wa majeshi yetu kama vile polisi JW, n.k kwani wao wnenyewe hawajui kuwa tunachokipigania ni kwa ajili ya matokeo mazuri kwa watu wote? au wanadhani CCM ikianguka basi nao wameanguka? wao ni watumishi wa serikali kupitia majeshi yao hivyo serikali ya chama chochote itawatambua tu.

    Wanaharakati tuna kazi kubwa kuifungua jamii yetu toka kwenye wimbi kuu la umasikini na ujinga uliokithiri. Hii itawezekana tu pale ambapo tutatwaa serikali na uongozi wa nchi yetu kwa watu wanaofahamu ni nini haswa maana ya utumishi wa umma.

    Best Regards,

  • ndugu zangu naomba tujielekeze ktk kuangalia mistakabali wa taifa letu na matatizo makubwa yanayoikumba taifa letu.Hivi mtu mwenye utimamu akili aliopewa na mwenyezi Mungu anaweza kweli kupoteza mda wake ktk kuwinda maisha ya wenzake?mie naomba tusitumike ktk hii mikakati ya hovyo kupita zote,tuyungumzie maswala na si kuzungumzia watu.maana inatakakuonekana hivi sasa kuwa anapoonekana mtu anaibua maswala ya kuisaidia jamii kwa kueleza maovu yanayofanywa na baadhi ya viongozi basi anaanza kusongwasongwa.

  • tangu nikue hapa bongo sijawahi kuona mwanasiasa yeyote bongo ameibuka tu ivivi mm nanona wote hao ni watumishi wa uma ila ndo ivyo

  • Mnaidhalilisha idara kutokana na utaratibu mkongwe mliojijengea wa kurithishana kazi hiyo, matokeo yake kufanya kazi kwa mazoea marehemu baba yake nilifanya naye kazi sehemu fulani, matokeo yake mnakosa mawazo mapya ua mnapitwa na wakati kwa kuifanya idara ka MAFIA MOB.

  • Ukombozi wa Mtanzania dhidi ya wizi,dhuluma na unyanyasaji unaofanywa na Magamba uko njiani. CCM inatumia nguvu zaidi kuliko ukweli ktk kujibu tuhuma walizonazo;wamechoka ndiyo maan hata baba yao hapendi tena kukaa hapa nchini. Your day is coming!!! PEOPLES POWER!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  • dah kama chadema mmeanza vita adi na usalama wataifa kazi kwenu kwani ivi siasa bila kutukana chamakingine kuleta fujo migomo na uchochezi unao pandikizwa kwa watanzania wa hali ya chini tena wasojua hata sheria na katiba nini hivi haiwezekani na nilini tutapata muda wa kufanya maendeleo kama malumbano hayaishi inasikitisha kuona kwamba mbunge wananchi wa arusha walomchagua kuwakilisha maslahi yao ndani ya bunge la jamuhuri eti anatoka nje ya bunge akigoma sasa matatizo yetu yatatatulikaje nje yabunge? sini wewe ulie waambia maaskari kuwa hajui chochote zaidi ya kirungu….alaf haohao ndo wakulinde na dharau zako naskitika kuwa watanzania wa chini ambao wana elimu duni ndo itawapashida kutambua siasa ya kweli na kubaki kuyumbishwa kwenye machafuko yanao sababisha vifo vya watanzania uku viongozi hao wakitoa salam zarambirambi na kuendelea na maisha yao uku wakisisitiza eti marehem kafa kishujaa kumbe ni siasa potofu isiyo na chembe ya usomi ndaniyake

  • ccm waache watu watfute maendeleo na si vitisho visivyokuwa na maana kwa waleta maendeleo. Nani asiyejua umuhimu wa CHADEMA? Tunajua siri iliyopo ni kuwalinda vigogo na watoto wao waendelee kutunyonya bila kupingwa.

  • Kama CCM haikujua hasira za wanyonge isubiri uchaguzi mdogo wa ARUSHA, wanafikiri Tanzania ya leo ni ile ya akina Mangungo? watu wanataka kusoma, matibabu, barabara na si braabraa tupuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu. Hata hivyo MUNGU hakuwapa chapa kututawala kwa nguvu.

  • Kati ya wabunge ambao hawajui wajibu wake ni Lema. Anaacha kutekeleza wajibu wa kuwaletea wananchi wa jimbo lake maendeleo yy anahamasisha vurugu na maandamano. Kwani watu kuhojiwa na polisi ni ajabu au ni sehemu ya wajibu wao. Pia wakati wa kampeni yako mbona hukutuambia kwamba bila meya hatutatawala hili jimbo. Unatuchosha best na siasa za vijiweni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *