Imani za kishirikina na kasi ya malaria Butiama

Stella Mwaikusa

Mganga mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Butiama, Joseph Musagara, amesema imani za kishirikina zimechangia ugonjwa wa malaria kuwa tishio katika wilaya hiyo.

Anasema baadhi ya wagonjwa wanaopatwa na ugonjwa wa malaria hawafiki Hospitali au vituo vya afya kwa haraka, badala yake huenda kwa waganga wa kienyeji wakiamini kwamba wamelogwa.

butiama 2

Akinamama  wakisubiri huduma ya daktari wa watoto. katika hospitali ya Butiama

Anasema baada ya kutibiwa huko na kushindwa kupata nafuu, ndipo hufika hospitali huku hali zao zikiwa mbaya  na wengine wakiwa wameishiwa damu.

Hali hiyo haishii kwa watu wazima tu, kwani hata watoto wao wakiumwa pia hupelekwa kwa waganga wa kienyeji, ni mpaka pale wazazi hao watakapobadili mawazo na kumpeleka mtoto kwenye kituo cha  afya au Hospitali, ambapo mara nyingi huwa wamechelewa na kusababisha vifo vya watoto.

Anasema hawawezi kukiri kama waliwapeleka watoto kwa waganga wa kienyeji,au wao wenyewe walienda kutibiwa huko, lakini chale na baadhi ya dawa walizofungwa mwilini hudhihirisha hilo.

butiama3

Boke Chacha akiwa na watoto wake mapacha katika Hospitali ya Butiama, watoto Vailet Nkwabi na Yosta Nkwabi wote wanaumwa Malaria

Pamoja na kuwepo kwa imani hizo za kishirikina, Musagara alizitaja sababu zingine ambazo zimesababisha malaria kuwa tishio Butiama kuwa ni umbali wa kuzifikia huduma za afya, umasikini na ubovu wa miundombinu ya barabara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *